Quotessence
Home / Authors / Enock Maregesi

Enock Maregesi Quotes

Author

Filter quotes by topic

Famous Enock Maregesi Quotes

“John Murphy amefariki dunia. Ndege aliyotoka nayo hapa, Dar es Salaam, ndiyo aliyotoka nayo Paris na ndiyo hiyo iliyoanguka katika mazingira ya kutatanisha. Watu waliobahatika kuing’amua fununu hii ni wachache na ambao hivi sasa hawajiwezi kabisa, akiwemo kamishna wetu wa kanda Profesa Mafuru. Profesa yuko mahututi. Ameshtuka baada ya kusikia taarifa hizo katika redio ya hapa. Yuko chini ya uangalizi mkali wa madaktari. Mungu aiweke roho ya John Murphy, shujaa wa karne, mahali pema peponi. Bwana alitoa na Bwana ametwaa. Jina la Bwana lihimidiwe.”

“Kuna aina tatu za upendo hapa ulimwenguni. Kuna upendo wa ‘agape’, upendo kati ya Mungu na binadamu na kati ya binadamu na binadamu mwenzake lakini hao binadamu shuruti wawe marafiki wa msalaba wa Yesu Kristo. Aidha kuna upendo wa ‘phileo’, upendo kati ya mtu na mtu au kati ya mtu na kitu au kati ya mtu na jambo; na kuna upendo wa ‘philadelphia’, upendo wa wanachama wa mashirika ya siri ambapo mtu humpenda mwenzake kama ndugu yake wakati si ndugu yake. Heri upendo wa ‘agape’ kuliko upendo ajmaina.”

“Mungu si wa kudhihakiwa (Wagalatia 6:7)! Katika maneno kadhaa ya Biblia, anasema bila masihara kabisa kwamba yeye ni Mungu mwenye wivu (Kutoka 34:14; Kumbukumbu la Torati 6:4-15) – Yeye si wa kuabudiwa kama mungu mwingine yeyote yule (Kumbukumbu la Torati 12:3-4, 30-31). Alipowaagiza watu wake wateule Israeli kwa njia ya ibada yake, aliwaonya wasiongeze juu ya kile alichokuwa amewapa wala wasipunguze chochote (Kumbukumbu la Torati 4:2; 12:32; angalia pia Ufunuo 22:18-19). Kwa mfano, angalia hasira yake kuu wakati wana wa Israeli walipojaribu kumwabudu kupitia Ndama wa Dhahabu (Kutoka 32:1-9). Walitangaza kuwa ilikuwa sikukuu ya Bwana (mstali wa 5), lakini Mungu hakulithamini hilo! Alikuwa na hasira kali juu ya ibada ya sanamu za watu, kiasi kwamba alifikiria kuangamiza taifa zima na kuanza upya na familia ya Musa. Mungu huyohuyo – Yahweh, Bwana wa Agano la Kale – akawa Yesu Kristo! Je, Mwokozi wetu atakubali kuabudiwa kwa namna yoyote ambayo misingi yake imejikita kwenye uongo? Hapana! Na hili kwa vyovyote vile limezingatia mila na desturi zisizo za kibiblia (labda tunaweza kusema za “kipagani”) ambazo zimechukua nafasi ya maadhimisho ya kafara na ushindi wa kishindo wa Yesu Kristo.”

“Boresha maisha ya watu kwa kadiri utakavyoweza. Ukisaidia mtu 1 watahurumiwa watu 10. Ukisaidia watu 10 watahurumiwa watu 100. Ukisaidia watu 100 watahurumiwa watu 1000. Kila mmoja wetu akitambua wajibu wake katika jamii, Mungu atatuhurumia sisi wote. Maisha ya mtu mmoja yakiboreka, mmoja huyo ataboresha na ya wengine wengi. Hivyo, endelea kuogelea lakini usisahau kurudi nyuma katika jamii.”

“Kiungo chochote kikikuuma ghafla na kuacha au kikiendelea kukuuma kwa muda fulani halafu kikaacha, halafu huna sababu ya kwa nini kinakuuma, angalia unawaza nini wakati kiungo hicho kinakuuma. Kisha lifanyie kazi wazo hilo kwa maombi hata ya sekunde tano! Funika tatizo hilo, hata kama hulijui, kwa damu ya Yesu!”

“Mungu humwambia mtu kitu cha kusema na mtu huwambia wenzake kile ambacho Mungu amemwambia aseme. Lakini utajuaje kama Mungu amekuchagua wewe kusema au kufanya kitu? Mungu atakwambia kupitia Roho Mtakatifu, na utajisikia msukumo mkubwa wa kusema au kufanya kile ambacho Mungu anataka useme au ufanye. Unabii unaweza kumtokea mtu yoyote, mahali popote, anayejua jinsi ya kuwasiliana na Mungu.”

“People speak broken Swahili on purpose. Business people for instance will speak Sheng – a mixture of Swahili and English – because that’s what people want to hear. And what is the government doing? They speak broken Swahili most of the time. Swahili is getting lost and I am really sorry for the future generations.”

“Mbegu ni neno la Mungu na kudondoka kwake kwenye ardhi si mwisho wa maisha yake. Mambo kadha wa kadha yanaweza kutokea yanayoweza kuathiri ukuaji wa mbegu husika. Nyingine zinaweza kuanguka karibu na njia ndege wakaja wakazila, nyingine zinaweza kuanguka penye miamba pasipokuwa na udongo mwingi wa kutosha, nyingine zinaweza kujifukia ndani kabisa ya ardhi na kupotelea huko kwa miaka mingi, mvua inaweza kunyesha na kuhamisha baadhi ya mbegu kwa kuzisomba na maji. Lakini kwa kuwa maisha yamo ndani ya mbegu, jambo fulani litatokea.”

“Akili yangu itakaponipeleka kwa mgonjwa hospitalini halafu sekunde hiyohiyo jicho langu likacheza au kiungo changu chochote cha mwili kikauma na kuacha ghafla ‘bila’ sababu yoyote, najua kile ninachokifikiria kuhusu mgonjwa huyo ama kitatokea au hakitatokea. Nikifikiria amepona, halafu ghafla kichwa kikaniuma na kuacha, kitakuwa kinyume chake. Yaani, hatapona. Nikifikiria amekufa, halafu ghafla kichwa au kiungo kingine chochote kikaniuma na kuacha, kitakuwa kinyume chake pia. Yaani, hatakufa. Hivyo, nikifikiria amepona, nikifikiria amekufa, na kichwa kikaniuma na kuacha, sekunde hiyohiyo natakiwa kumwombea mgonjwa huyo. Kama ni kupona, apone kama Mungu alivyokusudia; na kama ni kufa, afe kama Mungu alivyokusudia. Si kama Shetani alivyokusudia.”

“Kazi yenu kwetu ni kutusaidia, na kazi yetu kwenu ni kuwasaidia pia; kwani kila mwananchi anao wajibu wa kuisaidia serikali yake. BASATA, katika jina la Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, endeleeni kuhamasisha na kuhakikisha wasanii wote nchini wanajisajili; kwa kuendelea kutoa tuzo mbalimbali za sanaa na jitihada nyingine, na kwa kuendelea kufuatilia kuhakikisha kuwa kila msanii anajisajili na kupata kibali.”

“Unapofikia hatua ya kuwa na kila kitu katika maisha, unapokuwa umefanya kila kitu ulichotamani kufanya katika maisha, unakuwa na bahari nzima ndani ya tone ambalo ni wewe. Unaridhika. Wewe si tone tena ndani ya bahari, wewe ni bahari ndani ya tone. Kinachobaki baada ya hapo ni kusaidia jamii iliyosaidia kukulea ulipokuwa mdogo, kuacha alama katika dunia kabla na baada ya wewe kuondoka, bila kujali watu watasema nini juu ya maisha yako.”

“Mafundisho mengine ambayo si ya kweli ya Ukristo ambayo hutokana na utambuzi wao wa matukio haya ni ‘Siku ya Bwana’. Makanisa ya Kikatoliki na Kiprotestanti kote duniani yanaonekana kuwa na nia njema lakini huwadanganya watu kuamini kuwa Kristo alibadili siku ya kupumzika kutoka Sabato kwenda Jumapili. Angewezaje kufanya hivyo? Angeweza kufanya hivyo kwa ufufuo wake!”

“Umoja ni nguvu, utengano ni udhaifu. Umoja una sisi (ubinadamu) si mimi (ubinafsi). Watu wanne wakifanya kazi kwa ushirikiano watakuwa na nguvu ya watu watano! Watakuwa na nguvu ya ziada kufanikisha malengo kama vile kuwa na uwezo wa kusaidia jamii kama timu moja au kama mtu binafsi, kujenga shule ya kijiji, kutengeneza ziada katika masuala ya uchumi wa nyumbani au wa kampuni au wa nchi au wa mtu binafsi, ushindi katika jambo lolote lile, na kadhalika. Mimi ni ubinafsi. Sisi ni ubinadamu. Ubinafsi ni uvivu. Ubinadamu ni uchapakazi.”

“Muda haututoshi. Tunajua mizigo hiyo ni ya nani. Tunajua nani aliua maafisa wetu wa polisi na maafisa wa polisi wa Meksiko na Marekani na wapita njia na kwa nini alifanya hivyo. Hatujui kwa hakika imefichwa wapi. Kuwakamata wahusika ni kazi nzito, ndugu wajumbe. Inahitaji ujasiri wa kupindukia … na kujitoa mhanga. Kuzuia mizigo ya CS-14, na kumkamata kiongozi wake, lazima tupigane kufa na kupona. Kwa siku kumi shehena zikamatwe na kuharibiwa, na viongozi wa Santita (wote) wakamatwe na kuwekwa chini ya sheria.”