Quotessence
Home / Topics / Faida Quotes

Faida Quotes

Browse 8 quotes about Faida.

Faida Quotes

“Hasira ni Shetani. Hekima ni Mungu. Kila kitu kimo ndani yetu. Hasira imo ndani yetu. Hekima imo ndani yetu. Atomu ni matofali ya ujenzi wa kila kitu ulimwenguni likiwemo jua na miili ya wanadamu. Ndani ya atomu kuna nguvu ya chanya na kuna nguvu ya hasi. Kama miili yetu imetengenezwa na atomu na katika kila atomu kuna nguvu ya chanya na kuna nguvu ya hasi, hivyo basi, tuna uwezo mkubwa wa kufanya mambo mazuri na tuna uwezo mkubwa wa kufanya mambo mabaya. Mtu akikutukana mwambie asante. Akikupiga mwambie asante. Akiendelea kukupiga, pigana. Geuza hasira yako kuwa hekima kwa faida yako na kwa faida ya wengine.”

“Kila binadamu hapa duniani ni wa thamani kubwa. Chochote utakachofanya, kizuri au kibaya, kidogo au kikubwa, kitabadilisha maisha ya watu. Ukiwa na msingi mzuri kwa mwanao ataishi vizuri atakapokuwa mkubwa, atakuwa na uwezo mkubwa wa kuacha dunia katika hali nzuri kuliko alivyoikuta. Ukiwa na msingi mbaya kwa mwanao ataishi vibaya atakapokuwa mkubwa, atakuwa na uwezo mdogo wa kuacha dunia katika hali nzuri kuliko alivyoikuta. Kuwa mkarimu kwa mazingira, kuwa mkarimu kwa wanyama, kuwa mkarimu kwa binadamu wenzako, kwa faida ya vizazi vijavyo.”

“Afrika isomeshe watu wake, na itumie vizuri mapato yanayotokana na mauzo ya rasilimali zake kwa faida ya jumla ya wananchi wa nchi zake, kusudi baadaye wawe wataalamu wa rasilimali za nchi zao wenyewe, kuepukana na utumwa wa rasilimali. Rasilimali za Afrika zina miiko na masharti yake.”

“Maana halisi ya ukarimu si kutoa vitu au mali nyingi kwa watu wanaohitaji msaada, bali ni kutoa vitu au mali hizo bila kinyongo au unafiki wowote. Ukarimu unapaswa kutolewa kwa watu sahihi, wakati sahihi, kiasi sahihi na kwa moyo mmoja bila kinyongo chochote. Ukitoa kwa lengo la kupata faida, huo ni ubinafsi na unafiki mkubwa.”