“Lakini kabla Rais hajaendelea kuongea, na ‘John Murphy wa Kolonia Santita’, Mogens aliruka na kumnyang’anya simu. “Ambilikile,” Mogens aliita, akiangalia saa. “Brodersen,” Sauti ya upande wa pili ilijibu, baada ya sekunde kumi. “60111906,” Mogens alisema, baada ya sekunde kumi. “57121906,” Sauti ya upande wa pili ikajibu, baada ya sekunde kumi. “Jumapili,” Mogens aliendelea, baada ya sekunde kumi. “Ijumaa,” Sauti ya upande wa pili ikajibu, baada ya sekunde kumi. John Murphy wa Kolonia Santita aliposema ‘Ijumaa’, Mogens aliunda kicheko na kurusha mkono katika matundu ya kuongelea ya simu ...” PresidentVoiceLaughterHolesSundayFridayMurphyHandWatchKolonia SantitaJohn MurphyTelephoneJohn Murphy AmbilikileSautiSimuIjumaaJumapiliRais Wa Tume Ya DuniaFrederik MogensSaaMogensRaisAmbilikileMkono5712190660111906BrodersenKichekoMatunduPresident Of WodeaSekunde KumiTen Seconds Book:Kolonia Santita Source: Kolonia Santita
“Ghillie ni mavazi yaliyotumiwa na makomandoo wa Tume ya Dunia ya Kudhibiti Madawa ya Kulevya (Frederik Mogens, Radia Hosni, Daniel Yehuda na John Murphy) kama mbinu ya kujificha kwa kujifananisha na rangi au maumbo ya mazingira ya Msitu wa Benson Bennett, kama afanyavyo kinyonga. Hata hivyo, walivyoingia katika jumba la utawala katika maabara za Kolonia Santita ndani ya Msitu wa Benson Bennett katika mji wa Salina Cruz, Vijana wa Tume walivua suti zao za ghillie; kusudi iwe rahisi kwao kupambana na jeshi binafsi la Kolonia Santita, liitwalo 'autodefensa'.” TechniqueForestChameleonCamouflageCommandosJohn MurphyTume Ya DuniaVijana Wa TumeSalina CruzWorld CommissionAdministration BlockDaniel YehudaFrederik MogensRadia HosniMakomandooMsitu Wa Benson BennettBenson BennettMbinuThe Benson Bennett JungleAutodefensaGhillieGhillie SuitJeshi BinafsiJumba La UtawalaKamaflejiKinyongaKolonia Santita LaboratoriesMaabara Za Kolonia SantitaMsituPrivate ArmySuti Za Ghillie Author:Enock Maregesi
“Ujanja wote ulimwisha Murphy. Ilimbidi kutoboa siri ili adui asizidi kumuumiza. Alilaumu mno kufa wakati alishakula ng’ombe mzima. Alifikiri Mogens na Yehuda walishauwawa kulingana na hasira nyingi za magaidi. Walihakikisha hawafanyi makosa hata kidogo. Alivyomaliza kumhoji, yule adui alizunguka nyuma katika mgongo wa Murphy na kwenda katika dirisha lililokuwa wazi – la mashariki – ambapo aliegemea na kuvuta sigara. Alichungulia kidogo nje kisha akageuka na kuendelea kupata upepo mdogo wa baridi.” WindWindowEastSecretsCigaretteCriminalBackTerroristsSiriJohn MurphyJohn Murphy AmbilikileAduiMagaidiSigaraDaniel YehudaFrederik MogensDirishaUpepoMasharikiMgongo Book:Kolonia Santita Source: Kolonia Santita
“Wakiwa na suti nzito za kijani na madoa meusi (‘Ghillie Suits’) kwa ajili ya kupigania porini; Vijana wa Tume walikuwa na kofia za chuma, miwani ya kuonea usiku (iliyokuwa na uwezo wa kubinuka chini na juu), redio na mitambo ya mawasiliano migongoni mwao juu ya vizibao vya kuzuia risasi, vitibegi vya msalaba mwekundu (‘Blowout Kits’ – katika mapaja ya miguu yao ya kulia, ndani yake kukiwa na pisto na madawa ya huduma ya kwanza), vitibegi vya kujiokolea (‘Evasion Kits’ – katika mapaja ya miguu yao ya kushoto, ndani yake kukiwa na visu na pesa na ramani ya Meksiko) na bunduki za masafa marefu. Kadhalika, Vijana wa Tume waliamua kuchukua Punisher – waliyoafikiana baadaye kuwa ilikuwa nzuri kuliko RPG-7, ‘Rocket Propelling Gun’, ambayo Mogens alipendekeza waitumie kubomolea Kiwanda cha Dongyang Pharmaceuticals; kwa sababu hakutaka kuleta madhara kwa watu waliokuwa hawana hatia.” PeopleNightMoneyEffectsGreenRadioGuiltyKnivesMexicoBulletsMedicationRiflesThighsWatuMapSuitPesaPistolGogglesPunisherVijana Wa TumeFirst AidMeksikoRisasiMadharaFrederik MogensUsikuMadawaRedioBlowout KitsEvasion KitsMogensPistoVisuVitibegi Vya KujiokoleaVitibegi Vya Msalaba MwekunduBullet Proof VestsBunduki Za Masafa MarefuGhillie SuitsHatiaKofia Za ChumaMitambo Ya MawasilianoMsalaba MwekunduRamaniVizibao Vya Kuzuia RisasiCommunications EquipmentKijaniMadoa MeusiMapajaMiwaniRocket Propelling GunRpg 7Suti Book:Kolonia Santita Source: Kolonia Santita
“Radia Hosni alikuwa na bahati kuliko watu wote duniani. Frederik Mogens alipofika katika helikopta na kukuta Murphy na Yehuda wakihangaika kuutafuta mwili wa Radia, hakushangazwa na walichomwambia. Kwa sababu alijua nini kilitokea. Radia alikutwa akipumua kwa mbali. Hivyo, Debbie na marubani walimchukua na kumpeleka Mexico City haraka ilivyowezekana. Black Hawk waliyokuwa wakiishangaa ilikuwa ya DEA. Lakini si ile waliyokwenda nayo Oaxaca. Ilikuwa nyingine ya DEA, iliyotumwa na Randall Ortega kuwachukua Vijana wa Tume na kuwapeleka Mexico City haraka ilivyowezekana. Black Hawk waliyokwenda nayo Oaxaca ndiyo iliyomchukua Radia na Debbie na kuwapeleka Altamirano (hospitali ya tume) mjini Mexico City. Mogens angekwenda pia na akina Debbie; lakini alibaki kwa ajili ya kumlinda El Tigre, na mizigo yake, na baadhi ya makamanda wake wachache. El Tigre angeweza kutoroka kama angebaki na polisi peke yao, na Mogens hakutaka kufanya makosa.” BodyLuckMistakesPilotsCommandersHospitalMurphyCargoMexico CityMwiliHelicopterVijana Wa TumeDebbieDeaOaxacaMakosaEl TigreFrederik MogensRadia HosniBahatiBlack HawkHelikoptaMakamandaMogensAltamiranoHospitali Ya TumeMarubaniMizigoRandall OrtegaYehuda Book:Kolonia Santita Source: Kolonia Santita