Quotessence
Home / Authors / Enock Maregesi

Enock Maregesi Quotes

Author

Filter quotes by topic

Famous Enock Maregesi Quotes

“Kuwepo kwa Mti wa Uzima wa Milele katika Bustani ya Edeni (pamoja) na Mti wa Maarifa ya Mema na Mabaya inamaanisha, Adamu na Hawa walikuwa hai kiroho mpaka walipokula tunda la mti wa katikati ambapo hali yao ya maisha ilibadilika. Adamu na Hawa walikufa lakini hawakufa – walikufa baadaye kabisa. Hii inamaanisha kwamba (haya ni mawazo yangu tu) mtu anapokufa anakuwa amekula tunda la mti wa katikati, litakalomwezesha kuendelea kuishi katika hali nyingine ya maisha ambayo sisi hatuijui.”

“Kitu cha kwanza kufanyika mwanadamu anapozaliwa ni kuvuta pumzi ya kwanza katika mapafu ya mwili wake. Cha mwisho kufanyika kabla ya kufa ni kutoa pumzi ya mwisho katika mapafu ya mwili wake. Pumzi iliyoingia kwanza baada ya kuzaliwa, itakuwa ya mwisho kutoka kabla ya kufa. Pumzi ni bora kuliko muda halafu pumzi ni uhai. Bila uhai watu hawataweza kusherehekea mwaka mpya au kufanya chochote. Likumbuke jina la Mwenyezi Mungu katika kila pumzi unayoingiza na kutoa.”

“Kuna ushahidi wa kutosha katika maandiko kwamba Yesu aliugua hipovolimia kutokana na kuchapwa. Yesu alipobeba msalaba wake kuelekea Golgotha alianguka, na mtu mmoja aliyeitwa Simoni alilazimishwa ama kuubeba au kumsaidia Yesu kuubeba msalaba huo hadi kilimani. Kuanguka huko kunaonyesha kwamba Yesu alikuwa na shinikizo la damu. Alama nyingine inayoonyesha kwamba Yesu alipatwa na ugonjwa wa hipovolimia ni pale alipodai kuwa alikuwa na kiu, akiwa msalabani, akimaanisha kiu ya maji.”

“Mnamo mwaka 1957 Rais David Eisenhower wa Marekani (inasemekana) alipewa taarifa usiku mmoja akiwa Washington, D.C., kuhusu chombo cha ajabu kilichoanguka kwenye jangwa la Nevada huko Marekani. Ndani ya chombo kile kulikuwa na ‘aliens’ wawili, nao waliomba kuonana na Eisenhower kuhusu ujumbe waliokuja nao kutoka katika ulimwengu wao. Bila kuchelewa, Eisenhower alipanda ndege usiku huohuo mpaka Texas. Huko alichukua gari hadi kwenye eneo la kijeshi liitwalo Area 51, ambapo ndipo ule ujumbe wa ulimwengu mwingine ulipokuwa umeshikiliwa. Mkutano wa aina yake ulifanyika chini ya ardhi, kati ya Rais Eisenhower na hao viumbe wawili wa anga za mbali, chini ya tafsiri ya wanasayansi wa NASA. Walichotaka ni urafiki na dunia yetu, inayogombewa na dunia nyingi za ‘aliens’, kwa mbadala wa teknolojia kadha wa kadha ambazo sisi hatukuwa nazo. Pande zote mbili zilifikia maafikiano, wao wakitupa teknolojia, sisi tukiwapa uwezo wa kufanya majaribio ya kisayansi kwa binadamu wa dunia nzima. Hivyo kuanzia hapo ‘aliens’ wakawa na uhalali wa kuteka watu katika mazingira ya kutatanisha na kuingilia watu usiku wakiwa wamelala, katika tukio la kiulimwengu wa roho lijulikanalo kama ‘sleep paralysis’. ‘Sleep Paralysis’ ni tukio la ajabu. Mtu anapokuwa amelala mwili wake huonekana kufa ganzi, kiasi kwamba anajihisi hawezi hata kunyanyua mkono. Aghalabu hali hiyo inapotokea maana yake ni kwamba ‘aliens’ wanamchukua huyo mtu, kupitia kwenye paa la nyumba aliyolala, hadi mawinguni katika ndege yao. Ndani ya ndege wanaulaza mwili wa binadamu juu ya kitanda cha upasuaji, na kumfanyia upasuaji, ili kusoma biolojia iliyotumika kuumba wanadamu na kujua kwa nini sisi tuko tofauti na wao. Baada ya hapo wanamrudisha huyo mtu kitandani kwake, ambapo atalala usingizi wa kawaida hadi asubuhi. Atakapoamka hatajua kama alifanyiwa upasuaji. Wapo mamilioni ya watu duniani waliolalamika kutokewa na ‘aliens’, lakini serikali haziwahi kuilithibitisha hilo. Inavyosemekana, teknolojia za ‘aliens’ zinahifadhiwa na Jeshi la Marekani (Pentagon) na shirika la kijasusi la MAJI au MJ12. MJ12 ni watu 12 hatari zaidi duniani, wakiongozwa na mkurugenzi mkuu wa CIA (anayejulikana kama MJ1).”

“Kabla ya kukata roho mapigo ya kasi ya moyo aliyoyapata Yesu kutokana na mshtuko wa hipovolimia, pia yalisababisha maji kujikusanya katika vifuko vya maji au ute kandokando ya moyo na kandokando ya mapafu. Mkusanyiko huu wa maji kandokando ya moyo hujulikana kama ‘pericardial effusion’ na mkusanyiko wa maji kandokando ya mapafu hujulikana kama ‘pleural effusion’. Hii ndiyo maana baada ya Yesu kukata roho, na askari wa Kirumi kurusha mkuki katika ubavu wake, baada ya kutoboa mapafu na moyo, damu na maji vilitoka katika mbavu za Yesu kama Yohana alivyorekodi katika Injili yake. Mapafu ya Yesu na tumbo la Yesu vilijaa damu na maji. Mkuki ulivyotupwa maji yalitoka katika mapafu ya Yesu na katika tumbo la Yesu, na katika utando unaozunguka moyo wa Yesu, kutokana na kupasuka kwa moyo.”

“Robert Louis Stevenson wa Uskochi aliponukuu nahau ya ‘kamera haiwezi kudanganya’ katika kitabu chake cha ‘South Seas’ mwaka 1896, miaka 57 baada ya sanaa ya upigaji wa picha kugunduliwa, hakumaanisha tuwe asili. Hakumaanisha tusizirekebishe picha zetu baada ya kuzipiga na kuzisafisha! Alimaanisha tuwe nadhifu tuonekanapo mbele za watu au mbele ya vyombo vya habari; ambapo picha itapigwa, itasafishwa, itachapishwa na itauzwa kama ilivyo bila kurekebishwa.”

“Usiwe na wasiwasi, Peter. Hizo ni hisia zangu tu. Huwezi kuwa mpelelezi. Lakini, kusema ule ukweli, ningependa sana kuonana na John Murphy. Kuna kazi binafsi ningependa kumpa. Wewe unatoka Afrika, hujawahi kumwona?” Debbie alizidi kumshtua Murphy. “Nani?” Murphy aliuliza huku akitabasamu. “John Murphy wa Afrika.” “Sijawahi kumwona. Mbona unamuulizia hivyo?” Debbie alitulia. Kisha akarusha nywele ili aone vizuri. “Nampenda sana!” “Kwa nini?” “Simpendi kwa mahaba, lakini.” “Ndiyo. Kwa nini?” “OK. Nampenda kwa kipaji chake. Alichopewa na Mungu, cha ujasusi. Kusaidia watu.” “Ahaa!” Murphy alidakia, sasa akifikiri sana. “Murphy ana mashabiki wengi hapa Meksiko bila yeye mwenyewe kujua, kwa sababu ya kupambana na wahalifu wa madawa ya kulevya – hasa wa huku Latino. Tatizo lake haonekani. Wengi hudhani ni hadithi tu, kwamba hakuna mtu kama huyo hapa duniani.” “Hapana! Murphy yupo! Ni mfanyabiashara maarufu huko Tanzania. Lakini ndiyo hivyo kama unavyosema ... Haonekani!”

“Kutokana na utafiti wa kisayansi wa kionairolojia ambayo ni sayansi ya ndoto; wakati tumelala, sehemu yetu ya akili isiyotambua huamka na kuanza kazi; kwa kupangilia mawazo, kuanzia mawazo ya siku iliyopita, na kuimarisha mahusiano baina ya mawazo hayo na matukio ya wakati ujao, huku ikiondoa mawazo yasiyokuwa na maana, kunusuru ubongo usielemewe na msongo. Kazi hiyo hutambuliwa haraka na akili inayotambua, kwa njia ya alamu, lakini akili inayotambua inapagawa kwa sababu haijui akili isiyotambua inamaanisha nini kutuma alamu kama hizo. Kwa hiyo inajaribu kwa kadiri inavyoweza kutunga hadithi kuhusiana na vitu mbalimbali, ambayo baadaye hutafsiriwa kama ndoto. Hii ndiyo sababu tunaota ndoto za ajabu ambazo aghalabu hazina maana yoyote, na hazina maana yoyote kwa sababu hazitakiwi kuwa na maana yoyote, na hazina ujumbe wowote halisi kutoka akilini mwetu. Hayo ni matokeo ya akili kujaribu kusanisi sauti, kutoka katika akili isiyotambua.”

“Siku moja, jambo baya litatokea. Labda babu yako au mnyama wako kipenzi atafariki au shangazi yako atagundulika na kansa. Labda utafukuzwa kazi au utaachika kwa mumeo au mkeo mliyependana sana. Labda rafiki yako kipenzi atapata ajali mbaya ya gari na utatakiwa kupeleka taarifa kwa ndugu na marafiki zake. Kutoa taarifa ya jambo baya kwa mtu ni kazi ngumu sawa na kupokea taarifa ya jambo baya kutoka kwa mtu. Kama umeteuliwa kupeleka taarifa ya kifo au ya jambo lolote baya kwa mtu fanya hivyo kwa makini. Toa taarifa ya msiba au ya jambo lolote baya kwa hekima na busara kama Ibrahimu alivyofanya kwa Sara kuhusiana na kafara ya Isaka, si kama Mbenyamini alivyofanya kwa Eli kuhusiana na kutwaliwa kwa sanduku la agano na kuuwawa kwa watoto wake wawili. Jidhibiti kwanza wewe mwenyewe kama umeteuliwa kupeleka taarifa ya kifo au ya jambo lolote baya. Angalia kama wewe ni mtu sahihi wa kupeleka taarifa hiyo. Pangilia mawazo ya kile unachotaka kwenda kukisema au unachotaka kwenda kukiandika. Mwangalie machoni, si usoni, yule unayempelekea taarifa kisha mwambie kwa sauti ya upole nini kimetokea.”

“Mimi na wewe na vitu vyote ulimwenguni ni wazito kwa sababu ya 'Higgs Boson', inayojulikana pia kama 'The God’s Particle'. Wanasayansi wa CERN wamekuwa wakiitafuta 'higgs' (iliyojificha ndani ya 'higgs field') kwa zaidi ya miaka hamsini sasa, kwa bajeti ya pauni za Uingereza bilioni sita. Chembe ya 'higgs' ikipatikana itawajulisha wanasayansi jinsi ulimwengu unavyofanya kazi na jinsi ulivyoumbwa, na jibu la kitendawili cha 'Standard Model' litapatikana.”

“Kiongozi wa kanda ya Afrika ya Kusini ya Tume ya Dunia Kamishna Profesa Justin Mafuru, alijitolea maisha yake kufanya vitu viwili vya msingi kwa ajili ya dunia: Kukomesha madawa haramu ya kulevya nchini Tanzania na duniani kwa jumla, kupitia Tume ya Dunia, na kutafuta kupitia maabara za CERN ('Conseil Européen pour la Recherche Nucléaire') chembe ndogo ya 'higgs' ('Higgs Boson') inayosemekana kuhusika na uzito ('mass') wa chembe ndogo kumi na sita za atomu kasoro chembe ya mwanga; iliyopotea mara tu baada ya mlipuko wa ulimwengu wa 'Big Bang', miaka bilioni kumi na tatu nukta saba iliyopita kwa faida ya uanadamu.”

“Mungu alikuumba miaka mingi kabla hujazaliwa. Ndani ya roho yako kulikuwa na mpango mkuu wa Mungu juu ya maisha yako katika kipindi chote utakachokuwa hai, na katika kipindi chote utakachokuwa mfu. Lakini Shetani katika mji wa angani unaosemekana kuzuia majibu ya maombi ya Danieli ya siku ishirini na moja, kutoka mbinguni kuja duniani, uitwao Sadiki, wenye mashetani wenye nguvu kuliko mashetani wote katika ufalme wa giza, akaizuia roho hiyo kisha akaiwekea mpango mkuu wa Shetani juu ya maisha yako ili umtumikie yeye badala ya kumtumikia Mwenyezi Mungu. Kwa mfano, Mungu alipanga uzaliwe mkoani Arusha. Halafu akapanga mke au mume wako azaliwe mkoani Mwanza. Mkoani Arusha Mungu alipanga uwe mwinjilisti wa vitabu, wakati mkoani Mwanza alipanga mke au mume wako awe mwimbaji wa nyimbo za injili. Katika mikoa yote miwili Mungu alishatuma malaika wema wa kuwasaidia katika mipango mikuu ya maisha yenu na kuwaepusha na hila zote za adui. Lakini badala ya kuzaliwa Arusha au Mwanza Shetani ataziprogramu roho zenu upya ili wa Arusha azaliwe Dodoma au Mara au Venezuela na wa Mwanza azaliwe Lindi au Kagera au Mombasa, ambapo hakutakuwa na malaika wema wa kuwasaidia. Badala ya kuwa mwinjilisti wa vitabu, Shetani atakufanya uwe jambazi; na badala ya kuwa mwimbaji wa nyimbo za injili, Shetani atakufanya uwe mwanamuziki. Ndiyo maana wakati mwingine ni vizuri kuhama sehemu unapoishi na kwenda kuishi sehemu nyingine, ambapo kwa kusaidiana na malaika wako wa mwanzo ambaye Mungu alikupangia kabla hujazaliwa, utafanikiwa katika maisha yako, kama alivyofanya Ibrahimu. Watu wengi wanaishi maisha ambayo si ya kwao. Kukomboa kile ambacho Mungu alikipanga ndani ya roho yako kabla hujazaliwa, na kabla roho yako haijazuiwa na mashetani wa angani, kuwa karibu na Mwenyezi Mungu. Kwa Mungu hakuna siri, atakufunulia tu.”

“Mwalimu Julius Kambarage Nyerere alikuwa baba kwa familia yake. Kwa Tanzania alikuwa mlezi; wa ndoto ya haki, amani, uzalendo, ujamaa, na uhuru.”

“Radia Hosni, mhitimu wa mikanda miwili myeusi ya sanaa za mapigano za kareti na kung’fu katika ngazi ya dani mbili za kung’fu na dani moja ya kareti, mwanajeshi wa Tunisia aliyepata mafunzo ya kawaida ya kijeshi nchini Ufaransa na mafunzo ya kikomandoo nchini Uingereza kabla ya kujiunga na Tume ya Dunia, alikuwa mshindi wa tuzo ya shujaa wa taifa la Tunisia. Hussein Kashoggi alipokuwa akiwasili Tunis kutokea Copenhagen, Radia alikuwa katika Uwanja wa Mpira wa El Menzah akiangalia mechi kati ya Stade Tunisien na Espérance ST – timu ambayo mchumba wake Fathi Meoki alikuwa kocha msaidizi. Fujo zilipozuka, baada ya Stade Tunisien kufungwa bao moja kwa sifuri na Espérance ST, Radia alipanda Quadrifoglio na kuondoka kuelekea Uwanja wa Ndege wa Tunis-Carthage; ambapo alimpokea Hussein Kashoggi na jambazi wa Kolonia Santita, Delfina Moore.”

“Kipo kitu kinaendelea kufanyika katika siku zetu za furaha na katika siku zetu za huzuni kwa kila mmojawetu hapa duniani bila ya upendeleo wowote. Kitu hicho ni kuingia na kutoka kwa pumzi, au kupumua. Ukiithamini pumzi inayoingia na kutoka ndani ya mwili wako utapata zawadi ya amani katika maisha yako. Utapata pia zawadi ya furaha, uelewa na ufasaha! Ijapokuwa una matatizo mengi katika maisha, kitu bora cha kufanya ni kushukuru Mungu kwa maana wewe ni mzima.”

“Mungu akikubariki kipaji chako watu watasema ni laana. Maisha yako ni sawa na mto. Unakoelekea ni baharini. Lakini sasa umefika kwenye mlango wa bahari. Unahangaika upite wapi kufika baharini, ambapo utaogelea kwa kadiri utakavyoweza. Utakapofika baharini, watu, badala ya kusema umebarikiwa, watasema umelaaniwa, badala ya kukuita malaika, watakuita shetani. Mafanikio hayapimwi kwa pesa au mali kiasi gani unayo, mafanikio yanapimwa kwa amani ya moyo au maisha ya watu kiasi gani umeboresha.”

“Ukiwaza kwa kufuata kanuni ya nguvu ya uvutano (ambayo ni kuwaza na kuamini kama kile unachokiwaza tayari umeshakipata bila hata kujua umekipataje) utaishi kama ulivyowaza. Ukiwaza kuwa jambazi utakuwa jambazi hakika, ukiwaza kupona ugonjwa unaokusumbua utapona hakika, na ukiwaza kuwa tajiri utakuwa tajiri hakika. Mafanikio hayo yanaweza kuchukua mwezi mmoja kutimia au yanaweza kuchukua miaka kumi. Unachotakiwa kufanya ni kuwaza na kuamini.”