“Wakati Ford Bronco inatoka katika Kiwanda cha Dongyang Pharmaceuticals S.A de C.V. (kilichomilikiwa na mkurugenzi mkuu wa 'methamphetamine' wa Kolonia Santita mfanyabiashara wa Kichina kutoka Chaling, katika jimbo la Hunan, kusini ya kati ya China, Li Dongyang; na mkurugenzi wa usalama wa Kolonia Santita kutoka Lomas de Chapultepec, Mexico City, Gortari Manuel) Daniel Yehuda na Radia Hosni, waliokuwa wakipiga picha kila kitu kilichokuwa kikiingia na kutoka kiwandani kwa ajili ya ripoti ya upelelezi wao ya baadaye, waliiona. Lakini, hawakujua kama ilikuwa ikienda Varsovia kumuua Murphy na Sajini Mogens. Bronco ilipofika Varsovia ilisimama kwa fujo mbele ya SUV ya msafara wa Mtoto wa Rais Debbie Patrocinio Abrego, aliyekuwa ndani ya Mgahawa wa Angus akicheza muziki wa 'mariachi' na John Murphy, huku Mogens akilinda usalama wa kamanda wake na usalama wa baa nzima. Kabla majambazi wa Kolonia Santita hawajaleta madhara au fujo yoyote kwa Vijana wa Tume, polisi walifika eneo lile haraka ilivyowezekana! Kwa msaada wa walinzi wa Debbie! Wale majambazi walipekuliwa na kukutwa na bastola moja ya Akdal Ghost, bunduki mbili za AK-47, na picha nne za Vijana wa Tume ndani ya gari yao. Polisi waliwakamata na kuwapeleka katika kituo cha polisi cha Tume ya Dunia kilichopo Zona Rosa, Mexico City.”
Quote by Enock Maregesi
Author
You May Also Like
Source: Lessons in Truth
“I always assume that anyone who approaches me in the USA has a gun.”
“Shouting ‘Gun! Gun! Gun!’ is a police officers license to kill.”
Source: The Builders
“You do not want to be holding a legally owned gun when the police are around.”
“I have lived in the USA for over two decades and no one has ever pointed a gun at me.”
“Owning a gun puts your risk of illegally killing a person much higher.”
Source: The Zodiac Quest: A LitRPG Adventure