“Musa alipokuwa mlimani kupokea Amri Kumi za Mungu kwa ajili ya Wana wa Israeli alikawia sana kurudi, kiasi cha watu kukata tamaa na kujiona wapweke wakiwa njiani kuelekea katika Nchi ya Ahadi. Kutokana na woga usio na kifani na kukata huko kwa tamaa waliamua kutosubiri tena kusikia neno kutoka kwa Mungu, au kuiona sura halisi ya Mungu kama Musa alivyokuwa amewaahidi, hivyo wakamlazimisha Haruni awatengenezee mungu kutokana na taswira ambayo tayari walishakuwa nayo vichwani mwao kuhusu mungu waliyemtaka; yaani ndama wa dhahabu, au mungu mpya ambaye angewapa chochote walichotaka muda wowote waliotaka.” PeopleGodDespairLonelyMosesWordImageMunguPromised LandWatuAaronMusaAnytimeAmri Kumi Za MunguKukata TamaaNenoTaswiraWana Wa IsraeliThe Ten CommandmentsNew GodTrue FaceWapwekeChildren Of IsraelExtraordinary FearGolden LambHaruniIn Their HeadsMlimaniMuda WowoteMungu MpyaNchi Ya AhadiNdama Wa DhahabuOn The MountainSura HalisiVichwani MwaoWoga Usio Na Kifani Author:Enock Maregesi
“Nini kingetokea kama Adamu na Hawa wasingekula tunda la Mti wa Maarifa ya Mema na Mabaya mpaka siku ya Sabato? Mungu angewaruhusu kula na lengo la uumbaji wa Mungu lingekamilika. Wanadamu wakifuata Amri Kumi za Mungu katika maisha yao watakuwa na uwezo maalumu ambao baadaye utawawezesha, kupitia Roho Mtakatifu, kuwa na maarifa ya siri ya uumbaji wa Mungu.” MenLifeGodKnowledgeCreationCapacityFruitHoly SpiritAdamSabbathTen CommandmentsMunguMaishaEveMaarifaSabatoUwezoWanadamuRoho MtakatifuGod S CreationAdamuHawaAmri Kumi Za MunguTundaUumbajiUumbaji Wa MunguMti Wa Maarifa Wa Mema Na Mabaya Author:Enock Maregesi
“Kukiuka Amri Kumi za Mungu si dhambi ni matawi ya dhambi. Dhambi ni kumkana Mungu na kumkubali Shetani.” GodSatanBranchesCommandmentsTen CommandmentsMunguSinsShetaniDhambiAmri Kumi Za MunguAmriMatawi Author:Enock Maregesi
“Ufalme wa mbinguni uko juu. Akili ya binadamu iko juu. Kupata Amri Kumi za Mungu, Musa alipanda juu katika mlima Sinai. Yesu alijaribiwa na Shetani akiwa juu katika jangwa la Yuda. Ukifanikiwa tunasema uko juu. Tai hawezi kuona vizuri akiwa chini anaweza kuona vizuri akiwa juu. Ulaya na Amerika tunaita majuu kwa sababu ziko juu ya ikweta. Kwa nini juu? Kwa sababu juu kuna utukufu.” MindJesusMosesTen CommandmentsYesuAkiliThe Kingdom Of HeavenMusaAmri Kumi Za MunguUfalme Wa Mbinguni Author:Enock Maregesi
“Sabato ilianzishwa na Mungu siku ya saba ya uumbaji wake. Siku ya Sabato ni siku takatifu, iliyoko katika Amri Kumi za Mungu, ambayo hatuna budi kuitunza na kuiheshimu. Sheria ya Siku ya Sabato haikufa baada ya kifo cha Yesu Kristo msalabani kama Wakolosai wanavyodai. Wakolosai walifuata falsafa za kipagani, na walizileta falsafa hizo ndani ya mwili wa Kristo ambalo ni kanisa. ‘Usiiamini’ Wakolosai 2:17. Iamini Wakolosai 2:20-23, ambapo Paulo anafundisha Mataifa jinsi ya kuitunza Sabato, na 1 Wakorintho 12:27 ambayo inatoa maana halisi ya Wakolosai 2:17. ‘Mwili wako ni wa Kristo’ ni tofauti na ‘mwili wa Kristo’ na ni tofauti na kanisa. Ukiamini kama mwili wako ni wa Kristo na ni kanisa, utaitunza Sabato.” GodBodyDeathChurchCreationJesus ChristSabbathTen CommandmentsMunguGentilesPaulYesu KristoMwiliSabatoKifoColossiansPauloAmri Kumi Za MunguKanisaMataifaUumbaji1 Corinthians 12 271 Wakorintho 12 27Christ S BodyColossians 2 17Colossians 2 20 23Falsafa Za KipaganiHoly DayLaw Of The SabbathMwili Wa KristoPagan PhilosophiesSeven S DaySheria Ya Siku Ya SabatoSiku TakatifuSiku Ya SabaWakolosaiWakolosai 2 17Wakolosai 2 20 23 Author:Enock Maregesi
“Hakimu na Kuhani Mkuu wa Shilo Eli alipata matatizo makubwa wakati wa mgogoro wa Waisraeli na Wafilisti, kati ya mwaka 2871 na 2870 Kabla ya Kristo. Mara tu baada ya kupewa taarifa ya kifo cha watoto wake wawili, Hofni na Finehasi, na kutwaliwa kwa Sanduku la Agano la Bwana wa Majeshi lililohifadhi Amri Kumi za Mungu, Eli alianguka kutoka katika kiti chake na kufariki papo hapo akiwa na umri wa miaka 98. Aidha, mkwe wa Eli, mke wa Finehasi, alijifungua ghafla na kufariki alipopata taarifa ya kifo cha mkwewe na taarifa ya kuuwawa kwa mumewe na ya kutekwa nyara kwa Sanduku la Agano. Mwanajeshi kutoka Benyamini falaula angetumia hekima na busara kutoa taarifa ya kifo na ya kutwaliwa kwa Sanduku la Agano huenda Eli asingefariki, na huenda mkwewe asingejifungua mtoto njiti na huenda asingekufa siku hiyo. Kwani Sanduku la Agano lilirejeshwa nchini Israeli, na Wafilisti wenyewe, baada ya miezi saba tangu litwaliwe, na kifo cha watoto wa Eli yalikuwa mapenzi ya Mungu. Hivyo Eli asingeweza kuzuia kifo cha watoto wake, na Wafilisti wasingeweza kukaa na Sanduku la Agano milele. Lakini katika kafara ya Isaka ambapo Isaka aliamua kujitoa kafara mwenyewe kumfurahisha Mungu na baba yake kama Yesu alivyoamua kujitoa kafara mwenyewe kumfurahisha Mungu na baba yake wa mbinguni, Sara angekufa kama Ibrahimu hangetumia hekima alipomwambia anakwenda kumtolea Bwana kafara ya mwanakondoo wakati akijua anakwenda kumtoa Isaka mtoto wa pekee wa Sara. Hekima inatoka moyoni, busara inatoka mdomoni. Kwa vile suala la kutoa taarifa mbaya kwa mtu ni gumu kwa yule anayetoa na kwa yule anayepokea, hekima na busara havina budi kutumika.” JesusAbrahamTen CommandmentsIsaacSarahYesuEliSaraArk Of The CovenantPhineasAmri Kumi Za MunguIbrahimuHekima Na BusaraIsakaWisdom And InsightBefore ChristDeath AnnouncementSanduku La AganoTaarifa Ya Kifo98 Years OldBenjaminite SoldierBetween 2871 And 2870Hakimu Na Kuhani Mkuu Wa ShiloHer HusbandHofni Na FinehasiIsraeli Conflict With PhilistineJudge And High Priest Of ShillohKabla Ya KristoKati Ya Mwaka 2871 Na 2870Mke Wa FinehasiMumeweMwanajeshi Kutoka BenyaminiPhineas WifeUmri Wa Miaka 98 Author:Enock Maregesi