Quotessence
Home / Topics / Baba Quotes

Baba Quotes

Browse 190 quotes about Baba.

Baba Quotes

“Mwanampotevu dunia ilimfundisha ndiyo maana akarudi kwa baba yake akiwa amenyooka, hakuwa na maadili mema. Yusufu dunia ilimfundisha ndiyo maana akawa waziri mkuu wa Misri, na ndiyo maana akaokoa familia yake kutokana na njaa, alikuwa na maadili mema. Heri kudharaulika kwa kutenda mema kuliko kudharaulika kwa kutenda maovu. Ukidharaulika kwa kutenda maovu hutaishi sawasawa na mapenzi ya Mungu. Ukidharaulika kwa kutenda mema Mungu atakuinua.”

“Tupo watu takriban bilioni saba katika dunia hii. Kila mtu ni wa kipekee. Mathalani, wewe ni tofauti na baba yako au mama yako au mtu mwingine yoyote yule. Kila mtu aliumbwa kivyake na Mwenyezi Mungu. Kila mtu ana nafasi ya kwake mwenyewe aliyopangiwa na Mungu hapa duniani. Haijalishi wewe ni mwanamke au mwanamume, mweupe au mweusi, mfupi au mrefu, mzuri au mbaya, una nafasi katika nchi na dunia hii. Unachotakiwa kufanya ni kuamka, kufumbua macho na kuujua ukweli. Tafuta maarifa katika Biblia kama wewe ni Mkristo. Tafuta maarifa katika Kurani kama wewe ni Mwislamu. Tafuta maarifa katika Yoga kama wewe haumwamini Mungu. Ukishaamka na kuujua ukweli, ukishapata nafasi katika nchi yako, kuwa kiongozi na mkarimu kwa wenzako. Jifunze kutoka kwa wengine ndani na nje ya tasnia yako. Usiwe mchoyo wa maarifa. Kuwa mwadilifu. Ukifanya hivyo utafanikiwa zaidi, utaipa heshima tasnia yako, na utaacha alama katika dunia baada ya kuondoka. Kuacha alama katika dunia si lazima upate nafasi katika dunia. Kuacha alama katika dunia acha alama katika nchi yako.”

“Kusudi mimba itungwe lazima kuwepo na kromosomu X na kromosomu Y. Kromosomu ni nyuzinyuzi katika kiini cha seli zenye jeni au DNA, ambazo hubeba taarifa kuhusu sifa za kimaumbile zinazorithishwa kwa kiumbe hai kutoka kwa mama na baba wa kiumbe hicho. Kwa upande wa Yesu Kristo, katika hali ya kawaida, kromosomu X ilitoka kwa Maria Magdalena na kromosomu Y ilitoka kwa malaika Gabrieli. Yesu alikuwa Myahudi lakini Kristo ni Mungu. Yesu Kristo alikuwa binadamu kama sisi, lakini alikuwa na utukufu na alikuwa na damu ya Mungu iliyotakasika. Damu kama hiyo ndiyo inayotiririka katika miili ya kila mmojawetu ijapokuwa ni damu ya Adamu, ambayo bado haijatakaswa. Damu ya Yesu si kitu kidogo. Ilipomwagika msalabani ilifunika dunia nzima. Ndiyo maana tukasamehewa. Bila damu hiyo, bila utukufu huo wa Mungu, hakuna binadamu atakayeokolewa, hakuna pepo atakayeondolewa.”