Quotessence
Home / Topics / Elimu Quotes

Elimu Quotes

Browse 14 quotes about Elimu.

Elimu Quotes

“Pesa ina thamani pale unapokuwa nayo, si pale unapokuwa huna, hivyo iweke mahali unapoweza kuiona: katika nyumba, katika shamba au katika elimu. Badala ya kumpa mtu pesa ili ajenge nyumba, mpe nyumba. Badala ya kumpa mtu pesa ili afanye biashara, mpe biashara. Halafu, mpe elimu afanye maamuzi ya biashara yake. Pesa ina laana na Mungu pekee ndiye anayeweza kuiondoa laana hiyo. Ni rahisi kwa tajiri kupata baraka ya pesa kwa sababu ana pesa na ana uwezo mkubwa wa kusaidia maskini. Ni vigumu kwa maskini kupata baraka ya pesa kwa sababu hana au ana uwezo mdogo wa kusaidia maskini. Mungu anaweza kuondoa laana ya pesa kupitia hisani kwa maskini, kitu ambacho aghalabu hufanywa na matajiri wenye uwezo mkubwa. Heri kutoa kitu au huduma au elimu kwa maskini kuliko pesa.”

“Inavyoonekana, kadiri mtu anavyozidi kupata elimu ndivyo anavyozidi kudharau uwepo wa Shetani na uwepo wa Mungu pia. Lakini, kwa upande mwingine, ndivyo anavyoonekana hajasoma sana na ndivyo Shetani anavyozidi kulaumiwa kwa kila dhambi inayotendeka. Kuna elimu ya kidunia na kuna elimu ya kidini. Huwezi kutawala dunia bila elimu ya kidunia, kwa sababu Shetani anajua ukiipata elimu hiyo hutajua kama yupo; na huwezi kutawala dunia bila elimu ya kidini, kwa sababu Mungu anajua ukiipata elimu hiyo utajua kama yupo. Hivyo, utamdharau Mungu ukipata elimu ya kidunia, utamheshimu Mungu ukipata elimu ya kidini.”

“Ukiwaza kitu kwa dakika moja na sekunde nane – huu ni utafiti wangu tu – hicho kitu kitaanza kujiumba kwa ajili yako sehemu fulani ulimwenguni. Ukiamini kwa kiasi cha kutosha kwamba umekipata, utakipata. Haijalishi kama una elimu au huna. Hiyo ndiyo siri kubwa zaidi ya utajiri kuliko zote duniani – MAWAZO YAKO.”

“Ili kupambana na matumizi mabaya ya madawa ya kulevya katika jamii ya Tanzania, ni muhimu kutoa elimu kwa Watanzania juu ya madhara yanayoambatana na matumizi ya madawa hayo. Tusipambane na madawa ya kulevya peke yake. Tupambane na elimu ya madawa ya kulevya pia.”

“Yusufu alikuwa hohehahe kabla na baada ya kuuzwa na nduguze kama mtumwa nchini Misri. Hakuwa na pesa, hakuwa na elimu, hakujuana na viongozi wa serikali. Lakini kwa vile alikuwa na Mungu, Mungu alimbariki mpaka watu wote wakashangaa. Yusufu alikuwa maskini ili mimi na wewe tuwe na tumaini leo, kwamba tukiwa na Mungu katika maisha yetu hatutatafuta utajiri. Utajiri ndiyo utakaotutafuta sisi.”