“Vita ya Shetani na Mungu inatuathiri zaidi sisi wanadamu – na hapo baadaye itamuathiri Shetani pia. Vita hii haiwezi kuisha hadi siku ya mwisho, Yesu Kristo atakaporudi kuwachukua wateule wake. Pambana kwa njia ya maombi hadi siku ya mwisho kwa sababu adui tunayepambana naye hana muda wa kupumzika. Pambana kujiombea na kuwaombea wengine waliohai, na hata wale ambao bado hawajazaliwa, kabla mafuta ya dunia hii hayajalipuka. Usiishi kama adui wa msalaba wa Yesu Kristo, badala yake, ishi kama rafiki wa msalaba wa Yesu Kristo. Kuishi kama rafiki wa msalaba wa Yesu Kristo ni kupinga majivuno yote ya Shetani kwa upendo uliotukuka wa kujishusha au kujidharirisha, kutokutetereka hata kidogo na tamaa za ulimwengu huu kwa upendo mkubwa wa umaskini, na kutokuyumba wakati wa matatizo kwa sababu wakati wa amani ulijilimbikizia imani.” LoveNeedsHumansGodFaithPeaceEnemyPovertyPrideBattleJesus ChristSatanFightFriendVitaPrayersMunguShetaniAmaniYesu KristoMatatizoImaniUpendoWanadamuMaombiAduiUmaskiniRafikiDay Of JudgementPambanaMsalaba Wa Yesu KristoThe Cross Of Jesus ChristElectsSiku Ya MwishoWateuleMafuta Ya Dunia HiiMajivunoOil Of This WorldTamaa Za Ulimwengu HuuThe Desires Of This World Author:Enock Maregesi
“Wanasayansi wanaamini kuwa Yesu atarudi tarehe 29 Julai 2016. Tarehe hiyo kitu kikubwa sana kitatokea katika dunia yetu kitakachosababisha tetemeko kubwa la ardhi, litakalosababishwa na kubadilika kwa ncha za dunia, tendo litakalosababisha mionzi ya gama kutoka kwenye jua ifike duniani na kuua kila kitu kinachoonekana katika uso wa dunia hii. Watakatifu watafufuka na kumlaki Kristo mawinguni, ambaye anakuja kuwachukua wateule na kumweka Shetani kifungoni kwa miaka 1000. Hayo yote, wanasema, yatatokea ndani ya siku 11 kuanzia leo. Yaani, kusini mwa dunia kutakuwa kaskazini mwa dunia, kaskazini mwa dunia kutakuwa kusini mwa dunia. Kitendo hicho kitafanya dunia ikose kinga ya sumaku iitwayo ‘magnetosphere’ ambayo hukinga dunia dhidi ya mionzi ya gama kutoka kwenye jua. Mionzi hiyo hugonga ukuta wa ‘magnetosphere’ kila baada ya dakika 8 kwa mwendokasi wa kilometa milioni 1080 kwa saa; na kusambazwa katika ncha za dunia ambapo aghalabu huchanganyikana na oksijeni na kutengeneza kitu kinaitwa ‘aurora’, au mwanga wa ncha, ambacho ni maajabu mengine ya angani. Mwaka 2012 wanasayansi walisema ncha za dunia zingebadilika lakini hazikubadilika. Je, muda umefika sasa wa kuwaamini wanasayansi? Biblia ni chuo cha Mungu. Soma Biblia kupata maarifa.” WorldJesusChristKnowledgeSunBibleSatanOxygenScientistsSaintsDuniaShetaniWondersAurora2012BibliaEarthquakeYesuMaarifaJuaKristoWanasayansiOksijeni1000 YearsMaajabuMiaka 1000WatakatifuElectsMwaka 2012Wateule1080 Million Kilometers Per Hour29th July 20168 MinutesChuo Cha MunguDakika 8Gamma Rays RadiationsGod S CollegeKaskazini Mwa DuniaKilometa Milioni 1080 Kwa SaaKinga Ya SumakuKusini Mwa DuniaMagnetosphereMionzi Ya GamaMwanga Wa NchaNcha Za DuniaNorthern WorldSouthern WorldTarehe 29 Julai 2016Tetemeko La ArdhiWorld Poles Author:Enock Maregesi