Quotessence
Home / Authors / Enock Maregesi

Enock Maregesi Quotes

Author

Filter quotes by topic

Famous Enock Maregesi Quotes

“Tunapaswa kujisikia furaha kuu tunapokumbana na majaribu mbalimbali katika maisha yetu, tukijua kwamba kujaribiwa kwa imani yetu hutufanya wavumilivu na wapiganaji katika Jina la Yesu, na tunapaswa kuruhusu uvumilivu katika maisha yetu kwa sababu Mungu hutumia uvumilivu huo kutukomaza na kutukamilisha.”

“Marafiki zako wa mwanzo ambao bado ni marafiki zako mpaka sasa ni wazuri kuliko wote kutokana na sababu mbalimbali: Wamekuwepo pamoja nawe katika shida na raha; wanakujua vizuri unapokuwa na furaha, na wanakujua vizuri unapokuwa na huzuni; mmezoeana kwa miaka mingi na wanaujua hata utani wako wa ndani; wanajua nini unapendelea zaidi na nini hupendelei zaidi, na wanazijua sifa zako za ushupavu na sifa zako za udhaifu. Hata hivyo, katika maisha yetu, tunahitaji marafiki wa aina zote mbili kurahisisha maisha. Marafiki wapya hutuongezea viungo muhimu katika maisha yetu wakati marafiki wa mwanzo ni nguzo au miamba imara ya maisha yetu, na ndiyo watu hasa watakaotusaidia katika shida na raha! Usiwapoteze au usiwaache marafiki zako wa mwanzo lakini jenga mahusiano mapya. Marafiki zako wa mwanzo ni dhahabu, wa sasa ni fedha.”

“Sikujui. Lakini naamini hungependa kuishi maisha yako hapa duniani bila kuacha urithi au kumbukumbu ya aina yoyote katika jamii. Zifuatazo ni ngazi tano muhimu zitakazofanya uache dunia katika hali nzuri kuliko ulivyoikuta: Tambua vitu vya muhimu katika maisha yako ijapokuwa unaweza kuacha alama katika dunia bila kujitambua baada ya kuondoka; Tumia kipaji ulichopewa na Mungu; Fanya kazi kwa bidii na maarifa; Shindana na wenzako kuwa juu zaidi katika tasnia uliyojichagulia; Kuwa makini na kila kitu unachofanya kwa maana ubongo ni kitu cha ajabu, ubongo una uwezo wa kukupotosha.”

“Ukitambua vitu vya muhimu katika maisha yako hapa duniani na kuvipa kipaumbele cha kwanza, ukatumia kipaji ulichopewa na Mungu na ukafanya kazi kwa bidii na maarifa, halafu ukashindana na wenzako kuwa juu zaidi katika tasnia uliyojichagulia, ukafanya kila kitu kwa makini ukihofia maamuzi ya ubongo wako, utaacha urithi kwa faida ya vizazi vijavyo. Kuwa na akili, kuwa na uwezo wa kujiwekea malengo, kuwa mchapakazi hodari. Namna hiyo, hakuna kitakachoweza kushindikana.”

“Kufanikiwa katika maisha lazima kitu fulani ambacho si cha kawaida kitokee katika maisha yako, bila kujali uko upande wa Yesu au upande wa Shetani. Kufanikiwa katika maisha ni sawa na kwenda mbinguni, au kuishi mbinguni duniani. Kitu ambacho si cha kawaida kutokea katika maisha yako ni sawa na kifo. Fanya kitu ambacho hujawahi kufanya kupata kitu ambacho hujawahi kupata.”

“Adam Kuambiana umerudi nyumbani ulikotoka, ukiongozwa na imani na mwanga wa wale uliowapenda na kuwapoteza. Hatuwezi kukumbuka kwamba umetutoka bila kukumbuka kwamba uliishi, na kwamba maisha yako yalitupa kumbukumbu nzuri tusizoweza kuzisahau haraka. Jumanne, siku ya kuuaga mwili uliokuwa ukitumiwa na wewe, wengine watasema Kwa heri lakini mimi nitasema Asante! Asante kwa sababu ya kipaji chako. Asante kwa sababu ya kujitahidi kwa kadiri ya uwezo wako wote, kutoa sauti kwa wale wote waliokuwa hawawezi kusikika. Asante kwa sababu ya kuacha dunia katika hali nzuri kuliko ulivyoikuta wakati ukiingia, na Asante kwa sababu ya maisha yako. Tukiendelea kuomboleza kifo cha Adam Kuambiana hapa duniani, wengine wanasherehekea kukutana naye huko mbinguni. Mchungaji wa uhai wa wote Mungu wa mbinguni ailaze roho yake mahali pema peponi: Yeye ni mwandishi wa hadithi ya maisha yetu na ndiye aliyeandika ukurasa wa mwisho wa hadithi ya Adam.”

“Hakuna uponyaji pasipo imani ya kweli. Giza linapoingia katika maisha yako ongea na Mungu. Halafu ongea na tatizo linalokusumbua. Kama tatizo linalokusumbua ni saratani, iambie saratani iondoke na kamwe isirudi katika mwili wako tena. Baada ya hapo, nenda kwa mchungaji. Jiweke wakfu, kwanza, kabla ya kuombewa.”