“Shetani lengo lake ni kutawala dunia. Huwezi kutawala dunia bila elimu!” WorldPurposeEducationSatanDuniaShetaniElimuLengo Author:Enock Maregesi
“Shetani ni mjanja sana. Anajua bila elimu hataweza kutawala dunia, baada ya mpango wa Mungu kukamilika. Anajua, mtu akipata elimu ni rahisi sana kujua kama Shetani hayupo. Hivyo Shetani atatimiza malengo yake bila watu kujua.” WorldGodEducationSatanMunguDuniaShetaniElimu Author:Enock Maregesi
“Shetani ni mungu wa dunia hii kwa wale wasiomwamini Mungu. Kwa wale wanaomwamini Mungu, Mungu ndiye Mungu wa dunia hii.” WorldGodSatanMunguDuniaShetaniBelievers In GodNone Believers In GodWanaoamwamini MunguWasioamwami Mungu Author:Enock Maregesi
“Ukila kiapo fanya kile ulichoahidi katika kiapo, si kinyume chake hata kidogo, hata kama dunia haitakubaliana na wewe.” WorldYouOathDoDuniaWeweFanyaKiapo Author:Enock Maregesi
“Kuleta mabadiliko katika dunia si lazima upate nafasi katika dunia. Kuleta mabadiliko katika dunia leta mabadiliko katika nchi yako.” WorldCountryChangePlaceDuniaNchiMabadilikoNafasi Author:Enock Maregesi
“Tajiri asiyesoma lakini anayejali mambo ya ufalme wa Mungu kuliko anavyoijali dunia au yule aliyesoma lakini anayejali mambo ya ufalme wa Mungu kuliko anavyoijali dunia ni msomi. Anaweza kuuona ufalme wa Mungu.” WorldRichEducatedDuniaTajiriGod S KingdomMsomiUfalme Wa Mungu Author:Enock Maregesi
“Mwili wako una uwezo wa kujua kabla yako kitakachotokea baadaye. Kama una njaa kwa mfano, mwili wako utakwambia. Kama una kiu, mwili wako utakwambia. Kama unaumwa, mwili wako utakwambia. Kama kuna kitu kibaya kinatarajia kutokea katika maisha yako au katika maisha ya mtu mwingine, mwili wako utakwambia. Kuwa makini na alamu zinazotoka ndani ya mwili wako, kwani hizo ni ishara za Roho Mtakatifu kukuepusha na matatizo ya dunia hii.” WorldLifeBodyDiseaseManProblemsSignalsThirstySignsOmenDuniaMaishaDaemonMtuMatatizoMwiliRoho MtakatifuHangerUgonjwaAlamuKiuNjaaDaliliIsharaJakamoyo Author:Enock Maregesi
“Dunia imekata tamaa. Matatizo ya watu yamekuwa makubwa kuliko ukombozi wa maisha yao. Sekunde moja ya toba inaweza kukupa ufalme wa mbinguni. Hujachelewa.” PeopleWorldLifeSalvationRepentanceProblemsKingdom Of HeavenDuniaMaishaWatuSecondMatatizoSekundeDunia Imekata TamaaUfalme Wa MbinguniWorld Has Given UpTobaHujachelewaUkomboziYou Are Not Late Author:Enock Maregesi
“Unapofikia hatua ya kuwa na kila kitu katika maisha, unapokuwa umefanya kila kitu ulichotamani kufanya katika maisha, unakuwa na bahari nzima ndani ya tone ambalo ni wewe. Unaridhika. Wewe si tone tena ndani ya bahari, wewe ni bahari ndani ya tone. Kinachobaki baada ya hapo ni kusaidia jamii iliyosaidia kukulea ulipokuwa mdogo, kuacha alama katika dunia kabla na baada ya wewe kuondoka, bila kujali watu watasema nini juu ya maisha yako.” PeopleWorldSocietyOceanToneYouDuniaWatuDropWeweJamiiBahariBahari Ndani Ya ToneEverything In LifeKila Kitu Katika Maisha Author:Enock Maregesi
“Mbegu zilizopandwa kwenye udongo wenye rutuba ni rahisi sana kuvamiwa na magugu iwapo mwenye bustani hataipalilia bustani yake kila siku. Kila siku tunapaswa kupalilia bustani zetu za kiroho, kuondoa magugu ambayo ni raha za dunia hii.” WorldGardenSeedsSoilDuniaWeedsMbeguUdongoBustaniMagugu Author:Enock Maregesi
“Yesu Kristo wa Nazarethi ni mtu mashuhuri zaidi kuliko wote kuwahi kukanyaga ardhi ya dunia hii. Alikufa majira ya saa 9 kamili za mchana, siku ya Jumatano, katika kipindi cha demani cha AD 31. Saa chache baadaye, jua lilipokuwa likizama, alilazwa katika kaburi jipya la Yusufu wa Arimathaya. Katika siku ya kawaida ya Sabato, Jumamosi, siku tatu kamili baada ya mazishi yake, Mungu Baba alimfufua Mtoto Wake kwa ajili ya uzima wa milele.” WorldWednesdayDuniaSabatoJesus Christ Of NazarethJumatanoAd 31Joseph Of ArimatheaYesu Kristo Wa NazarethiYusufu Wa Arimathaya Author:Enock Maregesi
“Utajiri wa mbinguni ni wa milele na mungu wake ni Yehova. Utajiri wa duniani ni wa muda na mungu wake ni Mammon. Mammon, ambaye hata Yesu alimtaja katika Injili ya Mathayo 6 na katika Injili ya Luka 16, ni mungu wa uchoyo na utajiri wa dunia hii. Mammon kazi yake ni kufanya watu waliokufa kifedha na walio hai kifedha kuwa maskini wa milele ahera. Yesu Kristo alikuwa maskini, ili tuwe matajiri kupitia umaskini wake, lakini kwa sababu alikuwa na imani ya Mungu katika moyo wake alikuwa tajiri. Hivyo unaweza kuwa na utajiri wa mbinguni hapa duniani, ukiikaribisha amani ya Mungu katika moyo wako.” WorldHeartGodTimeJesusHeavenPeaceWealthPoorPovertyHellJesus ChristGreedWealthyGospelJehovahMunguDuniaEverAmaniYesu KristoYesuMaskiniTajiriMoyoMudaMbinguniUtajiriInjiliDunianiMammonUmaskiniMileleMatajiriAheraGod S FaithUchoyoYehovaImani Ya MunguLuka 16Luke 16Mathayo 6Matthew 6 Author:Enock Maregesi
“Shetani alikuwa malaika aliyeumbwa na Mungu lakini baadaye akamwonea Mungu wivu, wivu wa madaraka, hivyo Mungu akamtupa duniani kwa sababu ya kupingana na utawala wake mtakatifu. Duniani Shetani akamtumia nyoka kama mdakale kumdanganya Hawa. Hawa na Adamu wakamsikiliza Shetani badala ya kumsikiliza Mungu, nao wakalaaniwa. Shetani akajidai kuwa alikuwa na uwezo wa kufanya uzao wote wa Adamu na Hawa uwe mbali na Mungu, hivyo Mungu akampa muda wa kujaribu na kuthibitisha madai yake, lakini Shetani mpaka leo bado hajafanikiwa. Wakiitawala dunia leo kwa udanganyifu wa hali ya juu, pamoja naye, ni baadhi ya malaika ambao Shetani alifanikiwa kuwalaghai huko mbinguni. Mungu akawalaani pia na kuwatupa huku duniani, ambako Shetani alipapenda zaidi.” WorldGodTimeHeavenPowerClaimsEnvySatanDeceitAdamAngelsOffspringSerpentMunguRuleDuniaShetaniEveMouthpieceMudaMbinguniMalaikaAdamuHawaMadarakaUtawalaNyokaWivuUdanganyifuUzaoMadaiMdakaleRightful RulershipUtawala Mtakatifu Author:Enock Maregesi
“Dunia nzima imejaa giza! Kupenya lazima uwe jasiri.” WorldDarknessBraveryDuniaGizaUjasiri Author:Enock Maregesi