“Meli ya kwanza kuondoka katika Bandari ya Salina Cruz kusini mwa Meksiko katika Bahari ya Pasifiki ni 'La Diosa de los Mares', 'Mungu wa Bahari', au 'Goddess of the Seas', Tani 6000, iliyoondoka saa tisa kamili usiku kuelekea Miami nchini Marekani; wakati ya mwisho kuondoka ilikuwa CSS ('Colonia Santita of the Seas', Tani 10000), na SPD ('El Silencio Depredador del Profundo', 'Mnyama Mtulivu wa Kina Kirefu', 'The Silent Predator of the Deep' – nyambizi ya Panthera Tigrisi), zilizoondoka saa kumi na moja alfajiri kuelekea Guatemala na Kolombia. Salina Cruz ni sehemu iliyopo kandokando mwa Bahari ya Pasifiki kusini kabisa mwa Meksiko na kaskazini-mashariki kwa Reparo Jicara katika jimbo la Oaxaca. Kambi ya Panthera Tigrisi ilijengwa ndani ya Msitu wa Benson Bennett – katika ufuko wa bahari kubwa kuliko zote ulimwenguni, iliyopuliza hewa na kuyumbisha miti anuai juu ya maabara kubwa kuliko zote katika Hemisifia ya Magharibi; ya kokeini, heroini, bangi, eksitasi na hielo ya China na Kolombia. Panthera Tigrisi alikamatwa katika Bahari ya Pasifiki. Kahima Kankiriho alikamatwa katika Msitu wa Bennett.” AmericaChinaEcstasyMarijuanaMexicoCocaineHeroinMiamiColombiaShipPacific OceanGuatemalaMethamphetamineCssMeksikoSubmarineOaxacaPanthera TigrisiSalina CruzHarborMarekaniBangiHieloKolombiaMeliMsitu Wa Benson BennettBenson BennettEksitasiKahima KankirihoMethamfetaminiSpd10000 Tons6000 TonsBahari Ya PasifikiBandariColonia Santita Of The SeasGoddess Of The SeasGwatemalaHemisifia Ya MagharibiHeroiniKokeiniLa Dios De Los MaresMnyama Mtulivu Wa Kina KirefuMungu Wa BahariNyambiziReparo JicaraShumuyaTani 10000Tani 6000The Silent Predator Of The DeepWestern Hemisphere Author:Enock Maregesi