“Radia Hosni, mhitimu wa mikanda miwili myeusi ya sanaa za mapigano za kareti na kung’fu katika ngazi ya dani mbili za kung’fu na dani moja ya kareti, mwanajeshi wa Tunisia aliyepata mafunzo ya kawaida ya kijeshi nchini Ufaransa na mafunzo ya kikomandoo nchini Uingereza kabla ya kujiunga na Tume ya Dunia, alikuwa mshindi wa tuzo ya shujaa wa taifa la Tunisia. Hussein Kashoggi alipokuwa akiwasili Tunis kutokea Copenhagen, Radia alikuwa katika Uwanja wa Mpira wa El Menzah akiangalia mechi kati ya Stade Tunisien na Espérance ST – timu ambayo mchumba wake Fathi Meoki alikuwa kocha msaidizi. Fujo zilipozuka, baada ya Stade Tunisien kufungwa bao moja kwa sifuri na Espérance ST, Radia alipanda Quadrifoglio na kuondoka kuelekea Uwanja wa Ndege wa Tunis-Carthage; ambapo alimpokea Hussein Kashoggi na jambazi wa Kolonia Santita, Delfina Moore.” FranceKarateKung FuBlack BeltDanTunisiaCopenhagenAwardDaniTume Ya DuniaTunisNational HeroAlfa RomeoWorld CommissionMartial ArtRadia HosniUingerezaWodeaDelfina MooreMilitary OfficerUfaransaWodecAssistant CoachCommando TrainingEspérance StFathi MeokiHussein KashoggiJambazi Wa Kolonia SantitaKaretiKocha MsaidiziKolonia Santita Special AgentMafunzo Ya KikomandooMkanda MweusiMwanajeshiNational Hero Of TunisiaQuadrifoglioSanaa Ya MapiganoShujaa Wa TaifaShujaa Wa Taifa La TunisiaStade Olympique El MenzahStade TunisienTunis Carthage AirportTuzoUnited KindomUwanja Wa Mpira Wa El Menzah Author:Enock Maregesi