“Familia yako haikusaidii chochote katika mipango ya takdiri yako. Hii inasikitisha sana. Unajitahidi kila siku kuwafurahisha watu unaowapenda na watu wako wa karibu. Kila ukijitahidi kupata kibali cha watu unaishia kudharaulika na kuonekana mjinga asiyekuwa na maana. Sikiliza mazungumzo ya ndani ya moyo wako. Wapendwa wako watakukubali kama mtu hodari asiyekata tamaa, na tena watakuheshimu kutokana na tabia zako hizo. Mabadiliko haya ya kifikra hayatatokea haraka kama unavyofikiria. Yatachukua muda. Hivyo, kuwa mvumilivu. Wakati huohuo, endelea kucheza ngoma uliyoianzisha mwenyewe, endelea na mipango yako kama akili yako inavyokutuma.” PeopleTimeFamilyDestinyFoolRespectPatienceBraveLoved OnesApprovalListen To Your HeartFamiliaInstinctsWatuQualitiesAkiliDrumMudaHeshimaEndeavorsTabiaTakdiriUvumilivuKibaliMipangoMjingaChange Of AttitudeHodariMabadiliko Ya KifikraNgomaWapendwa Author:Enock Maregesi
“Nyota ni kipaji, kipawa, takdiri, karama, au uweza; ni kiashiria cha rohoni kinachoonyesha mtu atakuwa nani baadaye, mafanikio ya mtu, au takdiri ya maisha ya mwanadamu. Unabii na nyota ya ufalme ni kibali cha Mungu katika maisha ya mtu. Kupata kibali hicho, tembea na watu sahihi katika maisha yako (tembea na watu ambao Mungu amekuchagulia kushika funguo za takdiri ya maisha yako). Tamka na kukiri kibali cha Mungu katika maisha yako yote. Panda mbegu za kibali cha Mungu katika udongo wa maisha yako. Jifunze kutenda mema bila malipo, kwani wema ni mbegu ya kibali cha Mungu. Jali mambo ya ufalme wa Mungu.” PeopleLifeSuccessDestinyTalentKeysHumanSeedsGoodGiftManSoilGoodsProphecyStarMaishaWatuMtuGod S PowerMafanikioRight PeopleKipajiMemaMbeguWemaNyotaTakdiriUdongoUnabiiMwanadamuWatu SahihiFunguoGod S ApprovalGracious GiftKaramaLive Like A KingNyota Ya UfalmeKibali Cha MunguKipawaUweza Author:Enock Maregesi
“Usipobadilisha maisha yako kuelekea kwenye takdiri yako utaishi kama Shetani anavyotaka, si kama Mungu anavyotaka.” DestinyTakdiriAs God WantsAs Satan WantsIf You Do Not Change Your LifeKama Mungu AnavyotakaKama Shetani AnavyotakaUsipobadilisha Maisha Yako Author:Enock Maregesi
“Katika maisha watu wengi hawataki kukuona ukiendelea kwa sababu ukiendelea unakuwa kioo kwao. Ghafla wataanza kukutazama. Wanajua wana akili kama wewe, wamesoma kama wewe, au wana akili kuliko wewe, au wamesoma kuliko wewe, na labda wanazijua sifa zako za udhaifu na sifa zako za ushupavu toka utotoni kwako. Lakini ghafla unakuwa kioo, na wanapojitazama katika hicho kioo, wanajiona taswira zao isipokuwa sasa hawapo mahali ambapo wewe upo. Katika maisha watu watakushauri, watakufitini, watakurubuni na watakukatisha tamaa. Sema hapana kwa ndiyo nyingi kwa sababu hawaoni unachokiona, hawajui unachokifanya na hawajui unapoelekea. Unachokiona ni takdiri ya maisha yako, unachokifanya ni kupanda mbegu na kuzimwagilia kwa imani, na unapoelekea ni kileleni. Hivyo, songa mbele, kuwa wewe daima, wape muda, wape nafasi.” PeopleLifeFaithDestinyAdviceIntelligenceContemptIntrigueSummitDiscouragingYour LifeMirrorPlaceMove ForwardMaishaImagesWatuSowing SeedsSay NoImaniAkiliMaisha YakoTakdiriSema HapanaTaswiraA Lot Of YesesKiooMahaliNdiyo NyingiUshauriFitinaKukatisha TamaaKurubuniSonga MbeleBe You AlwaysGive Them SpaceGive Them TimeKileleKupanda MbeguKuwa Wewe DaimaSifa Zako Za UdhaifuSifa Zako Za UshupavuWape MudaWape NafasiYour StrengthsYour Weaknesses Author:Enock Maregesi
“Mtu akikushauri kufanya kitu ambacho ni kinyume na takdiri ('destiny') ya maisha yako, hata kama huyo mtu hana nia mbaya na wewe, sema 'hapana' kwa hiyo 'ndiyo' yake.” LifeDestinyAdviceManYouYour LifeMaishaMtuSay NoWeweMaisha YakoTakdiriSema HapanaUshauriBad IntentionNia MbayaHer YesHis YesNdiyo Yake Author:Enock Maregesi
“Mungu akikuweka mahali unapostahili kuwa, kulingana na takdiri ya maisha yako, hakuna mtu mwenye uwezo wa kushindana na kipaji chako.” LifeGodAbilityDestinyTalentPersonPlaceMunguMaishaMtuUwezoKipajiTakdiriMahali Author:Enock Maregesi