“Kutunza siri wakati mwingine ni kitu kigumu sana kwa baadhi ya watu lakini watu wanapaswa kuwa na uwezo wa kutunza siri kujijengea uaminifu, ambao ni siri ya mafanikio.” PeopleSuccessAbilityTrustSecretsWatuMafanikioSiriUwezoUaminifu Author:Enock Maregesi
“Mafanikio unapaswa kuyataka kama unavyotaka hewa. Hewa ni kitu cha muhimu zaidi kuliko kitu kingine chochote kile ulimwenguni. Ukipewa hewa au shilingi bilioni kumi chagua hewa.” SuccessAirOxygenMafanikioHewaUlimwenguniOksijeniIn The UniverseShilingi Bilioni KumiTen Billion Shillings Author:Enock Maregesi
“Ukiwaza kwa kufuata kanuni ya nguvu ya uvutano (ambayo ni kuwaza na kuamini kama kile unachokiwaza tayari umeshakipata bila hata kujua umekipataje) utaishi kama ulivyowaza. Ukiwaza kuwa jambazi utakuwa jambazi hakika, ukiwaza kupona ugonjwa unaokusumbua utapona hakika, na ukiwaza kuwa tajiri utakuwa tajiri hakika. Mafanikio hayo yanaweza kuchukua mwezi mmoja kutimia au yanaweza kuchukua miaka kumi. Unachotakiwa kufanya ni kuwaza na kuamini.” SuccessRichDiseaseLaw Of AttractionCriminalMafanikioTajiriJambaziUgonjwaKanuni Ya Nguvu Ya UvutanoTen YearsMiaka KumiMwezi MmojaOne Month Author:Enock Maregesi
“Kuwa na uraibu wa mafanikio, si wa dawa.” SuccessAddictionDrugsMafanikioDawaUraibu Author:Enock Maregesi
“Ukikaa nyuma yangu utafanikiwa, ukikaa mbele utaanguka.” SuccessBehindMafanikioNyumaMbeleIn Front Author:Enock Maregesi
“Mafanikio ni matokeo mazuri ya jambo lolote na ni tofauti kwa kila mtu. Kama ulivyo uzuri, mafanikio yapo katika macho ya aonaye. Ni jukumu lako kujua mafanikio yana maana gani kwako, na jinsi gani umeyapata mafanikio hayo.” SuccessEyesMachoMafanikio Author:Enock Maregesi
“Unataka kufanikiwa lakini hutaki watu wakuone. Kama una kipaji kionyeshe kwa watu.” PeopleSuccessTalentWatuMafanikioKipaji Author:Enock Maregesi
“Ukiwa juu uwezekano wa kushuka chini ni mkubwa sana, kuliko ukiwa chini ambapo uwezekano wa kupanda juu ni mkubwa sana.” UpDownMafanikioUmaskiniJuuChini Author:Enock Maregesi