“Jina langu ni Enock Maregesi na ningependa kukwambia kisa kidogo kuhusiana na bibi yangu, Martha Maregesi. Mwanamke huyu alikuwa mke mwenye upendo usiokuwa na masharti yoyote. Alikuwa mama na bibi aliyefundisha familia yake umuhimu wa kujitolea na umuhimu wa uvumilivu. Ijapokuwa hakupendelea sana kujizungumzia mwenyewe, ningependa kukusimulia kisa kidogo kuhusiana na hadithi ya maisha ya mwanamke huyu wa ajabu katika maisha yangu. Bibi yangu alizaliwa katika Kitongoji cha Butimba, Kijiji cha Kome, Kata ya Bwasi, Tarafa ya Nyanja (Majita), Wilaya ya Musoma Vijijini, Mkoa wa Mara, katika familia ya watoto kumi, mwaka 1930. Alisoma katika Shule ya Msingi ya Kome ambako alipata elimu ya awali na msingi na pia elimu ya kiroho kwani shule yao ilikuwa ya madhehebu ya Kisabato. Aliolewa na Bwana Maregesi Musyangi Sabi mwaka 1946, na kufanikiwa kupata watoto watatu; wa kiume wakiwa wawili na wa kike mmoja. Matatizo hasa ya bibi yalianza mwaka 2005, alipougua kiharusi akiwa nyumbani kwake huko Musoma. Hata hivyo alitibiwa hapo Musoma na Dar es Salaam akapona na kuwa mwenye afya ya kawaida. Lakini tarehe 19/10/2014 alipatwa tena na kiharusi na kulazwa tena katika Hospitali ya Mkoa ya Musoma, ila akajisikia nafuu na kuruhusiwa kurudi nyumbani – lakini kwa maagizo ya daktari ya kuendelea na dawa akiwa nje ya hospitali. Tarehe 29/10/2014 alirudi tena Hospitali ya Mkoa ya Musoma kwa tiba zaidi, lakini tarehe 4/11/2014 saa 7:55 usiku akafariki dunia; akiwa amezungukwa na familia yake. Dunia ina watu wachache sana wenye matumaini na misimamo ya kutegemea mazuri, na wachache zaidi ambao wako tayari kugawa matumaini na misimamo hiyo kwa watu wengine. Nitajisikia furaha siku zote kwamba miongoni mwa watu hao wachache, hata bibi yangu alikuwemo. Msalaba uliwekwa wakfu na Mwenyezi Mungu baada ya mwili wa Yesu Kristo kuning’inizwa juu yake. Kwa kuwa bibi yangu ametanguliwa na msalaba, msalaba utamwongoza mahali pa kwenda.” PeopleWorldLoveMotherHopeFamilyWifeSacrificeShareJesus ChristPerseveranceOptimisticWomanTreatmentGrandmotherStoryUnconditional LoveMamaDoctorCrossHospitalFamiliaDuniaWatuYesu KristoEnock MaregesiMwenyezi MunguStrokeMwanamkeUpendoSabatoGod AlmightyMara2005KujitoleaBibiUvumilivu1930Dar Es SalaamMkeMsalaba1946DaktariHadithiMusomaMartha MaregesiWakfuKiharusi01 55 Hours19 10 201429 10 20144 11 2014ButimbaBwasiHospitaliHospitali Ya Mkoa Ya MusomaKomeKome Primary SchoolKugawaMajitaMaregesi MusyangiMaregesi Musyangi SabiMatumainiMisimamoMusoma VijijiniNyanjaOrdinanceSaa 7 55 UsikuSeventh Day AdventistShule Ya Msingi Ya KomeTiba Author:Enock Maregesi
“Ningependa kujitokeza leo kutoa salamu zangu za rambirambi kwa Watu wa Musoma; kutokana na ajali mbaya ya mabasi ya J4 Express, Mwanza Coach, na gari ndogo aina Nissan Terrano, iliyotokea Ijumaa tarehe 5/9/2014 katika eneo la Sabasaba mjini Musoma. Kulingana na vyombo vya habari, watu 39 wamefariki dunia. Wengine wengi wamejeruhiwa vibaya. Mali za mamilioni ya fedha zimeteketea kabisa. Hii ni ajali mbaya na ya kusikitisha mno kwa maana halisi ya maneno mabaya na ya kusikitisha. Maneno hayataweza kuelezea kikamilifu huzuni niliyonayo juu ya ajali hii ya kutisha, lakini Mungu awasaidie wale wote waliofiwa au walioguswa na ajali hiyo kwa namna yoyote ile, na awasamehe marehemu wote dhambi zao na awapumzishe mahali pema peponi. Wale wote waliofariki hawataweza kurudi huku, lakini sisi tutakwenda huko.” GodFridayMunguSinsCondolencesMaliDhambiBusesIjumaaMusomaAjali395 9 2014J4 ExpressJ4 Express T 677 CycMabasiMahali Pema PeponiMajeruhiMara Regional CommissionerMarehemuMkuu Wa Mkoa Wa MaraMkuu Wa Wilaya Ya Musoma MjiniMwanza CoachMwanza Coach T 736 AwjNissan TerranoNissan Terrano T 332 AkkPresident Of TanzaniaSalamu Za RambirambiThe People Of MusomaWatu Wa Musoma Author:Enock Maregesi
“Bibi Martha Maregesi aliishi maisha mazuri sana hapa duniani. Alibarikiwa na Mungu. Aliishi miaka 84 – siku 30660 badala ya siku 25550 tulizopangiwa na Mungu. Katika uhai wake wote, kwa wale wote aliowalea, hakuna mtoto wake hata mmoja aliyefariki kabla yake. Hakuna mjukuu wake hata mmoja aliyefariki kabla yake. Hakuna kitukuu chake hata kimoja kilichofariki kabla yake. Bibi yangu ametimiza mwaka mmoja kamili leo hii, tangu amefariki dunia Novemba 4 mwaka 2014 mjini Musoma. Tunamkumbuka leo akiwa amefariki kama tulivyomkumbuka jana akiwa hai. Nguvu ya sala zetu imfanye Mwenyezi Mungu aendelee kumsamehe dhambi zake zote, na amweke mahali anapostahili, Amina.” LifeGodGrandmotherChildPrayersAmenMunguSinsDhambiMtotoBibiOne YearMusomaMartha MaregesiAminaSalaUhai25550 Days30660 Days84 Years OldGrandchildGreat GrandchildKitukuuMiaka 84MjukuuMwaka MmojaNovemba 4 Mwaka 2014Siku 25550Siku 30660 Author:Enock Maregesi
“Leo ni siku ya kumbukumbu ya giza lililoingia katika familia ya Enock Maregesi. Tarehe 4/11/14 ni siku nuru ya mwanga wa maisha ya nyanya yangu mpenzi Bi Martha Maregesi ilipozimika huko Musoma. Leo ni miaka miwili ametimiza akiwa kimya kabisa! Sikisikii tena kicheko chake wala siisikii tena hekima yake! Familia yake inamkumbuka sana. Palipokuwa kwake ni nyumbani kwetu. Hatuwezi kusahau upendo wake na umuhimu wake kwetu. Tulimpenda sana, lakini Mungu wa mbinguni alimpenda zaidi.” TodayDarknessTwo YearsMemorial DayMy GrandmaLeoHer LoveGizaMusoma4th November 2014Absolutely SilentBi Martha MaregesiBibi YanguBrightness Of LightEnock Maregesi S FamilyFamilia Ya Enock MaregesiFamilia YakeGod Loved Her MoreGrandma Martha MaregesiHatuwezi KusahauHekima YakeHer FamilyHer LaughterHer Value To UsHer WisdomKicheko ChakeKimya KabisaMiaka MiwiliMungu Alimpenda ZaidiNuru Ya MwangaNyanya YanguNyumbani KwetuOur HomePalipokuwa KwakeSiku Ya KumbukumbuTarehe 4 11 14Tulimpenda SanaUmuhimu Wake KwetuUpendo WakeWe Cannot ForgetWe Loved Her So MuchWhat Was Her Home Author:Enock Maregesi