“Mtu akikuita mjinga au mpumbavu juu ya maisha yako usikasirike kwa sababu wewe si mjinga wala mpumbavu. Sema hapana kwa ndiyo nyingi kwa sababu hawapaswi kuingilia mambo ya mtu mwingine bila idhini ya Mwenyezi Mungu. Kuingilia mambo ya mtu mwingine bila idhini ya Mwenyezi Mungu ni dhambi, tena dhambi kubwa, ni kuvunja amri kuu ya kwanza ya Mungu.” SinFoolishIdiotAlmighty GodSay NoDhambiMwenyezi MunguSema HapanaMjingaMpumbavu Author:Enock Maregesi
“Katika maisha watu wengi hawataki kukuona ukiendelea kwa sababu ukiendelea unakuwa kioo kwao. Ghafla wataanza kukutazama. Wanajua wana akili kama wewe, wamesoma kama wewe, au wana akili kuliko wewe, au wamesoma kuliko wewe, na labda wanazijua sifa zako za udhaifu na sifa zako za ushupavu toka utotoni kwako. Lakini ghafla unakuwa kioo, na wanapojitazama katika hicho kioo, wanajiona taswira zao isipokuwa sasa hawapo mahali ambapo wewe upo. Katika maisha watu watakushauri, watakufitini, watakurubuni na watakukatisha tamaa. Sema hapana kwa ndiyo nyingi kwa sababu hawaoni unachokiona, hawajui unachokifanya na hawajui unapoelekea. Unachokiona ni takdiri ya maisha yako, unachokifanya ni kupanda mbegu na kuzimwagilia kwa imani, na unapoelekea ni kileleni. Hivyo, songa mbele, kuwa wewe daima, wape muda, wape nafasi.” PeopleLifeFaithDestinyAdviceIntelligenceContemptIntrigueSummitDiscouragingYour LifeMirrorPlaceMove ForwardMaishaImagesWatuSowing SeedsSay NoImaniAkiliMaisha YakoTakdiriSema HapanaTaswiraA Lot Of YesesKiooMahaliNdiyo NyingiUshauriFitinaKukatisha TamaaKurubuniSonga MbeleBe You AlwaysGive Them SpaceGive Them TimeKileleKupanda MbeguKuwa Wewe DaimaSifa Zako Za UdhaifuSifa Zako Za UshupavuWape MudaWape NafasiYour StrengthsYour Weaknesses Author:Enock Maregesi
“Mtu akikushauri kufanya kitu ambacho ni kinyume na takdiri ('destiny') ya maisha yako, hata kama huyo mtu hana nia mbaya na wewe, sema 'hapana' kwa hiyo 'ndiyo' yake.” LifeDestinyAdviceManYouYour LifeMaishaMtuSay NoWeweMaisha YakoTakdiriSema HapanaUshauriBad IntentionNia MbayaHer YesHis YesNdiyo Yake Author:Enock Maregesi
“Katika maisha watu watakufitini, watakurubuni na watakukatisha tamaa. Sema hapana kwa ndiyo nyingi.” PeopleLifeContemptIntrigueDiscouragingMaishaWatuSay NoSema HapanaA Lot Of YesesNdiyo NyingiFitinaKukatisha TamaaKurubuni Author:Enock Maregesi