Quotessence
Home / Quotes / Quote by Enock Maregesi

Quote by Enock Maregesi

“Pesa ikitolewa kwa masharti mazuri chukua, kama masharti ya kibenki, si masharti mabaya kama ya kiganga, huyo anayeitoa si ya kwake. Pesa mbaya imebarikiwa na Shetani, ukiichukua umeingia agano na Shetani, jambo ambalo Mungu hapendi. Chukua pesa kutoka kwa mtu unayemjua ambaye hana masharti au hana masharti ya kishetani, au usiyemjua.”

Quote by Enock Maregesi

Author

Enock Maregesi

Browse famous quotes and profile details for Enock Maregesi. more

You May Also Like

“Usipoangalia kwa undani sana, mapepo wanatutawala kwa sababu hatuna uwezo wa kuwaona. Aidha, wanaweza, bila hata sisi kujua, kuwasiliana nasi kimawazo na kitabia kupitia hewa hiihii inayotusaidia katika kuishi. Watu wengi katika dunia hii hawajui kama wanadanganywa au walishadanganywa tayari. Shetani na mapepo wake hawataki tujue kama wanatudanganya au wameshatudanganya tayari, na hawataki tujue kama wako hapa kwa ajili ya kutudanganya sisi. Tunajua tu kwa sababu Neno la Mungu hudhihirisha ukweli huu kupitia Roho Mtakatifu na malaika wema, na tunauamini. Licha ya hili jambo kutokea katika maisha yetu, Shetani bado anaweza kutudanganya hadi pale tutakapoerevuka kwa kiasi cha kutosha kuhakikisha kwamba udanganyifu huo hautatokea tena.”

“Hata hivyo, Shetani anaweza kutudanganya kupitia tamaduni zetu tulizozaliwa nazo. Utamaduni, dunia tunapoishi, ndiyo chanzo cha udanganyifu huu. Yesu Kristo alikufa msalabani ili tupate uhuru kutoka kwa Shetani. Chukua hatua sasa kwa sababu Shetani anaweza kukuteka, na kukufanya mtumwa tena.”