Quotessence
Home / Quotes / Quote / Image

Quote image editor Enock Maregesi

Back to previous page

“Lakini kuna ndoto takatifu na kuna ndoto za kishetani. Ndoto takatifu hutokea wakati akili imetulia baada ya mwili wote kupumzika, kama ambavyo usiku unavyokuwa kimya na kila kitu kimetulia, karibu na saa za alfajiri, ambapo mfumo wa usagaji chakula unakuwa umemaliza kazi yake. Kipindi hicho malaika wa Mungu hutufunulia siri kuhusu ulimwengu huu, ili kwamba tutakapoamka asubuhi tuwe na baadhi ya maarifa yaliyojificha ndani ya maandiko ya vitabu vitakatifu; kwa sababu malaika wa Mungu ndiye anayetawala ufahamu wetu, kama ambavyo Mungu anavyotawala hiari yetu, na kama ambavyo nyota zinavyotawala miili yetu. Lakini kwa wale waliokomaa kiimani malaika mwema anaweza kuwafunulia siri wakati wowote, haijalishi wamelala au wameamka. Kwa ajili ya ujanja wa Shetani ndiyo maana Mungu hutufunulia siri zake, ili tujihadhari naye.” — Enock Maregesi

Quote 1080 x 1350 Instagram portrait
More
Platforms
Pure ratios
Lakini kuna ndoto takatifu na kuna ndoto za kishetani. Ndoto takatifu hutokea wakati akili imetulia baada ya mwili wote kupumzika, kama ambavyo usiku unavyokuwa kimya na kila kitu kimetulia, karibu na saa za alfajiri, ambapo mfumo wa usagaji chakula unakuwa umemaliza kazi yake. Kipindi hicho malaika wa Mungu hutufunulia siri kuhusu ulimwengu huu, ili kwamba tutakapoamka asubuhi tuwe na baadhi ya maarifa yaliyojificha ndani ya maandiko ya vitabu vitakatifu; kwa sababu malaika wa Mungu ndiye anayetawala ufahamu wetu, kama ambavyo Mungu anavyotawala hiari yetu, na kama ambavyo nyota zinavyotawala miili yetu. Lakini kwa wale waliokomaa kiimani malaika mwema anaweza kuwafunulia siri wakati wowote, haijalishi wamelala au wameamka. Kwa ajili ya ujanja wa Shetani ndiyo maana Mungu hutufunulia siri zake, ili tujihadhari naye.
— Enock Maregesi