“Saa nane za usiku timu nzima ya Vijana wa Tume ilirudi San Ángel katika helikopta ya DEA, tayari kwa safari ya Salina Cruz katika jimbo la Oaxaca. Kukamatwa kwa Gortari, Eduardo na Dongyang ulikuwa ushindi mkubwa wa kwanza wa Tume ya Dunia. Ushindi huo ukalipua wimbi la kukamatwa kwa wahalifu wa kimataifa, wa Kolonia Santita, dunia nzima.” JourneyTeamVictoryWaveSafariKolonia SantitaTume Ya DuniaHelicopterVijana Wa TumeDeaWorldwideOaxacaSalina CruzDunia NzimaUshindi2 AmEduardo Chapa De ChristopherGortari ManuelHelikoptaTimuLi DongyangDongyangEduardoGortariInternational CriminalsSaa 8 Za UsikuSan ÁNgelWahalifu Wa KimataifaWimbi Book:Kolonia Santita Source: Kolonia Santita
“Komandoo Nicolas Kahima Kankiriho ('Kahima the Warrior') alizaliwa katika Wilaya ya Bushenyi, Ankole, kusini-magharibi mwa Uganda, Julai 24, 1954, mtoto wa tano kuzaliwa, katika familia ya watoto sita ya Nicodemas Kankiriho; mzee wa heshima wa Wabaima, aliyekuwa akisifika sana kwa uchungaji (wa mifugo) na msisitizo mkali wa ukiristo kwa watoto wake wote; hasa Kahima na Yebare, binti yake wa pekee, aliyekuwa wa mwisho kuzaliwa. Kahima (futi 6 inchi 3 aliyekuwa akiongea Kinyankole, Kiswahili, Kiingereza na Kihispania kwa ufasaha), baada ya kutoka Uganda – kwa mafunzo ya mwanzo ya ukomandoo ya Kiisraeli – alikwenda Urusi na Korea ya Kaskazini ambako aliongeza ujuzi hadi kiwango cha juu kabisa; kabla ya kwenda Amerika ya Kusini, kama askari wa msituni wa vyama vya kisiasa visivyo rasmi vya magorila wa Kolombia. Akiwa Kolombia, Kahima alikutana na Eduardo Chapa de Christopher (kiongozi wa zamani wa Kateli ya Diablos de Amazonas, Mashetani wa Amazoni, iliyokuwa ikivilinda vyama vya kisiasa vya magorila vya Americas) ambaye alimwajiri kama mlinzi binafsi na baadaye kama mlinzi binafsi wa Carlos Pulecio Alcántara – kiongozi wa kwanza wa Kateli ya Kolonia Santita. Alcántara alipouwawa, Kahima alihamia kwa Panthera Tigrisi – Kiongozi Mkuu wa Kolonia Santita.” FamilyChristianityIsraelRussiaIsraeliNorth KoreaSpanishEnglishColombiaSouth AmericaBodyguardFamiliaUgandaKolonia SantitaSwahiliCommandoKiswahiliPanthera Tigrisi1954KiingerezaUrusiAmericasAmerika Ya KusiniEduardo Chapa De ChristopherKolombiaKomandooAskari Wa MsituniGuerrilla SoldiersKahima KankirihoKiongozi Wa Kolonia SantitaKolonia Santita LeaderKorea Ya KaskaziniAnkoleBaimasBushenyiCarlos Pulecio AlcántaraDiablos De AmazonasJulai 24Kahima The WarriorKihispaniaKinyankoleKusini Magharibi Mwa UgandaLast BornMashetani Wa AmazoniMlinzi BinafsiMwisho KuzaliwaNicodemas KankirihoNicolas Kahima KankirihoRunyankoleSouthwest UgandaUkiristoWabaimaYebare Author:Enock Maregesi
“Kwa sababu za kijiografia, Copenhagen iko mbele kwa masaa 9 (PST) kuilinganisha na Tijuana (kaskazini-magharibi mwa Meksiko) na masaa 7 (CST) kuilinganisha na Salina Cruz (kusini-magharibi mwa Meksiko). Mauaji ya Meksiko yametokea saa 4 usiku wa Jumanne, Copenhagen ikiwa saa 1 asubuhi Jumatano CET. Saa 5 usiku wa Jumanne, El Tigre anahamishwa (na ndege binafsi) kutoka katika milima ya Tijuana (alikokuwa amejificha) mpaka katika jumba la kifahari la Eduardo Chapa de Christopher (Mkurugenzi wa Usafirishaji wa Kolonia Santita) nje ya Salina Cruz – ambako Chui anafika saa 10 alfajiri na kuendesha kikao cha dharura cha Bodi ya Wakurugenzi ya Kolonia Santita.” MexicoTuesdayTigerCopenhagenPrivate JetMansionTijuanaMeksikoEl TigreSalina CruzEduardo Chapa De ChristopherJumanneKikao Cha Dharura04 00 Hrs22 00 Hrs23 00 Hrs7 Hours9 HoursChuiCstEmergence MeetingJumba La KifahariKaskazini MagharibiKusini MagharibiMasaa 7Masaa 9Mauaji Ya MeksikoMexican MassacreMilima Ya TijuanaNdege BinafsiNorth WestPstSaa 10 AlfajiriSaa 4 UsikuSaa 5 UsikuSouth WestTijuana Mountains Book:Kolonia Santita Source: Kolonia Santita