Quotessence
Home / Authors / Enock Maregesi

Enock Maregesi Quotes

Author

Filter quotes by topic

Famous Enock Maregesi Quotes

“Shetani ana mbinu nyingi za kuwateka wana wa Mungu. Mwanzo sura ya tatu inaonyesha jinsi Hawa alivyoona tunda linang’aa na akazama kwenye tunda pasipokujua kuna mauti ndani yake. Shetani anaangalia kipengele unachokitumia kuchukua maamuzi magumu naye anavaa jezi kama ya kwako ili usimgundue. Roho Mtakatifu akiwa anakuongoza penye hila nafsi yako itakuongoza.”

“Ningependa kujitokeza leo kutoa salamu zangu za rambirambi kwa Watu wa Musoma; kutokana na ajali mbaya ya mabasi ya J4 Express, Mwanza Coach, na gari ndogo aina Nissan Terrano, iliyotokea Ijumaa tarehe 5/9/2014 katika eneo la Sabasaba mjini Musoma. Kulingana na vyombo vya habari, watu 39 wamefariki dunia. Wengine wengi wamejeruhiwa vibaya. Mali za mamilioni ya fedha zimeteketea kabisa. Hii ni ajali mbaya na ya kusikitisha mno kwa maana halisi ya maneno mabaya na ya kusikitisha. Maneno hayataweza kuelezea kikamilifu huzuni niliyonayo juu ya ajali hii ya kutisha, lakini Mungu awasaidie wale wote waliofiwa au walioguswa na ajali hiyo kwa namna yoyote ile, na awasamehe marehemu wote dhambi zao na awapumzishe mahali pema peponi. Wale wote waliofariki hawataweza kurudi huku, lakini sisi tutakwenda huko.”

“Shetani na wafuasi wake wako kifungoni sasa hivi kwa sababu dhambi walizotenda hazisameheki. Dhambi ya kumkana Mungu na kumkubali Shetani haisameheki. Kwa maana nyingine, ukimuuzia Shetani roho yako jina lako halitaandikwa katika kitabu cha uzima litaandikwa katika kitabu cha mauti. Ukibidika kuuza roho, usimuuzie Shetani, muuzie Yesu.”

“Bibi Martha Maregesi aliishi maisha mazuri sana hapa duniani. Alibarikiwa na Mungu. Aliishi miaka 84 – siku 30660 badala ya siku 25550 tulizopangiwa na Mungu. Katika uhai wake wote, kwa wale wote aliowalea, hakuna mtoto wake hata mmoja aliyefariki kabla yake. Hakuna mjukuu wake hata mmoja aliyefariki kabla yake. Hakuna kitukuu chake hata kimoja kilichofariki kabla yake. Bibi yangu ametimiza mwaka mmoja kamili leo hii, tangu amefariki dunia Novemba 4 mwaka 2014 mjini Musoma. Tunamkumbuka leo akiwa amefariki kama tulivyomkumbuka jana akiwa hai. Nguvu ya sala zetu imfanye Mwenyezi Mungu aendelee kumsamehe dhambi zake zote, na amweke mahali anapostahili, Amina.”

“Mungu ni mtakatifu na kwa maana hiyo hatendi dhambi. Hivyo, hauwi wala hatesi. Tunajiua na kujitesa wenyewe. Ametupa hiari ya kuchagua mema au mabaya. Lakini anamtumia Shetani kama wakala wake wa kutoa adhabu kwa binadamu pale tunapoenenda sawasawa na machukizo yake. Damu ina nguvu kuliko Shetani na ina nguvu kuliko kuzimu. Unapojifunika kwa damu ya Mwanakondoo, Shetani hataweza kukuona. Hivyo, hataweza kukudhuru. Lakini usipojifunika kwa damu ya Mwanakondoo, Shetani atakuona. Hivyo, atakudhuru. Atakudhuru kwa sababu Mungu atakuwa ameruhusu akudhuru, kwa sababu ya uhuru wa kuchagua mema au mabaya aliotupatia, ijapokuwa ana uwezo wa kuzuia asikudhuru. Kwa mtindo huo Mungu anakuwa ametoa adhabu kwa binadamu.”

“Ukiua mtu bila kumwambia kwa nini unamuua anaweza kujua umemuua kwa kumwonea. Akijua umemuua kwa kumwonea roho yake inaweza kukusumbua wewe na familia yako maisha yenu yote. Makachero wa EAC wana leseni ya kuua. Lakini si kuua ovyo kama James Bond. Kila wanayemuua lazima waandike ripoti kwa nini wamemuua. Kachero wa EAC akiua mtu, kwa makosa, kwa bahati mbaya, atalindwa na Mwenyezi Mungu. Atalindwa na Tambiko la Tume ya Dunia.”

“Msamaha ni uamuzi wa makusudi wa kuachilia hisia za chuki au kisasi juu ya mtu au kikundi cha watu ambaye amekuumiza au ambacho kimekuumiza, bila kujali kama anastahili au kinastahili msamaha wako. Wataalamu wanaosoma au kufundisha msamaha huweka bayana ya kuwa, unaposamehe, hutakiwi kusitiri au kukana uzito wa kosa ulilofanyiwa. Msamaha haumaanishi kusahau wala haumaanishi kupuuza, au kujisingizia, makosa ambayo mtu amekufanyia au kikundi cha watu kimekufanyia. Ijapokuwa msamaha unaweza kusaidia kujenga uhusiano ulioharibika, haukulazimishi kupatana na mtu aliyekukosea au kumfanya asiwajibike kisheria kwa makosa aliyokufanyia. Badala yake, msamaha humletea yule anayesamehe amani ya moyo; na humpa uhuru kutokana na hasira aliyokuwa nayo, juu ya yule aliyemkosea.”

“Nyoka ni mnyama mdogo lakini anayeogopwa hata na majambazi wakubwa. Adui wa dirishani alipogeuka kumwangalia Murphy, alimwangalia pia mwenzake na kucheka bila Murphy kujua kilichofanya wafurahi. Ghafla, kuna kitu kilitokea! Nyoka mkubwa aina ya swila aliruka toka dirishani na kuanguka katika mabega ya yule adui. Adui aliruka kwa woga na kuanguka chini … halafu yakatokea maajabu! Bunduki ilifyatuka kutoka nje, ikaripuka kwa sauti ya juu, walinzi wote wa Murphy wakaruka na kuanguka chini shaghalabaghala, na kufa papo kwa papo!”

“Kirusi cha SARS-CoV-2 kina akili zaidi kuliko binadamu; kwani kinajua sehemu salama ya chenyewe kuishi ni ndani ya seli ya binadamu ambapo kitajificha na kujichanganya na mfumo wa seli, kiasi cha sayansi yote ya kibinadamu kushindwa kukiua bila kwanza kuua seli nzima! Lakini binadamu ni hatari zaidi kuliko kirusi cha SARS-CoV-2, kwa sababu binadamu huyohuyo ameshindwa kumwamini Mungu japo anamjua.”

“Ghillie ni mavazi yaliyotumiwa na makomandoo wa Tume ya Dunia ya Kudhibiti Madawa ya Kulevya (Frederik Mogens, Radia Hosni, Daniel Yehuda na John Murphy) kama mbinu ya kujificha kwa kujifananisha na rangi au maumbo ya mazingira ya Msitu wa Benson Bennett, kama afanyavyo kinyonga. Hata hivyo, walivyoingia katika jumba la utawala katika maabara za Kolonia Santita ndani ya Msitu wa Benson Bennett katika mji wa Salina Cruz, Vijana wa Tume walivua suti zao za ghillie; kusudi iwe rahisi kwao kupambana na jeshi binafsi la Kolonia Santita, liitwalo 'autodefensa'.”

“Komandoo Nicolas Kahima Kankiriho ('Kahima the Warrior') alizaliwa katika Wilaya ya Bushenyi, Ankole, kusini-magharibi mwa Uganda, Julai 24, 1954, mtoto wa tano kuzaliwa, katika familia ya watoto sita ya Nicodemas Kankiriho; mzee wa heshima wa Wabaima, aliyekuwa akisifika sana kwa uchungaji (wa mifugo) na msisitizo mkali wa ukiristo kwa watoto wake wote; hasa Kahima na Yebare, binti yake wa pekee, aliyekuwa wa mwisho kuzaliwa. Kahima (futi 6 inchi 3 aliyekuwa akiongea Kinyankole, Kiswahili, Kiingereza na Kihispania kwa ufasaha), baada ya kutoka Uganda – kwa mafunzo ya mwanzo ya ukomandoo ya Kiisraeli – alikwenda Urusi na Korea ya Kaskazini ambako aliongeza ujuzi hadi kiwango cha juu kabisa; kabla ya kwenda Amerika ya Kusini, kama askari wa msituni wa vyama vya kisiasa visivyo rasmi vya magorila wa Kolombia. Akiwa Kolombia, Kahima alikutana na Eduardo Chapa de Christopher (kiongozi wa zamani wa Kateli ya Diablos de Amazonas, Mashetani wa Amazoni, iliyokuwa ikivilinda vyama vya kisiasa vya magorila vya Americas) ambaye alimwajiri kama mlinzi binafsi na baadaye kama mlinzi binafsi wa Carlos Pulecio Alcántara – kiongozi wa kwanza wa Kateli ya Kolonia Santita. Alcántara alipouwawa, Kahima alihamia kwa Panthera Tigrisi – Kiongozi Mkuu wa Kolonia Santita.”

“Peter, naomba nitubu kosa. Mimi si mtoto wa Mwanasheria Mkuu wa Serikali. Ni mtoto wa Rais wa Meksiko. Lisa ni mtoto wa Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali,” Debbie alisema akitabasamu. “Hata mimi nilijua ulikuwa ukinidanganya. Lakini mbona Rais wa Meksiko haitwi Patrocinio Abrego?” Murphy aliuliza. “Utamaduni wa Meksiko ni tofauti kidogo na tamaduni zingine,” Debbie alijibu baada ya kurusha nywele nyuma kuona vizuri. “Hapa, watu wengi hawatumii majina ya pili ya baba zao. Hutumia jina la kwanza la mama la pili la baba; ndiyo maana Wameksiko wengi wana majina matatu. Kwa upande wangu, Patrocinio ni jina la baba yake mama yangu na Abrego ni jina la babu yake mama yangu – kwa sababu za kiusalama.”

“Kolonia Santita imesambaa dunia nzima. Hapa Meksiko wana magenge rafiki zaidi ya mia moja yakiwemo makubwa kabisa katika Latino ya Matamolos na Baja California. Nikitekwa nyara na memba yoyote wa magenge hayo, kuna uwezekano mkubwa wasinifanye chochote au nisilipe chochote kwa sababu ya Wanda. Fadhila ya uhalifu. Kwa sababu ya fadhila ya uhalifu; baba, au viongozi wengine wa serikali ambao watoto wao wamo ndani ya 'mpango' huo, wanatakiwa wawakingie kifua (kwa namna yoyote wanayoweza) pindi wanapoanguka katika mikono ya dola na sheria. Wasipofanya hivyo kutakuwa na vita ya ndani kwa ndani … kama unanielewa. Hivyo, kuna mtu anaitwa El Tigre – baba yake Wanda – ndiye ninayetaka unisaidie. Amemuua Marciano, na watu wengi wa Meksiko. Nataka kumlipia kisasi Marciano, na marafiki zangu wengi ambao El Tigre amewaua, hata kwa njia isiyodhahiri.”

“Kama miaka 1000 ya duniani ni sawa na siku moja ya Mungu; hivyo basi, miaka 930 aliyoishi Adamu ni sawa na siku 0.93 au saa 22:32 za Mungu. Kwa hiyo, ili siku ya Mungu itimie Adamu alipaswa kuishi miaka 70 (siku 0.07 au saa 1:68) zaidi! Ukiidadavua saa 1:68 unapata saa 2:08. Kulingana na muda wa mbinguni tunapaswa kuishi kwa muda wa saa 2:08! Muda huo ni mfupi sana.”

“Meja Jenerali U Nanda, 60, Kiongozi wa Kanda ya Asia-Australia ya Tume ya Dunia ya Kudhibiti Madawa ya Kulevya, alizaliwa Jumamosi ya tarehe 19/03/1932 kandokando ya mto huko Maubin nchini Bama. Yeye na familia yake ni waumini wa dini ya Ubuda. Mke wake, Daw Aung Phyu, ana miaka 57. Alizaliwa Jumapili ya tarehe 20/10/1935. Nanda na Aung Phyu wana watoto watatu. Ko Mahn Thiri (wa kiume na wa kwanza kuzaliwa) ana miaka 37. Alizaliwa Alhamisi ya tarehe 08/12/1955. Yeye na familia yake wanakaa nchini Tailandi. Ma Nang Nyi ni mtoto wa pili wa familia ya Nanda na Aung Phyu. Alikufa kwa madawa ya kulevya Jumamosi ya tarehe 12/05/1980 akiwa na miaka 23. Alizaliwa Jumamosi ya tarehe 06/04/1957. Miaka miwili baadaye mpenzi wake wa kiume, Ko San Pe, alikufa kwa madawa ya kulevya pia Jumatano ya tarehe 21/07/1982 akiwa na miaka 25. Alizaliwa Jumanne ya tarehe 29/01/1957. Ma Thida Wai Aung ni wa mwisho kuzaliwa. Ana miaka 34. Alizaliwa Jumatano ya tarehe 23/07/1958. Anakaa Rangoon na mume wake wa miaka sita na watoto wawili, wa kike na wa kiume. Saw Saya (Mkurugenzi wa Sekretarieti ya Kanda ya Asia-Australia ya Tume ya Dunia ya Kudhibiti Madawa ya Kulevya, kutoka katika kabila la Karen) ndiye aliyempa taarifa U Nanda za kikao cha dharura cha Tume ya Dunia. Ana miaka 54. Alizaliwa Jumanne ya tarehe 01/03/1938.”

“Ndoto za wachawi ni tofauti kidogo na ndoto takatifu. Wachawi wanapokuwa hawahitaji kusafiri kutoka sehemu moja kwenda nyingine, lakini wana hamu ya kuona wenzao wanafanya nini au wanasema nini, huwa wanalala ubavu mmoja upande wa kushoto kwa jina la mungu wao na la mashetani wote. Kisha wanatoa mvuke wa bluu midomoni mwao. Kupitia mvuke huo, kwa nguvu za Shetani na kwa ruhusa ya Mwenyezi Mungu, wataona na watasikia kila kinachofanyika upande wa pili. Kile wanachotaka kukiona na kukisikia hujifunua katika ufahamu wao kama taswira au maono, kutoka katika akili isiyotambua, ya watu wakifanya au wakisema kitu. Kama wanataka kujua siri za watu wengine, hata wale ambao si wachawi, watazijua kupitia ndoto hizo; kwa sababu ya makubaliano ya wazi, si ya siri, waliyoingia na Shetani. Makubaliano hayo si ya lelemama; yaani yale ambayo hufanywa kwa kutoa kafara ya mnyama, au kufuru ya aina yoyote ile kwa Mwenyezi Mungu, au kwa kuabudu dini za kichawi. Lakini ni kwa sadaka halisi ya wao wenyewe ya mwili na roho kwa Shetani na kwa kufuru ya kuikana kabisa, imani ya Mwenyezi Mungu. Lakini hiyo ni kwa wale wanaotumia uchawi wa kishetani. Wale wanaotumia uchawi wa asili, kama vile kutumia risasi kumroga mtu kwa sababu risasi mungu wake ni sayari ya Zohali, au wale walioingia mkataba wa siri na Shetani, hawana uwezo wa kuota hivyo. Hivyo, si kila mchawi anaweza kuota ndoto za namna hiyo, ni kwa wale tu walioingia mkataba wa wazi na Shetani.”

“Tunazaliwa, kuteseka na kufa kwa sababu ya dhambi ya asili ya wazazi wetu wa kwanza (Adamu na Hawa). Kama Hawa asingekubali kudanganywa na Shetani, tungezaliwa bila uchungu, tungeishi bila kuteseka na tusingekufa milele. Lakini haya ndiyo mawazo yangu: Mungu Ahusiki na dhambi, Ahusiki na mwili, Anahusika na roho. Hivyo, mtu anapofariki mwili unabaki duniani lakini roho inarudi kwa Mungu; kwani Yeye ndiye aliyeitengeneza na kuiweka katika moyo wa mtu. Mimi na wewe ni viumbe vyenye thamani kubwa sana mbele za Mwenyezi Mungu; mapenzi Yake kwetu hayana masharti yoyote. Hainiingii akilini (hata kidogo) kumtesa mtu unayempenda kiasi hicho milele, wakati uwezo wa kumwokoa unao.”

“Kula sana kunaweza kusababisha virutubisho kuzidi mwilini zaidi ya kiwango kinachohitajika na mwili, ambavyo baadaye vinaweza kusababisha madhara ya papo kwa hapo kama tumbo kuuma au tumbo kujaa gesi! Baada ya muda mrefu wingi wa virutubisho hivi unaweza kuingiliana na ufyonzaji wa madini kama fosforasi, kalisi, magnesi, chuma, na zinki, hali inayoweza kusababisha upungufu mkubwa wa virutubisho, unaoweza kusababisha kifo.”

“Kasoro za Uzi zilizofanya zisitumiwe tena na kikosi cha usalama cha rais wa Marekani ni kutokuwa na shabaha imara katika umbali mfupi (hutawanya risasi na huleta madhara makubwa katika umbali mfupi hivyo kuweza kudhuru hata watu wasiokuwa na hatia) na kutokuwa na uwezo wa kutoboa kinga ya risasi dhidi ya magaidi wanaotumia mavazi ya kuzuia risasi, wanaotishia usalama wa rais wa Marekani. Gaidi mwenye mavazi ya kuzuia risasi aliweza kumdhuru rais kwa maana ya USSS kushindwa kumdhibiti. Badala yake, sasa USSS wanatumia FNP90 – zenye uwezo wa kutoboa kinga ya risasi, na ambazo hazileti madhara makubwa katika umbali mfupi na katika umbali mrefu. Bunduki hizi, zenye uwezo wa kubeba risasi 100 katika chemba zake mbili za Kampuni ya Beta ('Century Magazines'), zilitumiwa na magaidi wa Kolonia Santita dhidi ya Vijana wa Tume na dhidi ya polisi wa Tume ya Dunia ya Kudhibiti Madawa ya Kulevya.”

“Kujua nini kitatokea kesho, au kesho kutwa, au kujua jinsi usaili wako wa kazi utakavyokuwa, au ni maswali gani utakayoulizwa kwenye mtihani kwa mfano, kutarahisisha sana maisha yetu. 'Madirisha' madogo katika kipindi cha saa za usoni hufunguka mara kwa mara katika maisha yetu, kimiujiza na bila kutegemea. Hudokeza kidogo jinsi tukio fulani, au hali fulani, au kitu fulani kitakavyotokea katika kipindi cha wakati ujao bila sisi wenyewe kujua. Hali hii hujulikana kama jakamoyo. Jakamoyo ni sanaa ya kubashiri vitu visivyojulikana. Kazi yake ni kutuhadharisha na kutusaidia! Kujua mapema hatari iliyoko mbele yako inamaanisha kuwa na uwezo wa kujilinda kutokana na hatari hiyo, na kuwa na uwezo wa kuepuka mitego. Jakamoyo huweza kumtokea mtu katika hali ya 'maono', au 'mwako wa mwanga' (yaani kufumba na kufumbua). Mara nyingi huonekana kama ndoto. Hutokea wakati mtu amelala usingizi. Ikitokea wakati mtu yuko macho, wakati mwingine huendana na misisimko ya mwili kabla ya mwako, ikiwa na maana ya kumfanya mtu awe makini na kitu chochote kinachotarajia kutokea. Ndiyo maana baadhi ya watu utakuta wakisema wanaumwa tumbo, kifua au kichwa cha ghafla katika kipindi ambacho taswira ya tukio fulani inakuwa ikitokea akilini mwao, ikiwaambia waende mahali fulani bila kukosa kwa mfano, na kadhalika. Hakuna mtu anaweza kufanya jakamoyo imtokee. Hutokea yenyewe muda wowote kuleta ujumbe, kuhusiana na matukio ya wakati ujao. Kamwe usipuuze wito wa moyo wako.”

“Manabii wa uongo, na wafuasi wao, hawautaki ukweli. Kazi yao ni kutulazimisha tumwabudu Mpinga Kristo, badala ya Yesu Kristo, bila sisi wenyewe kujua. Wana mamlaka yote ya Mpinga Kristo kwa sababu, kama Mpinga Kristo, wanaongozwa na Shetani. Walimu hawa wa uongo wanaopenda kuvalia misurupwenye ya kisawasawa, na wanaoongea utafikiri wamemeza Biblia na kuitapika kwenye mikrofoni, lengo lao ni kutupeleka kwenye ufalme wa Shetani. Hatuna budi kuitangaza injili ya kweli ya Yesu Kristo, kwa imani ya kweli, kupata urithi usiohongeka wa ufalme wa Mungu.”

“Wafuasi wa Yesu Kristo watapata taabu kubwa ambayo haijawahi kutokea. Yeyote atakayempinga Mpinga Kristo, yeyote atakayepinga utawala wa Mpinga Kristo, atakiona cha mtema kuni. Watu wengi watauwawa kwa sababu ya ufuasi wao kwa Masihi. Wale watakaokuwa na talanta ya kuhubiri watauwawa kinyama, hadharani, ili liwe fundisho kwa wafuasi wengine wa Yesu Kristo. Miongoni mwa wale watakaokuwa wanahubiri injili ya kweli ya ufalme wa Mungu bila woga wa aina yoyote ile, atakuwemo Eliya na Enock. Eliya na Enock Mungu aliwachukua bila kuonja mauti, kama akiba, kwa sababu ya kipindi hicho cha Taabu ya Yakobo. Eliya na Enock wataibuka ghafla jijini Yerusalemu na kuanza kuhubiri injili ya kumpinga Mpinga Kristo. Kwa vile hawataogopa chochote, wala hawatamwogopa yeyote, serikali ya Israeli itawakamata na kuwatesa lakini hawatanyamaza.”

“Mpinga Kristo atakapoona imeshindikana kuwanyamazisha, Eliya na Enock, huku akitamba kwamba yeye ndiye Yesu Kristo ambaye kila mtu ndiye aliyekuwa akimsubiri arudi kwa mara ya pili; na kwamba yeye anatoka katika ukoo wa mfalme Daudi, ili watu waamini kama kweli yeye ndiye Yesu Kristo, ataamuru Eliya na Enock wauwawe hadharani kama wahubiri wengine. Eliya na Enock watakapouwawa, Mungu atawafufua na watarudi mbinguni wakiwa wameonja mauti kama binadamu mwingine yeyote yule. Hapo mlango wa rehema utakuwa umefungwa. Muda wowote kuanzia hapo Yesu atarudi, kwa mara ya pili, na kwa ajili ya ufufuo wa kwanza.”

“Damu ya Mwanakondoo ina nguvu kuliko maombi. Mungu hauwi, Anamtumia Shetani kama wakala wake wa kutoa adhabu kwa binadamu. Ukifunikwa na damu ya Mwanakondoo Shetani, ambaye ni wakala, hatakuona. Lakini Mungu atakuona. Bila kafara ya damu hakuna msamaha wa dhambi. Bila kafara ya damu hakuna mafanikio.”

“Ndege ya Kolonia Santita, Grumman Gulfstream III, tofauti na ndege alizokuwa akitumia Panthera Tigrisi na makompade wake wa karibu, ilifanya kazi kubwa katika mgogoro wa Kolonia Santita na Tume ya Dunia. Dar es Salaam Grumman ilipomchukua kachero Giovanna Garcia wa Kolonia Santita, baada ya ndege hiyo kutumwa na makamanda wa Kolonia Santita wa Copenhagen, ilimpeleka Paris nchini Ufaransa kuhudhuria kikao cha siri cha CS-Paris. Katika kikao hicho yeye na wenzake wakapanga mauaji ya Kamanda John Murphy Ambilikile, kwa kusuka mbinu kamambe za kumteketeza, kabla ndege yake haijafika Copenhagen. Giovanna akashiriki pia kupeleka taarifa za Murphy duniani kote katika matawi yote ya Kolonia Santita, Urusi ikiwemo, ambapo Murphy alitekwa nyara na CS-Moscow. Baada ya 'mauaji' ya Murphy, Grumman iliwapeleka baadhi ya maadui waliohusika na mauaji hayo Mexico City katika makao makuu ya Kolonia Santita; kisha ikarudi Copenhagen kumchukua kiongozi wa CS-Copenhagen, Regner Steiner Valkendorff, na Kachero wa Kolonia Santita Delfina Moore.”

“To be able to influence Tanzanian literature and African literature, and sell our books in Tanzania as well as in our continent, we need to be committed to what we do. And what we do is writing. Write as much as you can. Read as much as you can. Use the library and the internet carefully for research and talk to people, about things that matter. To make a living from writing, and make people read again in Tanzania and Africa; we must write very well, very good stories.”

“John Murphy alifika Moscow tarehe 1/11/1992 saa 11 alfajiri akitokea Cairo, Misri. Wakati huo Moscow kulikuwa na baridi sana. Teksi yake ilipofika Teatralny Proezd, upande wa kusini wa Hoteli ya Metropol – karibu na mojawapo ya minara ya mwanzo ya Kitay-gorod, kitovu kikuu cha biashara cha Moscow ya kale – kwa matatizo ya injini; magaidi wanne, waliokuwa wakimfuatilia kwa gari aina ya Bentley Continental S nyeusi – iliyokuwa na namba za kitemi za B 001 BB 77 RUS mali ya Kiongozi wa CS-Moscow Dmitri Olegushka – toka Uwanja wa Ndege wa Sheremetyevo II wa kaskazini-magharibi mwa jiji la Moscow, waliendelea mbele na kusimama mkabala na Jumba la Maonyesho ya Tamthilia la Bolshoy; kisha wawili kati yao wakashuka na kuingia ndani ya kioski, wawili wakibaki ndani ya gari kuhakikisha John Murphy hawapotei. Magaidi hao wa CS-Moscow, Tawi la Kolonia Santita la Urusi na nchi zote za Ulaya ya Mashariki na baadhi ya nchi za Ulaya ya Kusini, walijua Murphy alishawahisi.”

“Ndani ya kibweta cha risasi kuna vitu vitano vyenye uwezo wa kulipuka kama vile risasi, kasha, baruti, kitako na fataki. Risasi hutumika kama kombora – kitu kinachoweza kusafiri hewani na kulipuka baada au kabla ya kugonga shabaha – wakati kasha kazi yake ni kuhifadhi vitu vyote vya kibweta kwa pamoja kusudi visisambae. Baruti inayotoa au isiyotoa moshi ni poda yenye uwezo wa kulipuka ambayo ndani yake kuna mkaa, salfa na shura; ambayo husukuma kombora mbele kwa nguvu kubwa baada ya fataki kulipuka kupitia katika kitako cha kibweta. Kitako cha kibweta hutumika kama kiziduo cha risasi kutoka katika chemba ya silaha, wakati fataki kazi yake ni kuwashia baruti.”

“Ford Bronco ilikuwa sehemu ya upelelezi wa polisi wa Tume ya Dunia, na ilipigwa mnada baada ya upelelezi na kesi kumalizika. Kiasi kikubwa cha pesa iliyopatikana kilikwenda kwa WPD – Idara ya Polisi ya Tume ya Dunia – ili iendelee kuimarisha huduma ya kukomesha biashara haramu ya madawa ya kulevya duniani.”