Quotessence
Home / Topics / Udongo Quotes

Udongo Quotes

Browse 6 quotes about Udongo.

Udongo Quotes

“Roho haina mifumo ya ufahamu! Haina pua, haina macho, haina ladha, haina harufu wala haina masikio. Kwa sababu roho haina mifumo ya ufahamu mtu, anapokufa mifumo yake yote 21 aliyokuwa nayo binadamu huoza na kuwa udongo. Hivyo, kuongea na mtu aliyekufa ni sawa na kuongea na udongo ukitegemea udongo huo ukusikie au uongee na wewe.”

“Nyota ni kipaji, kipawa, takdiri, karama, au uweza; ni kiashiria cha rohoni kinachoonyesha mtu atakuwa nani baadaye, mafanikio ya mtu, au takdiri ya maisha ya mwanadamu. Unabii na nyota ya ufalme ni kibali cha Mungu katika maisha ya mtu. Kupata kibali hicho, tembea na watu sahihi katika maisha yako (tembea na watu ambao Mungu amekuchagulia kushika funguo za takdiri ya maisha yako). Tamka na kukiri kibali cha Mungu katika maisha yako yote. Panda mbegu za kibali cha Mungu katika udongo wa maisha yako. Jifunze kutenda mema bila malipo, kwani wema ni mbegu ya kibali cha Mungu. Jali mambo ya ufalme wa Mungu.”

“Mbegu ni neno la Mungu na kudondoka kwake kwenye ardhi si mwisho wa maisha yake. Mambo kadha wa kadha yanaweza kutokea yanayoweza kuathiri ukuaji wa mbegu husika. Nyingine zinaweza kuanguka karibu na njia ndege wakaja wakazila, nyingine zinaweza kuanguka penye miamba pasipokuwa na udongo mwingi wa kutosha, nyingine zinaweza kujifukia ndani kabisa ya ardhi na kupotelea huko kwa miaka mingi, mvua inaweza kunyesha na kuhamisha baadhi ya mbegu kwa kuzisomba na maji. Lakini kwa kuwa maisha yamo ndani ya mbegu, jambo fulani litatokea.”

“Katika karne iliyopita, wanaakiolojia waligundua mbegu za pamba na ngano katika baadhi ya makaburi waliyokuwa wakiyafukua kwa ajili ya utafiti wao wa kisayansi. Mbegu hizo, zilizokadiriwa kuwa na umri wa kuanzia miaka 2000 hadi 4000, zilimea na kukua zilipopandwa katika udongo sahihi wenye rutuba. Roho ya maisha ilikuwa bado imo ndani ya mbegu hizo, pamoja na kwamba zilikosa mvua na jua kwa zaidi ya miaka 2000. Huu ni uthibitisho kwamba kama mbegu itapandwa, itamea na kukua kama itapandwa katika udongo sahihi wenye rutuba. Matumizi sahihi, watu ni ardhi na mazingira yetu na kile tunachokifanya baada ya kupanda mbegu ni neno la ukweli ambalo ndani yake kuna kanuni na mafundisho ya Mungu, ndicho kinachoathiri matumizi ya mbegu.”