Quotessence
Home / Authors / Enock Maregesi

Enock Maregesi Quotes

Author

Filter quotes by topic

Famous Enock Maregesi Quotes

“Biblia pamoja na historia vinatwambia kuwa mitume kumi na wawili wa Yesu Kristo waliamua kufa kinyama kama mfalme wao alivyokufa, kwa sababu walikataa kukana imani yao juu ya Yesu Kristo. Mathayo alikufa kwa ajili ya Ukristo nchini Ethiopia kwa jeraha lililotokana na kisu kikali, Marko akavutwa na farasi katika mitaa ya Alexandria nchini Misri mpaka akafa, kwa sababu alikataa kukana jina la Yesu Kristo. Luka alinyongwa nchini Ugiriki kwa sababu ya kuhubiri Injili ya Yesu Kristo katika nchi ambapo watu hawakumtambua Yesu. Yohana alichemshwa katika pipa la mafuta ya moto katika kipindi cha mateso makubwa ya Wakristo nchini Roma, lakini kimiujiza akaponea chupuchupu, kabla ya kufungwa katika gereza la kisiwa cha Patmo (Ugiriki) ambapo ndipo alipoandika kitabu cha Ufunuo. Mtume Yohana baadaye aliachiwa huru na kurudi Uturuki, ambapo alimtumikia Bwana kama Askofu wa Edessa. Alikufa kwa uzee, akiwa mtume pekee aliyekufa kwa amani. Petro alisulubiwa kichwa chini miguu juu katika msalaba wa umbo la X kulingana na desturi za kikanisa za kipindi hicho, kwa sababu aliwaambia maadui zake ya kuwa alijisikia vibaya kufa kama alivyokufa mfalme wake Yesu Kristo. Yakobo ndugu yake na Yesu (Yakobo Mkubwa), kiongozi wa kanisa mjini Yerusalemu, alirushwa kutoka juu ya mnara wa kusini-mashariki wa hekalu aliloliongoza la Hekalu Takatifu (zaidi ya futi mia moja kwenda chini) na baadaye kupigwa kwa virungu mpaka akafa, alipokataa kukana imani yake juu ya Yesu Kristo. Yakobo mwana wa Zebedayo (Yakobo Mdogo) alikuwa mvuvi kabla Yesu Kristo hajamwita kuwa mchungaji wa Injili yake. Kama kiongozi wa kanisa hatimaye, Yakobo aliuwawa kwa kukatwa kichwa mjini Yerusalemu. Afisa wa Kirumi aliyemlinda Yakobo alishangaa sana jinsi Yakobo alivyolinda imani yake siku kesi yake iliposomwa. Baadaye afisa huyo alimsogelea Yakobo katika eneo la mauti. Nafsi yake ilipomsuta, alijitoa hatiani mbele ya hakimu kwa kumkubali Yesu Kristo kama kiongozi wa maisha yake; halafu akapiga magoti pembeni kwa Yakobo, ili na yeye akatwe kichwa kama mfuasi wa Yesu Kristo. Bartholomayo, ambaye pia alijulikana kama Nathanali, alikuwa mmisionari huko Asia. Alimshuhudia Yesu mfalme wa wafalme katika Uturuki ya leo. Bartholomayo aliteswa kwa sababu ya mahubiri yake huko Armenia, ambako inasemekana aliuwawa kwa kuchapwa bakora mbele ya halaiki ya watu iliyomdhihaki. Andrea alisulubiwa katika msalaba wa X huko Patras nchini Ugiriki. Baada ya kuchapwa bakora kinyama na walinzi saba, alifungwa mwili mzima kwenye msalaba ili ateseke zaidi. Wafuasi wake waliokuwepo katika eneo la tukio waliripoti ya kuwa, alipokuwa akipelekwa msalabani, Andrea aliusalimia msalaba huo kwa maneno yafuatayo: "Nimekuwa nikitamani sana na nimekuwa nikiitegemea sana saa hii ya furaha. Msalaba uliwekwa wakfu na Mwenyezi Mungu baada ya mwili wa Yesu Kristo kuning’inizwa juu yake." Aliendelea kuwahubiria maadui zake kwa siku mbili zaidi, akiwa msalabani, mpaka akaishiwa na nguvu na kuaga dunia. Tomaso alichomwa mkuki nchini India katika mojawapo ya safari zake za kimisionari akiwa na lengo la kuanzisha kanisa la Yesu Kristo katika bara la India. Mathiya alichaguliwa na mitume kuchukua nafasi ya Yuda Iskarioti, baada ya kifo cha Yuda katika dimbwi la damu nchini India. Taarifa kuhusiana na maisha na kifo cha Mathiya zinachanganya na hazijulikani sawasawa. Lakini ipo imani kwamba Mathiya alipigwa mawe na Wayahudi huko Yerusalemu, kisha akauwawa kwa kukatwa kichwa. Yuda Tadei, ndugu yake na Yesu, aliuwawa kwa mishale alipokataa kukana imani yake juu ya Yesu Kristo. Mitume walikuwa na imani kubwa kwa sababu walishuhudia ufufuo wa Yesu Kristo, na miujiza mingine. Biblia ni kiwanda cha imani. Tunapaswa kuiamini Biblia kama mitume walivyomwamini Yesu Kristo, kwa sababu Biblia iliandikwa na mitume.”

“Mitume kumi na wawili wa Yesu Kristo waliamua kufa kinyama kulinda heshima ya mfalme wao Yesu Kristo, kama Biblia na historia vinavyosema. Kwa nini watu (wengine) wa kizazi hiki wanasema hakuna Mungu na kwa sababu hiyo hawamwamini Yesu? Je, uko tayari kufa kwa ajili ya mtu aliyekufa kwa ajili yako? Kwa ajili ya mtu ambaye mitume walikuwa tayari kufa kwa ajili yake? Je, wewe una akili zaidi kuliko mitume? Yesu aliamua kufa ili wewe uishi, lakini bado unakuwa mbishi. Badilika.”

“Tupo watu takriban bilioni saba katika dunia hii. Kila mtu ni wa kipekee. Mathalani, wewe ni tofauti na baba yako au mama yako au mtu mwingine yoyote yule. Kila mtu aliumbwa kivyake na Mwenyezi Mungu. Kila mtu ana nafasi ya kwake mwenyewe aliyopangiwa na Mungu hapa duniani. Haijalishi wewe ni mwanamke au mwanamume, mweupe au mweusi, mfupi au mrefu, mzuri au mbaya, una nafasi katika nchi na dunia hii. Unachotakiwa kufanya ni kuamka, kufumbua macho na kuujua ukweli. Tafuta maarifa katika Biblia kama wewe ni Mkristo. Tafuta maarifa katika Kurani kama wewe ni Mwislamu. Tafuta maarifa katika Yoga kama wewe haumwamini Mungu. Ukishaamka na kuujua ukweli, ukishapata nafasi katika nchi yako, kuwa kiongozi na mkarimu kwa wenzako. Jifunze kutoka kwa wengine ndani na nje ya tasnia yako. Usiwe mchoyo wa maarifa. Kuwa mwadilifu. Ukifanya hivyo utafanikiwa zaidi, utaipa heshima tasnia yako, na utaacha alama katika dunia baada ya kuondoka. Kuacha alama katika dunia si lazima upate nafasi katika dunia. Kuacha alama katika dunia acha alama katika nchi yako.”

“Mungu alilibariki taifa la Israeli katika misingi ya kidini na si katika misingi ya kisiasa au misingi ya kihistoria; na asili ya dini ya Kikristo ni kutoka katika taifa hilo ambalo Biblia imelitaja kama taifa teule la Mwenyezi Mungu. Mgogoro wa Israeli na Palestina ulianzishwa na Israeli mwenyewe. Yakobo alipokea baraka iliyokuwa si ya kwake kwa kutumia hila ya Rebeka. Baraka ya Yakobo ilikuwa ya Esau.”

“Mungu hutumia watu 'wajinga' na 'wapumbavu' kufanya mambo makubwa katika maisha yao na ya watu wengine. Katika Biblia, Musa aliitwa mjinga alipokiuka amri ya Farao ya kuendelea kuwafanya watumwa wana wa Israeli nchini Misri; Nuhu aliitwa mpumbavu alipohubiri kwa miaka mia kuhusu gharika, katika kipindi ambacho watu hawakujua mvua ni nini; Daudi aliitwa mjinga alipojitolea kupambana na Goliati bonge la mtu, shujaa wa Gathi; Yusufu aliitwa mjinga alipokataa kulala na mke wa bosi wake, baada ya kuwa ameuzwa na nduguze kama mtumwa nchini Misri; Abrahamu aliitwa mjinga alipoamua kuhama nchi aliyoipenda na kwenda katika nchi ya ahadi, eti kwa sababu Mungu alimwambia kufanya hivyo; Yesu aliitwa mjinga mpaka akasulubiwa aliposema yeye ni Mfalme na Mwana wa Mungu. LAKINI, Musa alitenganisha Bahari ya Shamu na kuwapeleka Waisraeli katika nchi ya ahadi, ambako aliwakomboa kutoka utumwani. Nuhu aliokoa dunia. Daudi alimshinda Goliati. Yusufu aliokoa familia yake kutokana na njaa. Abrahamu alikuwa baba wa imani. Yesu aliyashinda mauti. Wakati mwingine tunatakiwa kufanya mambo makubwa kulingana na jinsi Roho Mtakatifu anavyotutuma, bila kujali watu au dunia itasemaje.”

“Ukipata matatizo kumbuka kwamba Yesu alipata matatizo pia, na kutokana na matatizo hayo mimi na wewe tulipata uhuru. Soma Biblia. Soma nyimbo katika kitabu cha Zaburi zinazomsifu Mungu katika kipindi cha matatizo. Funga na kuomba ukiamini kwamba mapenzi ya Mungu kwetu ni huru, yasiyokuwa na masharti yoyote. Toa msamaha kwa waliokukosea. Ni kitu cha muhimu kujilimbikizia imani katika kipindi cha amani, ili matatizo yakitokea usiweze kuyumba.”

“Majina ya vitabu yanapaswa kuchaguliwa kwa mantiki na kwa makini ya hali ya juu mno, kwa sababu ni miongoni mwa vitu vya kwanza watu wanavyoviona na kuvisoma. Watu wakivutiwa na jina la kitabu, au mwandishi; kitu cha pili watakachovutiwa kuangalia ni dibaji, kusudi wasome muhtasari wa kitabu kizima. Kwa hiyo dibaji inapaswa iandikwe kwa mantiki na kwa makini ileile iliyotumika katika kuchagua jina la kitabu. Lengo la jina la kitabu na dibaji ni kuishawishi hadhira kusoma kitabu na kukifurahia.”

“Palestina ni nchi ya Waisraeli waliyopewa na Mungu wa Yakobo. Hata hivyo, hawakutimiza masharti. Mungu aliwaagiza kuua kila mtu katika nchi ya Kaanani na miji yake yote. Waisraeli, wakiongozwa na Yoshua, waliua watu wengi katika nchi ya Kaanani. Hawakuua kila mtu katika miji ya Ashdodi, Gathi na Ukanda wa Gaza kama walivyoagizwa. Mungu alimwambia Ibrahimu kuwa angempa yeye na uzao wake nchi ya Kaanani kuwa milki yao ya milele, na kuwa Yeye ndiye angekuwa Mungu wao daima. Vita ya Israeli na Palestina itamalizwa na Mungu. Itamalizwa na hekima.”

“Kusudi mimba itungwe lazima kuwepo na kromosomu X na kromosomu Y. Kromosomu ni nyuzinyuzi katika kiini cha seli zenye jeni au DNA, ambazo hubeba taarifa kuhusu sifa za kimaumbile zinazorithishwa kwa kiumbe hai kutoka kwa mama na baba wa kiumbe hicho. Kwa upande wa Yesu Kristo, katika hali ya kawaida, kromosomu X ilitoka kwa Maria Magdalena na kromosomu Y ilitoka kwa malaika Gabrieli. Yesu alikuwa Myahudi lakini Kristo ni Mungu. Yesu Kristo alikuwa binadamu kama sisi, lakini alikuwa na utukufu na alikuwa na damu ya Mungu iliyotakasika. Damu kama hiyo ndiyo inayotiririka katika miili ya kila mmojawetu ijapokuwa ni damu ya Adamu, ambayo bado haijatakaswa. Damu ya Yesu si kitu kidogo. Ilipomwagika msalabani ilifunika dunia nzima. Ndiyo maana tukasamehewa. Bila damu hiyo, bila utukufu huo wa Mungu, hakuna binadamu atakayeokolewa, hakuna pepo atakayeondolewa.”

“Kuna mambo yanatokea hapa ulimwenguni ambayo yanafanya nikiri uwepo wa Mungu kwa asilimia kubwa. Wanasayansi wanasema ulimwengu ulianzishwa na mlipuko wa ‘Big Bang’, uliotokea takribani miaka bilioni 14 iliyopita, kutoka katika kitu kidogo zaidi kuliko ncha ya sindano, lakini hawatuambii nini kilisababisha mlipuko huo utokee au hicho kitu kidogo kuliko ncha ya sindano kilitoka au kilikuwa wapi. Wanaendelea kusema kuwa baada ya ‘Big Bang’ kutakuwepo na ‘Big Crunch’, ambapo ulimwengu utarudia hali yake ya awali ya udogo kuliko ncha ya sindano, na kila kitu kinachoonekana leo ulimwenguni hakitaonekana tena. Hapo sasa ndipo utata unapokuja. Mlipuko wa ‘Big Bang’ ulipotokea ulimwengu ulilipuka na kusambaa pande zote nne za ulimwengu kwa mwendokasi wa zaidi ya kilometa milioni 2 kwa saa, mpaka hivi leo unavyoonekana na bado unaendelea kusambaa. Kutokana na dhana ya ‘Big Crunch’, wanasayansi wanaamini ulimwengu utapanuka ila baadaye utapungua mwendo na utarudi mwanzo kabisa mahali ulipolipukia. Lakini mwaka 1995 wanasayansi hao hao waligundua kitu. Ulimwengu – badala ya kupungua mwendo wa kupanuka kama wanasayansi walivyokuwa wakitabiri – sasa unaongeza mwendo, tena kwa mwendokasi ambao haujawahi kutokea. Hiki ni nini kinachosababisha ulimwengu uongeze mwendokasi kiasi hicho badala ya kuupunguza? Hicho ni nini ambacho ulimwengu unapanukia? Wanasayansi hawana jibu. Wanasingizia kitu kinaitwa ‘dark matter’, maada ambayo haijawahi kuonekana, kwamba ndicho kinachosababisha ulimwengu uongeze mwendokasi kwa kiwango hicho ambacho hakijawahi kutokea; na hicho ambacho ulimwengu unapanukia wanahisi ulimwengu wetu unapanukia katika ulimwengu mwingine, kwa mujibu wa dhana nyingine kabisa iitwayo ‘multiverse’ au ‘meta-universe’. Kuna kitu kinaitwa ‘Higgs boson’ – chembe ndogo inayosemekana kuhusika na uzito (‘mass’) wa chembe ndogo 16 zilizomo ndani ya atomu, kasoro chembe ya mwanga, iliyopotea mara tu baada ya mlipuko wa ulimwengu wa ‘Big Bang’ miaka bilioni 13.7 iliyopita katika kipindi kilichoitwa ‘epoch’ – ambayo ilianza kutafutwa katika maabara za CERN, Uswisi, toka mwaka 1964, maabara ambazo kazi yake kubwa ni kutengeneza mazingira ya mwanzo kabisa ya mlipuko wa ‘Big Bang’, kusudi wanasayansi waone kama wanaweza kubahatisha kuiona na kuidhibiti hiyo bosoni. Bosoni itakapopatikana wanasayansi watajua siri ya ‘dark matter’, watajua jinsi ulimwengu unavyofanya kazi na jinsi ulivyoumbwa na jibu la kitendawili cha ‘Standard Model’ litapatikana. Hiyo ni kazi ngumu. Ndiyo maana ‘Higgs boson’ mwaka 1993 iliitwa ‘The God Particle’. Yaani, wanasayansi wanahisi kuna muujiza wa Kimungu na huenda wasiipate kabisa hiyo bosoni. Wanasema waliipata mwaka 2013. Lakini hiyo waliyoipata bado ina utata. Kutokana na kushindwa huko kwa sayansi na historia, kutokana na kushindwa kwa sayansi kutengeneza binadamu au mnyama, kutokana na miujiza iliyorekodiwa katika vitabu vitakatifu; naamini, Mungu yupo.”

“Wanasayansi wana uwezo wa kupeleleza hadi kipindi cha karne ya kwanza ambapo Yesu aliishi, alikufa, alifufuka na alipaa kwenda mbinguni, na wana uwezo wa kujua mambo mengi kwa hakika yaliyofanyika katika kipindi hicho na hata katika kipindi cha kabla ya hapo. Kuna miujiza ambayo Yesu aliifanya ambayo haiko ndani ya Biblia. Kwa mfano, Biblia inasema Yesu alizaliwa ndani ya zizi la ng’ombe wakati sayansi inasema alizaliwa nje ya zizi la ng’ombe; na muujiza wa kwanza kuufanya ambao hauko ndani ya Biblia ni kutembea mara tu baada ya kuzaliwa, na watu na ndege wa angani kuganda kabla ya kuzaliwa Masihi na kabla ya wakunga kufika kumsaidia Maria Magdalena kujifungua. Akiwa na umri wa miaka sita, sayansi inasema, Yesu alikuwa akicheza na mtoto mwenzake juu ya paa la nyumba ya jirani na mara Yesu akamsukuma mwenzake kutoka juu hadi chini na mwenzake huyo akafariki papo hapo. Watu walipomsonga sana Yesu kwa kumtuhumu kuwa yeye ndiye aliyesababisha kifo cha mwenzake, na kwamba wangemfungulia mashtaka, Yesu alikataa katakata kuhusika na kifo hicho. Lakini walipozidi kumsonga, aliusogelea mwili wa rafiki yake kisha akamwita na kumwambia asimame. Yule mtoto alisimama! Huo ukawa muujiza mkubwa wa kwanza wa Yesu Kristo, kufufua mtu nje ya maandiko matakatifu. Kuna mifano mingi inayodhihirisha uwepo wa Mungu ambayo wanasayansi hawawezi hata kuipatia majibu. Tukio la Yoshua kusimamisha jua limewashangaza wanasayansi hadi nyakati za leo. Mwanzoni mwa miaka ya 70 wanasayansi walijaribu kurudisha muda nyuma kwa kompyuta kuona kama kweli wangekuta takribani siku moja imepotea kama ilivyorekodiwa katika Biblia. Cha kushangaza, cha kushangaza mno, walikuta saa 23 na dakika 20 zimepotea katika mazingira ambayo hawakuweza na hawataweza kuyaelewa. Walipochunguza vizuri walikuta ni kipindi cha miaka ya 1500 KK (Jumanne tarehe 22 Julai) ambacho ndicho tukio la Yoshua la kusimamisha jua na kusogeza mwezi nyuma digrii 10, ambazo ni sawa na mzunguko wa dakika 40, lilipotokea. Kwa kutumia elimu ya wendo, elimu ya kupanga miaka na matukio ya Kibiblia, dunia iliumbwa Jumapili tarehe 22 Septemba mwaka 4000 KK. Hata hivyo, mahesabu ya kalenda yanaonyesha kuwa Septemba 22 ilikuwa Jumatatu (si Jumapili) na kwamba kosa hilo labda lilisababishwa na siku ya Yoshua iliyopotea. Hayo yote ni kwa mujibu wa Profesa C. A. Totten, wa Chuo Kikuu cha Yale, katika kitabu chake cha ‘Joshua’s Long Day and the Dial of Ahaz: A Scientific Vindication and a Midnight Cry’ kilichochapishwa mwaka 1890. Kama hakuna Mungu iliwezekanaje Yoshua aombe jua lisimame na jua likasimama kweli? Iliwezekanaje Yesu aseme atakufa, atafufuka na atapaa kwenda mbinguni na kweli ikatokea kama alivyosema? Ndani ya Biblia kuna tabiri 333 zilizotabiri maisha yote ya Yesu Kristo hapa duniani na zote zilitimia – bila kupungua hata moja. Utasemaje hapo hakuna Mungu? Mungu yupo, naamini, sijui. Tukio la Yesu kufa, kufufuka na kupaa kwenda mbinguni si la vitabu vitakatifu pekee, hata sayansi inakubaliana na hilo.”

“Roho haina mifumo ya ufahamu! Haina pua, haina macho, haina ladha, haina harufu wala haina masikio. Kwa sababu roho haina mifumo ya ufahamu mtu, anapokufa mifumo yake yote 21 aliyokuwa nayo binadamu huoza na kuwa udongo. Hivyo, kuongea na mtu aliyekufa ni sawa na kuongea na udongo ukitegemea udongo huo ukusikie au uongee na wewe.”

“Nyota ni kipaji, kipawa, takdiri, karama, au uweza; ni kiashiria cha rohoni kinachoonyesha mtu atakuwa nani baadaye, mafanikio ya mtu, au takdiri ya maisha ya mwanadamu. Unabii na nyota ya ufalme ni kibali cha Mungu katika maisha ya mtu. Kupata kibali hicho, tembea na watu sahihi katika maisha yako (tembea na watu ambao Mungu amekuchagulia kushika funguo za takdiri ya maisha yako). Tamka na kukiri kibali cha Mungu katika maisha yako yote. Panda mbegu za kibali cha Mungu katika udongo wa maisha yako. Jifunze kutenda mema bila malipo, kwani wema ni mbegu ya kibali cha Mungu. Jali mambo ya ufalme wa Mungu.”

“Kila binadamu hapa duniani ni wa thamani kubwa. Chochote utakachofanya, kizuri au kibaya, kidogo au kikubwa, kitabadilisha maisha ya watu. Ukiwa na msingi mzuri kwa mwanao ataishi vizuri atakapokuwa mkubwa, atakuwa na uwezo mkubwa wa kuacha dunia katika hali nzuri kuliko alivyoikuta. Ukiwa na msingi mbaya kwa mwanao ataishi vibaya atakapokuwa mkubwa, atakuwa na uwezo mdogo wa kuacha dunia katika hali nzuri kuliko alivyoikuta. Kuwa mkarimu kwa mazingira, kuwa mkarimu kwa wanyama, kuwa mkarimu kwa binadamu wenzako, kwa faida ya vizazi vijavyo.”

“Hakuna shaka yoyote (kwa mfano) kwamba mboga za majani na matunda vina vitamini nyingi mwilini na madini na vitu vyote vizuri katika mwili wa binadamu, na kwamba kadhalika vina kirutubisho cha ufumwele ambacho huzuia kufunga choo na matatizo mengine ya mfumo wa usagaji chakula. Kirutubisho hiki kikizidi mwilini utapata matatizo makubwa yatakayoweza hata kukusababishia kifo!”

“Jina langu ni Enock Maregesi na ningependa kukwambia kisa kidogo kuhusiana na bibi yangu, Martha Maregesi. Mwanamke huyu alikuwa mke mwenye upendo usiokuwa na masharti yoyote. Alikuwa mama na bibi aliyefundisha familia yake umuhimu wa kujitolea na umuhimu wa uvumilivu. Ijapokuwa hakupendelea sana kujizungumzia mwenyewe, ningependa kukusimulia kisa kidogo kuhusiana na hadithi ya maisha ya mwanamke huyu wa ajabu katika maisha yangu. Bibi yangu alizaliwa katika Kitongoji cha Butimba, Kijiji cha Kome, Kata ya Bwasi, Tarafa ya Nyanja (Majita), Wilaya ya Musoma Vijijini, Mkoa wa Mara, katika familia ya watoto kumi, mwaka 1930. Alisoma katika Shule ya Msingi ya Kome ambako alipata elimu ya awali na msingi na pia elimu ya kiroho kwani shule yao ilikuwa ya madhehebu ya Kisabato. Aliolewa na Bwana Maregesi Musyangi Sabi mwaka 1946, na kufanikiwa kupata watoto watatu; wa kiume wakiwa wawili na wa kike mmoja. Matatizo hasa ya bibi yalianza mwaka 2005, alipougua kiharusi akiwa nyumbani kwake huko Musoma. Hata hivyo alitibiwa hapo Musoma na Dar es Salaam akapona na kuwa mwenye afya ya kawaida. Lakini tarehe 19/10/2014 alipatwa tena na kiharusi na kulazwa tena katika Hospitali ya Mkoa ya Musoma, ila akajisikia nafuu na kuruhusiwa kurudi nyumbani – lakini kwa maagizo ya daktari ya kuendelea na dawa akiwa nje ya hospitali. Tarehe 29/10/2014 alirudi tena Hospitali ya Mkoa ya Musoma kwa tiba zaidi, lakini tarehe 4/11/2014 saa 7:55 usiku akafariki dunia; akiwa amezungukwa na familia yake. Dunia ina watu wachache sana wenye matumaini na misimamo ya kutegemea mazuri, na wachache zaidi ambao wako tayari kugawa matumaini na misimamo hiyo kwa watu wengine. Nitajisikia furaha siku zote kwamba miongoni mwa watu hao wachache, hata bibi yangu alikuwemo. Msalaba uliwekwa wakfu na Mwenyezi Mungu baada ya mwili wa Yesu Kristo kuning’inizwa juu yake. Kwa kuwa bibi yangu ametanguliwa na msalaba, msalaba utamwongoza mahali pa kwenda.”

“Siri ya utajiri ni mawazo ya mtu. Maisha unayoishi uliyataka mwenyewe. Amka uishi. Hii ndiyo siri kubwa ya utajiri kuliko zote ulimwenguni. Ukifikiria chanya maisha yako yatakuwa chanya, ukifikiria hasi maisha yako yatakuwa hasi. Unachofikiria ndicho unachokuwa. Siri ya mafanikio yako ni jumla ya mambo unayoyawaza.”

“Kutakuwepo na nguvu za chanya na hasi katika maisha yako kadiri utakavyoishi hapa duniani. Ukiruhusu moyo wako kuwa chanya utakuwa chanya. Ukiruhusu moyo wako kuwa hasi utakuwa hasi. Shetani hawezi kuona ndani ya moyo wako mpaka wewe mwenyewe umwonyeshe. Ukionyesha chanya Mungu atakupa chanya. Ukionyesha hasi Shetani atakupa hasi.”

“Kutakuwepo na nguvu za hasi na chanya katika maisha yako kadiri utakavyoishi hapa duniani. Ukiruhusu mwili wako utawaliwe na hasi utakuwa hasi. Ukiruhusu mwili wako utawaliwe na chanya utakuwa chanya. Shetani hawezi kuona ndani ya moyo wako hadi wewe wenyewe umwonyeshe. Ukionyesha tamaa ya uzinzi atakupa uzinzi. Ukionyesha tamaa ya ulevi atakupa ulevi. Ukionyesha tamaa ya wizi atakupa wizi, na kadhalika. Kadiri utavyojitahidi kuwa chanya ndivyo utakavyozidi kuwa chanya; na kadiri utavyojitahidi kuwa hasi ndivyo utakavyozidi kuwa hasi. Usipambane na Shetani katika dunia hii ambapo yeye ndiye mtawala. Pambana na Shetani katika dunia ya kiroho ambapo Shetani hana nguvu yoyote dhidi ya Yesu Kristo.”

“Mapema, kabla ndege haijaondoka na baada ya kuagana na maafisa waliomsindikiza, Nanda aliingia katika ndege na kutafuta namba ya kiti chake. Alivyoiona, alishtuka. Msichana mrembo alikaa kando ya kiti (cha Nanda) akiongea na simu, mara ya mwisho kabla ya kuondoka. Alivyofika, Nanda hakujizuia kuchangamka – alitupa tabasamu. Alivyoliona, kupitia miwani myeusi, binti alitabasamu pia, meno yake yakimchanganya kamishna. Alimsalimia Nanda, harakaharaka, na kurudi katika simu huku Nanda akikaa (vizuri) na kumsubiri. Alivyokata simu, alitoa miwani na kumwomba radhi Kamishna Nanda. Nanda akamwambia asijali, huku akitabasamu. Alikuwa na safari ya Bama kupitia Tailandi, kwa ndege ya Shirika la Ndege la Skandinavia na Maxair kutokea Bangkok; sawa kabisa na safari ya kamishna.”

“Nukuu ya mwandishi wa vitabu wa Brazili, Paulo Coelho, "Tunapopenda tunajitahidi siku zote kuwa wazuri zaidi kuliko jinsi sisi wenyewe tulivyo. Tunapojitahidi kuwa wazuri zaidi kuliko jinsi sisi wenyewe tulivyo, kila kitu katika maisha yetu kinakuwa kizuri hali kadhalika.", inadhihirisha kikamilifu tabia ambayo bibi yangu (Martha Maregesi) alijitahidi kuwa nayo katika kipindi cha maisha yake yote. Alikuwa mtu mwenye furaha sana. Alikuwa na tabasamu lenye kuambukiza ambalo marafiki na familia yake hawakuweza kujizuia kutabasamu pia alipofurahi nao. Pamoja na kwamba alikumbana na matatizo mengi na bahati mbaya nyingi katika maisha yake, alijulikana kama mtu mwenye upendo na uvumilivu mkubwa.”

“Lakini, akiendelea kuwaza na kuangaza, ghafla Murphy aliona kitu kama gari likiwa limesimama kwa mbali. Alisimama na kupata hamu ya kujua. Murphy alianza tena kutembea, lakini sasa akiifuata ile gari, halafu akaongeza mwendo na kukimbia; macho yote yakiwa mbele! Alipofika, karibu na gari ile, hakuminya kifyatulio kumpiga mtu risasi. Alijenga tabasamu na kuongeza mwendo. Gari ilikuwa Ferrari Testarrosa ya Lisa Madrazo Graciano!”

“Pesa ina thamani pale unapokuwa nayo, si pale unapokuwa huna, hivyo iweke mahali unapoweza kuiona: katika nyumba, katika shamba au katika elimu. Badala ya kumpa mtu pesa ili ajenge nyumba, mpe nyumba. Badala ya kumpa mtu pesa ili afanye biashara, mpe biashara. Halafu, mpe elimu afanye maamuzi ya biashara yake. Pesa ina laana na Mungu pekee ndiye anayeweza kuiondoa laana hiyo. Ni rahisi kwa tajiri kupata baraka ya pesa kwa sababu ana pesa na ana uwezo mkubwa wa kusaidia maskini. Ni vigumu kwa maskini kupata baraka ya pesa kwa sababu hana au ana uwezo mdogo wa kusaidia maskini. Mungu anaweza kuondoa laana ya pesa kupitia hisani kwa maskini, kitu ambacho aghalabu hufanywa na matajiri wenye uwezo mkubwa. Heri kutoa kitu au huduma au elimu kwa maskini kuliko pesa.”

“Maombi ya sifa huunganisha watu wa Mungu na hutayarisha njia kwa ajili ya uwezo wa Mungu katika maisha yetu. Thamani ya maombi ya sifa wakati wa matatizo ni kuimarisha imani yetu, na kuwa karibu na Mungu wetu. Mungu anataka tumpe sifa na kumshukuru kwa kila jambo, kama Mtume Paulo anavyosema katika waraka wa kwanza wa Wathesalonike 5:16-18. Kumshukuru Mungu wakati wa matatizo ni amri, si ombi.”

“Kwa vile hatasamehewa, Shetani hatawasamehe wanadamu. Atahakikisha anauwa kila mtu duniani na kumpeleka kuzimu; ambako anaishi yeye, majini, malaika waovu, wana wa Mungu waliotumwa na Mungu kuja duniani kufundisha watu utukufu lakini wakaasi na Mungu akawalaani (au Wanefili) pamoja na nguva. Nguva ni uzao wa Wanefili na samaki wa baharini na malaika wauvu na wanapatikana zaidi katika Bahari ya Atlantiki, ambako mkuu wake ni Malkia wa Pwani, na katika Bahari ya Hindi ambako mkuu wake ni Malkia wa Bahari ya Hindi. Chini ya Bahari ya Hindi ndipo yalipo makao makuu ya ufalme wa giza hapa duniani.”