“Kolonia Santita imesambaa dunia nzima. Hapa Meksiko wana magenge rafiki zaidi ya mia moja yakiwemo makubwa kabisa katika Latino ya Matamolos na Baja California. Nikitekwa nyara na memba yoyote wa magenge hayo, kuna uwezekano mkubwa wasinifanye chochote au nisilipe chochote kwa sababu ya Wanda. Fadhila ya uhalifu. Kwa sababu ya fadhila ya uhalifu; baba, au viongozi wengine wa serikali ambao watoto wao wamo ndani ya 'mpango' huo, wanatakiwa wawakingie kifua (kwa namna yoyote wanayoweza) pindi wanapoanguka katika mikono ya dola na sheria. Wasipofanya hivyo kutakuwa na vita ya ndani kwa ndani … kama unanielewa. Hivyo, kuna mtu anaitwa El Tigre – baba yake Wanda – ndiye ninayetaka unisaidie. Amemuua Marciano, na watu wengi wa Meksiko. Nataka kumlipia kisasi Marciano, na marafiki zangu wengi ambao El Tigre amewaua, hata kwa njia isiyodhahiri.” ChildrenWarFatherCrimeFriendsVitaLatinoBabaDuniaKolonia SantitaWatotoJohn Murphy AmbilikileWandaMeksikoSheriaMarafikiEl TigreDunia NzimaKisasiBaja CaliforniaDolaMarcianoMpelelezi Wa Tume Ya DuniaMtoto Wa Rais Wa MeksikoUhalifuBaba Yake WandaDebbie Parocinio AbregoFadhila Ya UhalifuMatamolosWanda S Dad Book:Kolonia Santita Source: Kolonia Santita
“Mpelelezi wa Tume ya Dunia kutoka Jerusalem, Israeli, Kanali Daniel 'Yehuda Ben-Asher' Ebenezer, Daniel Yehuda, alikuwa komandoo wa kitengo cha mauti na utekaji nyara cha Shirika la Kijasusi la Mossad la Israeli (Kidon) kabla ya kujiunga na Kikosi Maalumu cha Kikomandoo cha Tume ya Dunia (EAC) huko Oslo, kwa makubaliano maalumu kati ya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa (UNSC) na Shirika la Kijasusi la Mossad la Israeli.” IsraelIsraeliJerusalemOsloMossadUnscCommandoUnited Nations Security CouncilDaniel YehudaEacKomandooMpelelezi Wa Tume Ya DuniaExecutive Action CorpsKidonWodec Special AgentWodec Special ForceWorld Commission Special AgentWorld Commission Special Force Author:Enock Maregesi
“Mpenzi. Sikiliza. Magaidi yaliyomuua Marciano yana mtandao dunia nzima na watu wote wanayajua. Yanaitwa Kolonia Santita. Tatizo hata hivyo ni moja: Hakuna mtu amewahi kuthibitisha au kutoa ushuhuda wa uhalifu wao ili watiwe nguvuni. Huendesha maisha yao kibabe na yana kila mbinu ya kukwepa sheria, ndani na nje ya Meksiko. Watu wengi wameuwawa kwa sababu ya Kolonia Santita. Ukileta kidomodomo yanakuua; au yanakupa notisi ya kuhama mji au nchi, ukakae mbali na Meksiko au Mexico City.” MexicoDuniaMexico CityKolonia SantitaJohn Murphy AmbilikileDebbie Patrocinio AbregoMeksikoDunia NzimaMarcianoMpelelezi Wa Tume Ya DuniaMtoto Wa Rais Wa MeksikoMtandaoNotisi Book:Kolonia Santita Source: Kolonia Santita