“Kabla ya uasi, Mungu alimpa Shetani na wasaidizi wake ambao ni mapepo mamlaka makubwa juu ya kila kitu hapa duniani; kuanzia angahewa la dunia hadi ardhi ya dunia nzima nasi wakazi wake tukijumuishwa. Abadani tusisahau kwamba, kwa kiasi kikubwa, kupambana kwetu kama Paulo anavyosema ni dhidi ya hawa mapepo na mfalme wao ambaye ni Shetani. Tunaishi katika eneo ambapo hata wao wanaishi. Hawa mapepo wabaya huwatumia maadui wa msalaba wa Yesu Kristo kutekeleza mipango yao kwa lengo la kuwaangamiza marafiki wote wa msalaba wa Yesu Kristo, wanashawishiwa kwa kiasi kikubwa na hizo mamlaka za kimapepo, na kwa sababu wamedanganywa, hawajui hata kidogo kama Shetani anawatumia! Inawezekana hawajatwaliwa na mapepo lakini wanashawishiwa na mapepo kutenda kinyume na mapenzi ya Mungu kwa wanadamu wote.” HumansGodEarthPlansFriendsAuthorityAtmosphereSatanDemonsEnemiesKingMunguDuniaShetaniPaulWill Of GodMaaduiPauloWanadamuMamlakaMarafikiInhabitantsMapenzi Ya MunguMapepoMfalmeMipangoMsalaba Wa Yesu KristoThe Cross Of Jesus ChristAngahewaBefore RebellionDemonic PowersKabla Ya UasiMamlaka Za KimapepoMapepo WabayaWakazi Author:Enock Maregesi
“Jambo ambalo Mungu anataka tulitambue ni kwamba hatuko wenyewe katika bahari hii ya hewa. Hata nyangumi na wazira waovu wanapozunguka huko na huko baharini, ambao pia ni mapepo, wanaochukuliwa kama viumbe wabaya na wachafu na wala mizoga, wanaishi katika bahari hii ya hewa pamoja na sisi. Ni muhimu, kwa ajili ya ustawi wetu wa kiroho, kusikia onyo la Paulo katika Waefeso 6:10-12 kwamba vita yetu si dhidi ya hawa viumbe, na wanapambana usiku na mchana kutetea kile ambacho wanaamini ni cha kwao kwa sababu ya haki ya kuwepo hapa kwanza kabla yetu. Dunia, Biblia inatwambia, ilikuwa makazi yao ya kwanza (Yuda 1:6, KJV). Wanatuchukia kwa sababu taratibu tunakuwa Baba na Mwana, na kwa sababu wanajua hii dunia, urithi wetu, itachukuliwa kutoka mikononi mwao na kukabidhiwa kwa wale ambao ni watoto wa Mungu, wale ambao ni marafiki wa msalaba wa Yesu Kristo.” GodEarthAirFriendsBibleRightDemonsDay And NightMunguFather And SonDuniaPaulBibliaWhaleChildren Of GodPauloHakiKjvMarafikiHewaMapepoMsalaba Wa Yesu KristoThe Cross Of Jesus ChristWatoto Wa MunguBaba Na MwanaEphesians 6 10 12Evil CreaturesJudas 1 6NyangumiOur BattleOur HeritageUrithi WetuUsiku Na MchanaVita YetuViumbe WabayaWaefeso 6 10 12Wazira WaovuYuda 1 6 Author:Enock Maregesi
“Vita ya Shetani na Mungu inatuathiri zaidi sisi wanadamu – na hapo baadaye itamuathiri Shetani pia. Vita hii haiwezi kuisha hadi siku ya mwisho, Yesu Kristo atakaporudi kuwachukua wateule wake. Pambana kwa njia ya maombi hadi siku ya mwisho kwa sababu adui tunayepambana naye hana muda wa kupumzika. Pambana kujiombea na kuwaombea wengine waliohai, na hata wale ambao bado hawajazaliwa, kabla mafuta ya dunia hii hayajalipuka. Usiishi kama adui wa msalaba wa Yesu Kristo, badala yake, ishi kama rafiki wa msalaba wa Yesu Kristo. Kuishi kama rafiki wa msalaba wa Yesu Kristo ni kupinga majivuno yote ya Shetani kwa upendo uliotukuka wa kujishusha au kujidharirisha, kutokutetereka hata kidogo na tamaa za ulimwengu huu kwa upendo mkubwa wa umaskini, na kutokuyumba wakati wa matatizo kwa sababu wakati wa amani ulijilimbikizia imani.” LoveNeedsHumansGodFaithPeaceEnemyPovertyPrideBattleJesus ChristSatanFightFriendVitaPrayersMunguShetaniAmaniYesu KristoMatatizoImaniUpendoWanadamuMaombiAduiUmaskiniRafikiDay Of JudgementPambanaMsalaba Wa Yesu KristoThe Cross Of Jesus ChristElectsSiku Ya MwishoWateuleMafuta Ya Dunia HiiMajivunoOil Of This WorldTamaa Za Ulimwengu HuuThe Desires Of This World Author:Enock Maregesi