Quotessence
Home / Quotes / Quote / Image

Quote image editor Enock Maregesi

Back to previous page

“Msamaha ni uamuzi wa makusudi wa kuachilia hisia za chuki au kisasi juu ya mtu au kikundi cha watu ambaye amekuumiza au ambacho kimekuumiza, bila kujali kama anastahili au kinastahili msamaha wako. Wataalamu wanaosoma au kufundisha msamaha huweka bayana ya kuwa, unaposamehe, hutakiwi kusitiri au kukana uzito wa kosa ulilofanyiwa. Msamaha haumaanishi kusahau wala haumaanishi kupuuza, au kujisingizia, makosa ambayo mtu amekufanyia au kikundi cha watu kimekufanyia. Ijapokuwa msamaha unaweza kusaidia kujenga uhusiano ulioharibika, haukulazimishi kupatana na mtu aliyekukosea au kumfanya asiwajibike kisheria kwa makosa aliyokufanyia. Badala yake, msamaha humletea yule anayesamehe amani ya moyo; na humpa uhuru kutokana na hasira aliyokuwa nayo, juu ya yule aliyemkosea.” — Enock Maregesi

Quote 1080 x 1350 Instagram portrait
More
Platforms
Pure ratios
Msamaha ni uamuzi wa makusudi wa kuachilia hisia za chuki au kisasi juu ya mtu au kikundi cha watu ambaye amekuumiza au ambacho kimekuumiza, bila kujali kama anastahili au kinastahili msamaha wako. Wataalamu wanaosoma au kufundisha msamaha huweka bayana ya kuwa, unaposamehe, hutakiwi kusitiri au kukana uzito wa kosa ulilofanyiwa. Msamaha haumaanishi kusahau wala haumaanishi kupuuza, au kujisingizia, makosa ambayo mtu amekufanyia au kikundi cha watu kimekufanyia. Ijapokuwa msamaha unaweza kusaidia kujenga uhusiano ulioharibika, haukulazimishi kupatana na mtu aliyekukosea au kumfanya asiwajibike kisheria kwa makosa aliyokufanyia. Badala yake, msamaha humletea yule anayesamehe amani ya moyo; na humpa uhuru kutokana na hasira aliyokuwa nayo, juu ya yule aliyemkosea.
— Enock Maregesi