“Kolonia Santita imesambaa dunia nzima. Hapa Meksiko wana magenge rafiki zaidi ya mia moja yakiwemo makubwa kabisa katika Latino ya Matamolos na Baja California. Nikitekwa nyara na memba yoyote wa magenge hayo, kuna uwezekano mkubwa wasinifanye chochote au nisilipe chochote kwa sababu ya Wanda. Fadhila ya uhalifu. Kwa sababu ya fadhila ya uhalifu; baba, au viongozi wengine wa serikali ambao watoto wao wamo ndani ya 'mpango' huo, wanatakiwa wawakingie kifua (kwa namna yoyote wanayoweza) pindi wanapoanguka katika mikono ya dola na sheria. Wasipofanya hivyo kutakuwa na vita ya ndani kwa ndani … kama unanielewa. Hivyo, kuna mtu anaitwa El Tigre – baba yake Wanda – ndiye ninayetaka unisaidie. Amemuua Marciano, na watu wengi wa Meksiko. Nataka kumlipia kisasi Marciano, na marafiki zangu wengi ambao El Tigre amewaua, hata kwa njia isiyodhahiri.” ChildrenWarFatherCrimeFriendsVitaLatinoBabaDuniaKolonia SantitaWatotoJohn Murphy AmbilikileWandaMeksikoSheriaMarafikiEl TigreDunia NzimaKisasiBaja CaliforniaDolaMarcianoMpelelezi Wa Tume Ya DuniaMtoto Wa Rais Wa MeksikoUhalifuBaba Yake WandaDebbie Parocinio AbregoFadhila Ya UhalifuMatamolosWanda S Dad Book:Kolonia Santita Source: Kolonia Santita
“Mpenzi. Sikiliza. Magaidi yaliyomuua Marciano yana mtandao dunia nzima na watu wote wanayajua. Yanaitwa Kolonia Santita. Tatizo hata hivyo ni moja: Hakuna mtu amewahi kuthibitisha au kutoa ushuhuda wa uhalifu wao ili watiwe nguvuni. Huendesha maisha yao kibabe na yana kila mbinu ya kukwepa sheria, ndani na nje ya Meksiko. Watu wengi wameuwawa kwa sababu ya Kolonia Santita. Ukileta kidomodomo yanakuua; au yanakupa notisi ya kuhama mji au nchi, ukakae mbali na Meksiko au Mexico City.” MexicoDuniaMexico CityKolonia SantitaJohn Murphy AmbilikileDebbie Patrocinio AbregoMeksikoDunia NzimaMarcianoMpelelezi Wa Tume Ya DuniaMtoto Wa Rais Wa MeksikoMtandaoNotisi Book:Kolonia Santita Source: Kolonia Santita
“Majambazi huwapenda wanaowapenda. Chukulia mfano huu: Mimi na Wanda ni marafiki, OK? Baba yake, au genge la baba yake, hataweza kunidhuru au kuwadhuru watu ninaowapenda kwa sababu tu ya urafiki na mtoto wake. Na yeye anaweza kufumbiwa macho akifanya makosa kwa sababu mimi na mtoto wake ni marafiki wakubwa. Murphy, hapa Meksiko tuna kitu kinaitwa Bima ya Utekaji Nyara ('Ransom Insurance'). Zamani nilikuwa nalipa dola milioni kumi za Marekani kama bima ya utekaji nyara; Lisa alikuwa analipa milioni nne na Wanda bado analipa milioni mbili mpaka sasa hivi. Baada ya mimi na Lisa kujenga urafiki na Wanda, malipo yetu ya bima yamepungua mpaka dola milioni moja kwa mwaka.” FriendshipMexicoJohn Murphy AmbilikileLisaWandaDebbie Patrocinio AbregoMeksikoDolaMajambaziMtoto Wa Rais Wa MeksikoTen Million DollarsBima Ya Utekaji NyaraFour Million DollarsMpelelezi Wa Tume Ye DuniaOne Million DollarsRansom InsuranceTwo Million DollarsUrafiki Book:Kolonia Santita Source: Kolonia Santita