“Unabii ni uwezo alionao mtu wa kuongea mambo matakatifu ya Mungu, kuwaongoza wenzake katika njia njema. Mungu humwambia nabii kitu cha kusema na nabii huwambia wenzake kile ambacho Mungu amemwambia aseme. Mungu hawezi kuongea na watu mpaka watu wajue jinsi ya kuongea naye, na wakati mwingine ni rahisi sana kusikia ujumbe kutoka kwa mtu kuliko kuusikia ujumbe huo moja kwa moja kutoka kwa Mungu. Mungu anaweza kukwambia useme kitu fulani kwa mtu au watu fulani. Unaweza usijue kwa nini anakwambia ufanye hivyo, lakini utajisikia msukumo wa hali ya juu wa kutangaza ujumbe uliopewa kuuwasilisha. Mungu hatakulazimisha, lakini atakung’ang’aniza, na ni Mungu pekee anayejua lengo la mawasiliano hayo. Mungu akikwambia ufanye kitu fanya mara moja, usiulize kwa nini. Kazi yako ni kufanya unachotakiwa kufanya, kusema unachotakiwa kusema, si kuuliza maswali. Mtumie rafiki yako wa kiroho kukuongoza katika mema na mabaya, na usitambe – kwamba unaongea maneno uliyoambiwa na Mungu uyaongee. Ukiwa na uwezo mkubwa wa kuongea na Mungu utaleta mabadiliko katika dunia.” PeopleWorldGodEvilChangePowerCommunicationGoodProphetProphecyMunguMessageDuniaWatuUrgeUwezoMabayaMemaMabadilikoUnabiiUjumbeMawasilianoMsukumoNabii Author:Enock Maregesi
“Nyota ni kipaji, kipawa, takdiri, karama, au uweza; ni kiashiria cha rohoni kinachoonyesha mtu atakuwa nani baadaye, mafanikio ya mtu, au takdiri ya maisha ya mwanadamu. Unabii na nyota ya ufalme ni kibali cha Mungu katika maisha ya mtu. Kupata kibali hicho, tembea na watu sahihi katika maisha yako (tembea na watu ambao Mungu amekuchagulia kushika funguo za takdiri ya maisha yako). Tamka na kukiri kibali cha Mungu katika maisha yako yote. Panda mbegu za kibali cha Mungu katika udongo wa maisha yako. Jifunze kutenda mema bila malipo, kwani wema ni mbegu ya kibali cha Mungu. Jali mambo ya ufalme wa Mungu.” PeopleLifeSuccessDestinyTalentKeysHumanSeedsGoodGiftManSoilGoodsProphecyStarMaishaWatuMtuGod S PowerMafanikioRight PeopleKipajiMemaMbeguWemaNyotaTakdiriUdongoUnabiiMwanadamuWatu SahihiFunguoGod S ApprovalGracious GiftKaramaLive Like A KingNyota Ya UfalmeKibali Cha MunguKipawaUweza Author:Enock Maregesi
“Kila mtu kabla ya kuzaliwa alipewa na Mwenyezi Mungu unabii na nyota ya ufalme. Una bahari ya fursa ya kuwa kitu chochote unachotaka kuwa katika dunia hii. Kama unataka furaha, furaha iko ndani yako. Kama unataka utajiri, utajiri uko ndani yako. Kama unataka amani, amani iko ndani yako. Kama wewe ni tone na fursa ni bahari, wewe ni bahari ndani ya tone.” WorldGodHappinessOpportunityPeaceWealthOceanToneProphecyWillpowerMunguDuniaAmaniDropMwenyezi MunguGod AlmightyUtajiriFurahaUnabiiFursaBahariBahari Ndani Ya ToneLive Like A KingNyota Ya UfalmeMoyo Wa KuthubutuOcean In The DropUtashiWewe Ni Bahari Ndani Ya ToneYou Are The Ocean In The Drop Author:Enock Maregesi
“Kuna sababu za msingi na za kinabii za damu na maji vilivyotoka katika mbavu za Yesu Kristo msalabani. Ubavu wake uliochomwa na mkuki ulithibitisha kifo chake cha kibinadamu, huku vingine vyote vikitimiza unabii wake uliotajwa na Yohana.” DeathProphecyCrossJohnKifoSpearBlood And WaterMkukiDamu Na MajiMsalabaniUnabiiYohanaJesus Christ S RibsMbavu Za Yesu Kristo Author:Enock Maregesi
“Mungu humwambia mtu kitu cha kusema na mtu huwambia wenzake kile ambacho Mungu amemwambia aseme. Lakini utajuaje kama Mungu amekuchagua wewe kusema au kufanya kitu? Mungu atakwambia kupitia Roho Mtakatifu, na utajisikia msukumo mkubwa wa kusema au kufanya kile ambacho Mungu anataka useme au ufanye. Unabii unaweza kumtokea mtu yoyote, mahali popote, anayejua jinsi ya kuwasiliana na Mungu.” GodCommunicationManHoly SpiritProphecyMunguMtuUrgeRoho MtakatifuUnabiiMawasilianoMsukumo Author:Enock Maregesi