Quotessence
Home / Topics / Serikali Quotes

Serikali Quotes

Browse 18 quotes about Serikali.

Serikali Quotes

“Badilisha tabia. Badilisha mazingira ya maisha yako. Haijalishi una umri kiasi gani au wewe ni mwanamke au mwanamume, bado hujachelewa kubadili maisha yako kutoka duni kuwa bora – kuwa na amani, furaha na kuridhika. Kama desturi yako ni kuamka saa 12:00 asubuhi kila siku ili ufike kazini saa 2:00 asubuhi ambao ni muda wa serikali wa kuanza kazi, amka saa 11:30 asubuhi ili ufike kazini saa 1:30 asubuhi – nusu saa kabla ya kuanza kazi. Kama unafanya kazi ya taaluma uliyosomea lakini maisha hayaendi, fikiria kubadili mwelekeo wa maisha ikiwemo taaluma kufikia malengo uliyojiwekea.”

“Kitalifa ni utiifu kamili, woga, umbali (kwa maana ya kuwa mbali na biashara ya mamafia wengine mpaka kwa makubaliano maalumu) na nidhamu ya kutoshirikiana na mamlaka zote za serikali. Ukishtakiwa kwa kosa la madawa au ujambazi ambalo hukufanya, utatumikia kifungo mpaka mwisho bila kushirikiana na polisi (kwa maana ya kutaja aliyehusika au waliohusika na uhalifu huo) hata kama aliyehusika au waliohusika hana au hawana uhusiano wowote na Kolonia Santita. Falsafa ya Kitalifa ni Sheria ya Kitalifa ya Kiapo cha Swastika cha Kolonia Santita. Na adhabu ya kuvunja sheria hiyo ni kifo.”

“Ukanda wa Gaza ni jimbo lenye miji minne na kambi mbalimbali za wakimbizi za Umoja wa Mataifa – lenye urefu wa kati ya kilometa 41 au maili 25 na lenye upana wa kati ya kilometa 6 mpaka 12 au maili 3.7 mpaka 7.5, pamoja na eneo la jumla la kilometa za mraba 365 au maili za mraba 141. Jimbo hili liliwahi kutawaliwa na Wamisri, Wakaanani, Waisraeli, Wasiria, Wababelonia, Wagiriki, Warumi, Waturuki, Waingereza, na Wapalestina, na limekuwa uwanja wa vita kwa karne nyingi kwa sababu za kidini na kihistoria. Ukanda wa Gaza uko chini ya Palestina. Uko chini ya serikali ya Hamas.”

“Yusufu alikuwa hohehahe kabla na baada ya kuuzwa na nduguze kama mtumwa nchini Misri. Hakuwa na pesa, hakuwa na elimu, hakujuana na viongozi wa serikali. Lakini kwa vile alikuwa na Mungu, Mungu alimbariki mpaka watu wote wakashangaa. Yusufu alikuwa maskini ili mimi na wewe tuwe na tumaini leo, kwamba tukiwa na Mungu katika maisha yetu hatutatafuta utajiri. Utajiri ndiyo utakaotutafuta sisi.”