“Mbegu ni neno la Mungu. Mfano bora, msamaha, ndoto, tabasamu, uadilifu, uaminifu, uchapakazi na uvumilivu ni maneno ya Mungu. Kwa hiyo mfano bora, msamaha, ndoto, tabasamu, uadilifu, uaminifu, uchapakazi na uvumilivu ni mbegu. Watu ni ardhi. Panda mbegu ya mfano bora kwa watoto wako, msamaha kwa maadui zako, ndoto kwa malengo yako, tabasamu kwa marafiki zako, uadilifu kwa waajiri wako na kwa wafanyakazi wako pia kama unao, uaminifu kwa marafiki zako wa ukweli, uchapakazi kwa kazi zako na uvumilivu kwa wapinzani wako. Kila mbegu irutubishwe kwa imani na upendo kwa watu.” ChildrenForgivenessSeedsWord Of GodEnemiesWatotoMsamahaMaaduiMbeguNeon La Mungu Author:Enock Maregesi
“Mbegu ni neno la Mungu na kudondoka kwake kwenye ardhi si mwisho wa maisha yake. Mambo kadha wa kadha yanaweza kutokea yanayoweza kuathiri ukuaji wa mbegu husika. Nyingine zinaweza kuanguka karibu na njia ndege wakaja wakazila, nyingine zinaweza kuanguka penye miamba pasipokuwa na udongo mwingi wa kutosha, nyingine zinaweza kujifukia ndani kabisa ya ardhi na kupotelea huko kwa miaka mingi, mvua inaweza kunyesha na kuhamisha baadhi ya mbegu kwa kuzisomba na maji. Lakini kwa kuwa maisha yamo ndani ya mbegu, jambo fulani litatokea.” WaterSeedsSoilWord Of GodGroundMajiMbeguUdongoArdhiNeon La Mungu Author:Enock Maregesi
“Mitume wa Yesu Kristo wakati wanahubiri injili hawakuwa na Roho Mtakatifu, walikuwa hata bado hawajaongoka, lakini walikuwa na idhini maalumu kutoka kwa Mungu ya kuhubiri Neno la Mungu. Neno la Mungu halihubiriwi kwa nguvu zetu sisi wenyewe bali linahubiriwa kwa nguvu za Mungu kutokana na utii kwa uongozi wake.” GodHoly SpiritWord Of GodMunguRoho MtakatifuNeon La MunguApostles Of Jesus ChristHis LeadershipMitume Wa Yesu KristoUongozi Wake Author:Enock Maregesi