Quotessence
Home / Topics / Mti Wa Maarifa Ya Mema Na Mabaya Quotes

Mti Wa Maarifa Ya Mema Na Mabaya Quotes

Browse 3 quotes about Mti Wa Maarifa Ya Mema Na Mabaya.

Mti Wa Maarifa Ya Mema Na Mabaya Quotes

“Mungu hakutuumba ili tuwe roboti, ambayo hufanya kazi kama ilivyoelekezwa. Alituumba ili tuwe huru. Yaani, tuwe na uwezo wa kuchagua mema au mabaya – ndiyo maana akaweka Mti wa Maarifa ya Mema na Mabaya katika Bustani ya Edeni – ndiyo maana akamtuma Shetani kuwajaribu Adamu na Hawa, wazazi wetu wa kwanza.”

“Maamuzi ya Adamu na Hawa ya kutokumtii Mungu juu ya Mti wa Maarifa ya Mema na Mabaya, ndiyo yaliyosababisha Yesu Kristo ajitolee maisha yake ili wengine waweze kuishi. Hakuna Mungu bila Yesu. Mtafute Yesu, kukomboa sura na asili ya Mungu.”

“Kuwepo kwa Mti wa Uzima wa Milele katika Bustani ya Edeni (pamoja) na Mti wa Maarifa ya Mema na Mabaya inamaanisha, Adamu na Hawa walikuwa hai kiroho mpaka walipokula tunda la mti wa katikati ambapo hali yao ya maisha ilibadilika. Adamu na Hawa walikufa lakini hawakufa – walikufa baadaye kabisa. Hii inamaanisha kwamba (haya ni mawazo yangu tu) mtu anapokufa anakuwa amekula tunda la mti wa katikati, litakalomwezesha kuendelea kuishi katika hali nyingine ya maisha ambayo sisi hatuijui.”