Quotessence
Home / Books / Kolonia Santita

Kolonia Santita

Book by Enock Maregesi · 4 quotes · John Murphy, John Murphy Ambilikile, Murphy

Filter quotes by topic

Kolonia Santita Quotes

“Sigara zilizidi kuvutwa, ndani ya nyumba, na magaidi wale wawili, wakati Murphy akisinzia kudanganyia kama kweli nguvu zilishamwisha. Alimfikiria tena mpenzi wake Sophia, safari hii sana. Alimkumbuka Debbie; hakujua alikuwa wapi na hakujua mama yake angefanya nini kama Debbie angekufa, na Murphy ndiye aliyetoka naye. Debbie alimuuma zaidi. Alimkataza kufa kwa ajili ya mchumba wake. Sasa alikufa kwa ajili ya mtu ambaye hakumjua. Murphy alijilaumu kumtongoza na kumchukua kwao na kulala naye na kula chakula chake cha kifalme. Wazazi wake wangejisikiaje kama angekufa, tena katika mazingira ya kutatanisha kama yale. Kufa alijua angekufa; lakini Mungu angemsaidia, awaage watu wake.”

“Nyoka ni mnyama mdogo lakini anayeogopwa hata na majambazi wakubwa. Adui wa dirishani alipogeuka kumwangalia Murphy, alimwangalia pia mwenzake na kucheka bila Murphy kujua kilichofanya wafurahi. Ghafla, kuna kitu kilitokea! Nyoka mkubwa aina ya swila aliruka toka dirishani na kuanguka katika mabega ya yule adui. Adui aliruka kwa woga na kuanguka chini … halafu yakatokea maajabu! Bunduki ilifyatuka kutoka nje, ikaripuka kwa sauti ya juu, walinzi wote wa Murphy wakaruka na kuanguka chini shaghalabaghala, na kufa papo kwa papo!”

“Usiwe na wasiwasi, Peter. Hizo ni hisia zangu tu. Huwezi kuwa mpelelezi. Lakini, kusema ule ukweli, ningependa sana kuonana na John Murphy. Kuna kazi binafsi ningependa kumpa. Wewe unatoka Afrika, hujawahi kumwona?” Debbie alizidi kumshtua Murphy. “Nani?” Murphy aliuliza huku akitabasamu. “John Murphy wa Afrika.” “Sijawahi kumwona. Mbona unamuulizia hivyo?” Debbie alitulia. Kisha akarusha nywele ili aone vizuri. “Nampenda sana!” “Kwa nini?” “Simpendi kwa mahaba, lakini.” “Ndiyo. Kwa nini?” “OK. Nampenda kwa kipaji chake. Alichopewa na Mungu, cha ujasusi. Kusaidia watu.” “Ahaa!” Murphy alidakia, sasa akifikiri sana. “Murphy ana mashabiki wengi hapa Meksiko bila yeye mwenyewe kujua, kwa sababu ya kupambana na wahalifu wa madawa ya kulevya – hasa wa huku Latino. Tatizo lake haonekani. Wengi hudhani ni hadithi tu, kwamba hakuna mtu kama huyo hapa duniani.” “Hapana! Murphy yupo! Ni mfanyabiashara maarufu huko Tanzania. Lakini ndiyo hivyo kama unavyosema ... Haonekani!”

“Mateso yalishakuwa mengi, na Murphy alishakata tamaa. Kesho yake alitamani sana aione lakini hakukuwa na dalili yoyote ya maadui kumwacha hai. Walivyomning’iniza kama nyama ya kuokwa kwa kipindi kirefu, walichoka kupiga na kumkalisha katika kiti cha umeme na kumfunga miguu na mikono kwa machuma makubwa yaliyofanana na pingu.”