Quotessence
Home / Authors / Enock Maregesi

Enock Maregesi Quotes

Author

Filter quotes by topic

Famous Enock Maregesi Quotes

“Wakati Yuda ikiongozwa na kiongozi mzuri na mwenye haki kama Yosia, taifa lilistawi. Lakini ilipokuwa chini ya mwovu Manase, taifa lilisambaratika. Katika karne hii, Uingereza ilipata msukosuko mkubwa mwaka 1936 juu ya uamuzi wa Edward VIII kuoa mwanamke wa Kimarekani aliyekuwa mtalaka Wallis Simpson. Uamuzi huo ulisababisha matatizo makubwa ya kikatiba, na nusura serikali ya Uingereza ijiuzuru. Hata hivyo, kaka yake mdogo, George VI, kwa mapenzi makubwa na nchi yake, huku akikataa katakata kuondoka London wakati wa Vita Kuu ya Pili ya Dunia, aliliongoza taifa hilo katika kipindi kigumu zaidi kuliko vyote katika historia ya Uingereza. Kanuni hii ya uongozi ina ukweli katika jambo lolote kubwa na hata dogo la ujasiri.”

“Sanjay Kanaka Ramachandra, 'The Satellite', baada ya kutoka Korea ya Kaskazini na Salina Cruz kwa ajili ya kozi maalumu ya ugaidi na kwa ajili ya Kiapo cha Swastika kwa mpangilio huo, alirudi Mumbai kusimamia shughuli za Kolonia Santita za bara la Asia na Australia – kwa uaminifu wa Sheria ya Kitalifa ya Kolonia Santita. Ramachandra, anayeitwa 'The Satellite' kwa sababu ya jina lake la mwisho, alipewa pia jukumu la kuyachunga Makao Makuu ya Kanda ya Asia-Australia ya Tume ya Dunia; na kupeleka taarifa yoyote ya kijasusi (inayohusiana na WODEC-Rangoon) Mexico City kwa ajili ya maamuzi ya Mkurugenzi wa Usalama wa Kolonia Santita Gortari Manuel. Mojawapo ya operesheni kubwa alizowahi kuzifanya Ramachandra kwa niaba ya Kolonia Santita ni kuingiza nchini India mzigo wa tani 350 za majani ya koka, ijapokuwa tani 37 zilikamatwa na mamlaka za kuzuia madawa ya kulevya za India na za Tume ya Dunia, na kusambaza kilo 560 za kokeini safi (isiyokuwa na doa) katika nchi zote za Asia na Australia ndani ya siku 14.”

“Vijana wa Tume walipofika kambini chini ya ulinzi mkali wakiwa na Kahima, polisi wengi walionekana kuwapigia saluti lakini wakubwa wao wakawakataza na kuwambia wao walikuwa watu wa kawaida kama wao. Walisindikizwa na lundo la polisi mpaka ndani ya jumba la utawala Murphy alimokuwa ameuhifadhi mwili wa Radia. Walipofika walishtuka, na hata kuwashangaza polisi. Mwili wa Radia haukuwepo! Walitafuta kila sehemu, na kuwambia polisi wawasaidie kutafuta, lakini Radia alishapotea. Murphy alipata wazo na kutoka nje, kwa kukimbia, polisi wengi wakimfuata; mpaka katika helikopta ya DEA ambapo alifungua mlango na kuingia ndani. Ndani ya helikopta hakukuwa na mtu!”

“Polisi wa kituo cha kati cha Coyoacán kumbe hawakuwa mbali na sehemu zile. Walipoona gari zikifukuzana waliona ujanja ni kuwakatisha Vijana wa Tume katika vichochoro. Haikuchukua muda magari sita ya polisi yalitokeza Vallarta (Barabara ya Vallarta) na kuliona gari la Vijana wa Tume Gómez Farías likipepea kwa mwendo mkali kuelekea Cuauhtémoc, na gari za magaidi kwa nyuma yao. Kwa vile Ferrari ilikuwa mbali kidogo na magari ya magaidi, polisi hawakuitilia maanani sana kwa kudhani yale mawili (ya magaidi) ndiyo yaliyokuwa yakifukuzana. Bila kuchelewa, magari mawili ya polisi yalikamata Hidalgo na kuzunguka mpaka Moctezuma halafu yakasimama ghafla katikati ya Moctezuma na Gómez Farías – katikati ya magari mawili ya magaidi na gari la Vijana wa Tume. Wakati huohuo magari mengine (manne) ya polisi yakitokea Mtaa wa Vallarta nayo yakasimama nyuma ya magari ya magaidi; hivyo kufanya magari ya magaidi yawe katikati ya magari ya polisi, na polisi wakaisahau Ferrari ya Lisa.”

“Kwa sababu za kijiografia, Copenhagen iko mbele kwa masaa 9 (PST) kuilinganisha na Tijuana (kaskazini-magharibi mwa Meksiko) na masaa 7 (CST) kuilinganisha na Salina Cruz (kusini-magharibi mwa Meksiko). Mauaji ya Meksiko yametokea saa 4 usiku wa Jumanne, Copenhagen ikiwa saa 1 asubuhi Jumatano CET. Saa 5 usiku wa Jumanne, El Tigre anahamishwa (na ndege binafsi) kutoka katika milima ya Tijuana (alikokuwa amejificha) mpaka katika jumba la kifahari la Eduardo Chapa de Christopher (Mkurugenzi wa Usafirishaji wa Kolonia Santita) nje ya Salina Cruz – ambako Chui anafika saa 10 alfajiri na kuendesha kikao cha dharura cha Bodi ya Wakurugenzi ya Kolonia Santita.”