“Ndoto za wachawi ni tofauti kidogo na ndoto takatifu. Wachawi wanapokuwa hawahitaji kusafiri kutoka sehemu moja kwenda nyingine, lakini wana hamu ya kuona wenzao wanafanya nini au wanasema nini, huwa wanalala ubavu mmoja upande wa kushoto kwa jina la mungu wao na la mashetani wote. Kisha wanatoa mvuke wa bluu midomoni mwao. Kupitia mvuke huo, kwa nguvu za Shetani na kwa ruhusa ya Mwenyezi Mungu, wataona na watasikia kila kinachofanyika upande wa pili. Kile wanachotaka kukiona na kukisikia hujifunua katika ufahamu wao kama taswira au maono, kutoka katika akili isiyotambua, ya watu wakifanya au wakisema kitu. Kama wanataka kujua siri za watu wengine, hata wale ambao si wachawi, watazijua kupitia ndoto hizo; kwa sababu ya makubaliano ya wazi, si ya siri, waliyoingia na Shetani. Makubaliano hayo si ya lelemama; yaani yale ambayo hufanywa kwa kutoa kafara ya mnyama, au kufuru ya aina yoyote ile kwa Mwenyezi Mungu, au kwa kuabudu dini za kichawi. Lakini ni kwa sadaka halisi ya wao wenyewe ya mwili na roho kwa Shetani na kwa kufuru ya kuikana kabisa, imani ya Mwenyezi Mungu. Lakini hiyo ni kwa wale wanaotumia uchawi wa kishetani. Wale wanaotumia uchawi wa asili, kama vile kutumia risasi kumroga mtu kwa sababu risasi mungu wake ni sayari ya Zohali, au wale walioingia mkataba wa siri na Shetani, hawana uwezo wa kuota hivyo. Hivyo, si kila mchawi anaweza kuota ndoto za namna hiyo, ni kwa wale tu walioingia mkataba wa wazi na Shetani.” SecretConsciousnessDreamsSatanAgreementOfferingWitchesLeadVisionsSubconscious MindAlmighty GodVaporSaturnShetaniPicturesThe Other SideSiriBody And SoulMwenyezi MunguRisasiNdotoAnimal SacrificeMaonoWachawiUfahamuSadakaTaswiraAkili IsiyotambuaGod S FaithHoly DreamsLeft SideMwili Na RohoNdoto TakatifuAll The DevilsBlue VaporDini Za KichawiDreams Of The WitchesImani Ya Mwenyezi MunguKafara Ya MnyamaMakubalianoMakubaliano Ya SiriMakubaliano Ya WaziMashetani WoteMungu WaoMvukeMvuke Wa BluuNatural WichcraftNdoto Za WachawiOne Rib SideOpen AgreementSatanic WitchcraftSecret AgreementTheir GodUbavu MmojaUchawi Wa AsiliUchawi Wa KishetaniUpande Wa KushotoUpande Wa PiliWitchcraft ReligionsZohali Author:Enock Maregesi
“Kutokana na utafiti wa kisayansi wa kionairolojia ambayo ni sayansi ya ndoto; wakati tumelala, sehemu yetu ya akili isiyotambua huamka na kuanza kazi; kwa kupangilia mawazo, kuanzia mawazo ya siku iliyopita, na kuimarisha mahusiano baina ya mawazo hayo na matukio ya wakati ujao, huku ikiondoa mawazo yasiyokuwa na maana, kunusuru ubongo usielemewe na msongo. Kazi hiyo hutambuliwa haraka na akili inayotambua, kwa njia ya alamu, lakini akili inayotambua inapagawa kwa sababu haijui akili isiyotambua inamaanisha nini kutuma alamu kama hizo. Kwa hiyo inajaribu kwa kadiri inavyoweza kutunga hadithi kuhusiana na vitu mbalimbali, ambayo baadaye hutafsiriwa kama ndoto. Hii ndiyo sababu tunaota ndoto za ajabu ambazo aghalabu hazina maana yoyote, na hazina maana yoyote kwa sababu hazitakiwi kuwa na maana yoyote, na hazina ujumbe wowote halisi kutoka akilini mwetu. Hayo ni matokeo ya akili kujaribu kusanisi sauti, kutoka katika akili isiyotambua.” IdeasDreamRelationshipsWorkBrainStorySignalsSubconscious MindScientific ResearchConscious MindFuture EventsKaziMawazoNdotoUbongoHadithiAlamuAkili IsiyotambuaAkili InayotambuaKusanisi SautiMahusianoMatukio Ya Wakati UjaoSayansi Ya NdotoScience Of DreamsSynthesiseUtafiti Wa KisayansiWakati TumelalaWhile We Are Asleep Author:Enock Maregesi