“Mungu ni baba yetu wa kiroho. Hivyo basi, tunajua ya kuwa upendo wake umehifadhiwa ndani ya mioyo yetu. Kwa hiyo, kila mtu ana upendo wa ‘agape’ kwa kiasi fulani; lakini si upendo kamili. Upendo wa ‘agape’ kati ya binadamu na binadamu unahusiana na upendo wa kujitolea kwa ajili ya binadamu wengine. Kila mtu ana kiasi fulani cha upendo huo. Mtu akitaka awe na upendo kamili wa ‘agape’ sharti awe mtiifu na mnyenyekevu mbele za Mungu, na mbele ya binadamu wenzake, sharti ampende Mungu, na sharti ampende jirani yake kama anavyoipenda nafsi yake mwenyewe.” GodMunguHuman BeingAgape LoveBinadamuOur HeartsUpendo Wa AgapeMioyo Yetu Author:Enock Maregesi
“Nyerere alikuwa na upendo wa AGAPE, lakini kwa sababu alikuwa binadamu hakuutumia upendo huo kikamilifu.” NyerereUpendo Wa AgapeUpendo Love Author:Enock Maregesi
“Kuna aina tatu za upendo hapa ulimwenguni. Kuna upendo wa ‘agape’, upendo kati ya Mungu na binadamu na kati ya binadamu na binadamu mwenzake lakini hao binadamu shuruti wawe marafiki wa msalaba wa Yesu Kristo. Aidha kuna upendo wa ‘phileo’, upendo kati ya mtu na mtu au kati ya mtu na kitu au kati ya mtu na jambo; na kuna upendo wa ‘philadelphia’, upendo wa wanachama wa mashirika ya siri ambapo mtu humpenda mwenzake kama ndugu yake wakati si ndugu yake. Heri upendo wa ‘agape’ kuliko upendo ajmaina.” Jesus ChristAllAgape LoveYesu KristoUpendo Wa AgapeAjmainaPhiladelphia LovePhileo LoveUpendo Wa PhiladelphiaUpendo Wa Phileo Author:Enock Maregesi
“Mwalimu Julius Kambarage Nyerere alikuwa na sehemu ya upendo wa AGAPE. Alijitahidi kuwapenda wengine kuliko yeye na familia yake.” FamilyOthersFamiliaAgape LoveWengineMwalimu Julius Kambarage NyerereUpendo Wa Agape Author:Enock Maregesi