“Kila mmoja wetu ana kitu cha kutoa. Wengine wana pesa, wengine wana vipaji, wengine wana muda. Vipaji vyote tulivyopewa na Mungu, vikubwa au vidogo, hatuna budi kuvitumia kiukarimu kwa watu wanaovihitaji. Tunapofanya hivyo tunaleta mabadiliko katika dunia kwa ajili ya watu fulani, na tunapata maana halisi ya maisha na toshelezo la moyo katika maisha yetu.” PeopleWorldLifeHeartGodTimeMoneySatisfactionTalentsGiveChangesOthersMunguTrue MeaningDuniaMaishaWatuPesaMoyoMudaWengineVipajiMabadilikoEvery One Of UsMaana HalisiKila Mmoja WetuKutoaToshelezo Author:Enock Maregesi
“Kuna ndoto za mchana na kuna ndoto za usiku. Ndoto za mchana ni maono ya kile ambacho roho inatamani kuwa. Ndoto za usiku ni maono yanayotokea wakati akili imetulia baada ya mwili wote kupumzika. Ukiota kuhusu moto, hiyo ni ishara ya hasira; ukiota kuhusu maji, hiyo ni ishara ya siri; ukiota kuhusu ardhi, hiyo ni ishara ya huzuni; ukiota kuhusu Yesu, hiyo ni ishara ya mafanikio. Kitu cha kwanza kufanya unapoota ndoto za kishetani, utakapoamka, mwombe Mungu akunusuru kutoka katika matatizo yoyote yanayokunyemelea; au yanayomnyemelea mtu mwingine yoyote yule, hata usiyemjua. Ubongo ni kitu cha ajabu kuliko vyote ulimwenguni na umetengenezwa na Mungu. Ndoto zinapatikana ndani ya ubongo. Ubongo unapatikana ndani ya ufahamu. Ufahamu mtawala wake ni malaika mwema. Malaika mwema anajua siri ya ndoto. Kila mtu anaota na kila ndoto ina maana yake. Rekodi ndoto zako kila siku kwa angalau mwezi mzima kupata maana halisi ya ndoto hizo, na kujua kwa nini ulizaliwa.” MindGodBodySuccessSpiritJesusWaterSecretBrainConsciousnessFireDreamsSorrowAngerProblemsPersonVisionsMunguGroundMtuRecordYesuMatatizoDaydreamsMafanikioSiriAkiliMwiliRohoHasiraMajiNdotoUbongoMaonoUfahamuArdhiGood AngelHuzuniMalaika MwemaMotoNight DreamsMaana HalisiNdoto Za KishetaniReal MeaningRekodiSatanic DreamsKwa Nini UlizaliwaMwezi MzimaNdoto Za MchanaNdoto Za UsikuWhole MonthWhy You Were Born Author:Enock Maregesi