Quotessence
Home / Authors / Enock Maregesi

Enock Maregesi Quotes

Author

Filter quotes by topic

Famous Enock Maregesi Quotes

“The candle is the light of life that is constantly thriving to hang on and light up the darkness of life. Mwalimu Julius Kambarage Nyerere was a candle in the wind. He was a fighter fighting the odds to survive. And he did so with incredible power to change the world. Whether your life is long or short upon the earth, it is remarkable that our little flames burns on in spite of the wind, or the challenges of life.”

“Mandela alikuwa hodari ndiyo maana akapelekwa jela. Alikuwa mvumilivu ndiyo maana akakaa jela kwa miaka ishirini na saba. Alivyotoka akawa kiongozi bora wa Afrika Kusini. Utu ukafanya awasamehe binadamu wenzake. Urithi wa Nelson Mandela kwetu ni uhodari, uvumilivu, uongozi bora, utu na msamaha kwa binadamu wenzetu. Mandela alikuwa baba kwa familia yake. Kwa Afrika Kusini alikuwa mlezi wa ndoto, ya amani na uhuru.”

“Watu wanaohatarisha maisha yao kwa kudharau sheria wakati mwingine hawatakiwi kudharauliwa. Ni sawa na mtu aliyepoteza kila kitu katika maisha yake. Wana uwezo wa kufanya chochote. Serikali ya Meksiko ilipokataa kukidhi matakwa ya El Tigre ya kubadili katiba ya nchi – kuondoa kipengele cha mkataba wa kubadilishana watuhumiwa na washtakiwa – ili akikamatwa asipelekwe Marekani ambako atafungwa na kufia gerezani, El Tigre aliilaani Serikali ya Meksiko. Kujibu mapigo, ya laana ya maluuni, Serikali ya Meksiko ikawakabidhi makamanda 7 wa Kolonia Santita kwa mamlaka za Marekani, na kuongeza juhudi za kumsaka El Tigre mpaka nje ya Amerika ya Kusini na Kaskazini. El Tigre, kuikomoa serikali na kuwalipia kisasi makamanda wote waliouwawa na kufungwa na shirikisho, akamuua Mwanasheria Mkuu wa Serikali (PGR) na maafisa 7 wa Jeshi la Polisi la Nchi (PJF) kulinganisha idadi ya makamanda wake waliopelekwa Marekani – halafu 'akapotea', kabisa; baada ya kutangaza vita na Serikali ya Meksiko!”

“Mpelelezi wa Tume ya Dunia kutoka Jerusalem, Israeli, Kanali Daniel 'Yehuda Ben-Asher' Ebenezer, Daniel Yehuda, alikuwa komandoo wa kitengo cha mauti na utekaji nyara cha Shirika la Kijasusi la Mossad la Israeli (Kidon) kabla ya kujiunga na Kikosi Maalumu cha Kikomandoo cha Tume ya Dunia (EAC) huko Oslo, kwa makubaliano maalumu kati ya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa (UNSC) na Shirika la Kijasusi la Mossad la Israeli.”

“Kwa vile taifa la Israeli lilipoteza haki yake ya upendeleo, Mungu aliahidi kuliharibu kama alivyoyaharibu mataifa ya Waamori na Wamisri. Watu wa Israeli walishafika mbali sana kiasi cha Mungu kutokutegemea tena toba kutoka kwao. Kuna muda wa fursa na kuna muda ambao fursa haipo tena. Nafasi ya Israeli ya kutubu ilishafikia mwisho. Kama alivyokuwa amepigana vita vyao kwa ajili yao katika siku za nyuma sasa Mungu alipigana nao. Pamoja na ujasiri na utaalamu wao wote wasingependelewa tena. Mambo ambayo mwanzo yaliipa Israeli nguvu katika vita yaliwageukia.”

“Ukanda wa Gaza ni jimbo lenye miji minne na kambi mbalimbali za wakimbizi za Umoja wa Mataifa – lenye urefu wa kati ya kilometa 41 au maili 25 na lenye upana wa kati ya kilometa 6 mpaka 12 au maili 3.7 mpaka 7.5, pamoja na eneo la jumla la kilometa za mraba 365 au maili za mraba 141. Jimbo hili liliwahi kutawaliwa na Wamisri, Wakaanani, Waisraeli, Wasiria, Wababelonia, Wagiriki, Warumi, Waturuki, Waingereza, na Wapalestina, na limekuwa uwanja wa vita kwa karne nyingi kwa sababu za kidini na kihistoria. Ukanda wa Gaza uko chini ya Palestina. Uko chini ya serikali ya Hamas.”

“Shetani anajua kwamba sisi ni warithi wa wokovu na kwamba dunia hii ni kitu kilichoahidiwa kwa Ibrahimu na watoto wake. Sisi wote ni watoto wa Ibrahimu. Anajua kabisa kwamba baadaye sisi ndiyo tutakaokuwa watawala halisi wa dunia hii. Hivyo, anajitahidi kwa kadiri ya uwezo wake wote ili hilo lisitokee. Shetani na malaika wake ni wengi sana, na wanatumia kila silaha waliyokuwa nayo kutawala dunia.”

“Kofia za chuma au sandarusi zenye uwezo wa kukwepesha risasi za wadunguzi na kuzuia mpaka risasi tatu za AK-47, ijapokuwa zimetengenezwa kuzuia risasi moja tu, ni miongoni mwa vitu 17 vilivyobebwa na makomandoo wa Tume ya Dunia; wakati wakitekeleza Operesheni ya Kifo au Ushindi Kamili (operesheni ndogo ya Operation Devil Cross ya Tume ya Dunia) katika Msitu wa Benson Bennett, Salina Cruz, Oaxaca, nchini Meksiko. Thamani ya vitu vya komandoo mmoja wa EAC ('Executive Action Corps') akiwa vitani ni zaidi ya dola za Kimarekani 65,000; ikiwa ni pamoja na magwanda ya jeshi ('Ghillie Suits'), kofia za chuma, miwani ya kuonea usiku (yenye uwezo wa kubinuka chini na juu), redio na mitambo ya mawasiliano migongoni mwao juu ya vizibao vya kuzuia risasi, vitibegi vya msalaba mwekundu ('Blowout kits' – katika mapaja ya miguu yao ya kulia, ndani yake kukiwa na pisto na madawa ya huduma ya kwanza), vitibegi vya kujiokolea ('Evasion Kits' – katika mapaja ya miguu yao ya kushoto, ndani yake kukiwa na visu na pesa na ramani ya Meksiko) na bunduki za masafa marefu.”

“Vitibegi vya makomandoo wa Tume ya Dunia (vitibegi vya msalaba mwekundu na vitibegi vya kujiokolea) vilikuwa na vifaa maridadi vya kisasa kama vile pisto, visu, madawa ya huduma ya kwanza, kalamu za Inka, ramani za Meksiko, tochi ndogo zenye mwanga mkali za Cyba-Lite, Vioo vya TOPS, vibiriti vya Firesteel, pasi za kusafiria, pesa na vipenga vyenye viwango vya sauti vya desabo 126. Kipenga chenye kiwango cha sauti cha desabo 126 kinaweza kupasua ngoma za masikio ya adui, na kuwajulisha Vijana wa Tume mwenzao alipo hivyo kwenda haraka na kumpa msaada.”

“XM29 OICW ni bunduki iliyowasaidia Vijana wa Tume kubomoa jengo la utawala la Kolonia Santita katika Kiwanda cha Dongyang Pharmaceuticals jijini Mexico City, iliyowasaidia kukamata baadhi ya wakurugenzi wa Kolonia Santita kabla hawajatoroshwa na walinzi wao makomandoo. Bunduki hii inayotumia teknolojia ya OICW ('Objective Individual Combat Weapon') iliyotengenezwa na Kiwanda cha Heckler & Koch cha Ujerumani, ina uwezo wa kufyatua makombora ya HEAB ('High Explosive Air Bursting') yenye ukubwa wa milimeta 20; ambayo hulipuka hewani kabla ya kugonga shabaha, kwa lengo la kusambaza vyuma vya moto katika eneo lote walipojificha maadui. Bunduki hizi hazitumiki tena. Zilitumika mara ya mwisho mwaka 2004.”

“Kuamini (mbali na imani, ambayo ni nia ya kujua kisichoweza kujulikana) ni kwa ajili ya vitu usivyoweza kuvielezea. Unaamini kwamba siku moja dawa ya UKIMWI au saratani itapatikana mahali fulani, ilhali huwezi kufanya majaribio ya kisayansi kulithibitisha hilo. Unaweza kusubiri hata miaka mia, lakini kama bado dawa haijapatikana, unaweza kusubiri hata miaka mingine mia. Kuamini ni kujifanya kujua (na mara nyingi kujifanya kujua ni uongo) na kuamini hakuhitaji maarifa. Kujua kunahitaji maarifa na ni kuamini unakoweza kukuthibitisha. Ukiniuliza kama simu yangu ipo mfukoni nitakwambia ndiyo ipo, kwa sababu nitaingiza mkono mfukoni na kuitoa na kuiona. Siamini kama ipo mfukoni, najua.”

“Kolonia Santita ilikuwa na tani 627.54 za madawa ya kulevya ilizokuwa imezikusanya kwa siri kwa muda wa miezi 9 mfululizo. Ilikuwa imepanga kuzisafirisha ndani ya siku 10 baada ya kutokea kwa mauaji ya Tijuana-San Diego, katika mpaka wa Meksiko na Marekani; kwenda Asia, Afrika, Amerika, Ulaya na Australia, kabla ya kukamatwa na Mamlaka ya Kudhibiti Madawa ya Kulevya na Ugaidi wa Kimataifa Duniani WODEA. Kokeini tani 183, heroini tani 90, methamfetamini tani 81, eksitasi tani 27.54 (vidonge milioni 110.16). Bangi tani 186, uyoga wa kichawi tani 60. Madawa hayo yalikuwa na thamani ya mtaani ya shilingi za Kitanzania trilioni 12.9.”

“Kila sumu ina kiuasumu chake. Viuasumu vya 'cyanide' ni 'amyl nitrite', 'sodium nitrite', 'cyanokit', na 'sodium thiosulfate'. Kazi ya viuasumu hivi ni kuzalisha madini mengi ya chuma mwilini. Madini haya yatapambana na maada za rangi za uhai ('cytochromes') kwa ajili ya 'cyanide', ili 'cyanide' ing’ang’anie kwenye kiuasumu badala ya kung’ang’ania kwenye vimeng’enya vya seli za mwilini. Kiuasumu kinaposhinda mpambano huo; 'cyanide' hutolewa nje kwa njia ya mkojo, na mwathirika wa 'cyanide' hupona kabisa. 'Sodium thiosulfate' ndiyo bora zaidi kuliko 'amyl nitrite' au 'sodium nitrite', na ndiyo bora zaidi kuliko 'cyanokit'.”

“Kuna ndoto za mchana na kuna ndoto za usiku. Ndoto za mchana ni maono ya kile ambacho roho inatamani kuwa. Ndoto za usiku ni maono yanayotokea wakati akili imetulia baada ya mwili wote kupumzika. Ukiota kuhusu moto, hiyo ni ishara ya hasira; ukiota kuhusu maji, hiyo ni ishara ya siri; ukiota kuhusu ardhi, hiyo ni ishara ya huzuni; ukiota kuhusu Yesu, hiyo ni ishara ya mafanikio. Kitu cha kwanza kufanya unapoota ndoto za kishetani, utakapoamka, mwombe Mungu akunusuru kutoka katika matatizo yoyote yanayokunyemelea; au yanayomnyemelea mtu mwingine yoyote yule, hata usiyemjua. Ubongo ni kitu cha ajabu kuliko vyote ulimwenguni na umetengenezwa na Mungu. Ndoto zinapatikana ndani ya ubongo. Ubongo unapatikana ndani ya ufahamu. Ufahamu mtawala wake ni malaika mwema. Malaika mwema anajua siri ya ndoto. Kila mtu anaota na kila ndoto ina maana yake. Rekodi ndoto zako kila siku kwa angalau mwezi mzima kupata maana halisi ya ndoto hizo, na kujua kwa nini ulizaliwa.”

“Maisha tunayoishi ni mafupi, maisha ya mbinguni ni ya milele. Fundisha familia yako upendo na hofu ya Mungu, kwani hiyo ndiyo akili kushinda zote. Hekima ya kutunza familia inapatikana katika kitabu cha Mithali cha Agano la Kale.”

“Ikiwa huna pesa na una mke na watoto kwa mfano, mke wako (wanawake walio wengi) hatakuona wa maana kwa sababu ya ustawi wa maisha ya familia yake. Ikiwa una mwanamke asiyekuwa na busara au hekima ya kutosha, au mwanamke ambaye akili zake zimefyatuka kidogo, atakusaliti kutafuta bwana au mtu mwenye maana. Kama huna pesa huna maana kwa mwanamke.”

“Shetani hawezi kusoma ndani ya mioyo ya wanadamu mpaka wanadamu wenyewe wamwonyeshe. Ukionyesha tamaa ya ngono, Shetani atakupa ngono. Ukionyesha tamaa ya ulevi, Shetani atakupa ulevi. Ukionyesha tamaa ya wizi, Shetani atakupa wizi. Ukionyesha tamaa ya chuki, Shetani atakupa chuki. Ukionyesha tamaa ya upendo, Mungu atakupa upendo. Kama kuna ubishi kati ya moyo wako na akili yako, fuata moyo wako.”

“Kama ulikuwa ukimwambia mwanao kuwa atakuwa jambazi labda kwa sababu ya fujo zake alipokuwa mdogo, mambo mengi atakayokuwa anayafikiria au anayaota atakapopevuka akili ni ya kihalifu. Kwani hayo ndiyo mambo ya kwanza kabisa kujirekodi katika ubongo wake alipokuwa hajitambui. Lakini kama ulikuwa ukimwambia kuwa atakuwa daktari au mwanasheria, mambo mengi atakayokuwa anayafikiria au anayaota ni ya kidaktari au kisheria. Kuna uwezekano mkubwa akawa daktari au mwanasheria baadaye katika maisha yake.”

“Ufalme wa mbinguni uko juu. Akili ya binadamu iko juu. Kupata Amri Kumi za Mungu, Musa alipanda juu katika mlima Sinai. Yesu alijaribiwa na Shetani akiwa juu katika jangwa la Yuda. Ukifanikiwa tunasema uko juu. Tai hawezi kuona vizuri akiwa chini anaweza kuona vizuri akiwa juu. Ulaya na Amerika tunaita majuu kwa sababu ziko juu ya ikweta. Kwa nini juu? Kwa sababu juu kuna utukufu.”

“Tovuti za miadi (‘dating sites’) hutumia ‘optimal stopping’ kuwachagulia watu wachumba wao. Wanachofanya ni kwamba wanachagua watu 100. Wanaondoa 37% ya kwanza ya wale ambao sifa zao haziendani na sifa unazozitaka. Kisha wanakuchagulia mtu waliyeona ni bora zaidi kuliko wote waliobakia. Huyo waliyekuchagulia anaweza kuwa mke au mume bora. Lakini Mungu ana mipango yake. Unaweza kushangaa mke au mume bora akatoka kwenye 37% ya wale walioachwa.”

“Upendeleo na msamaha ni sumu na baraka ya usuluhishi miongoni mwa watu kwa mpangilio huo. Yaani, upendeleo ni sumu ya usuluhishi, msamaha ni baraka ya usuluhishi. Usuluhishi wenye msamaha, usiokuwa na upendeleo wowote, ni dawa ya uhusiano mwema miongoni mwa watu. Upendeleo ni sumu ya usuluhishi – Msamaha ni kiuasumu cha usuluhishi.”

“Maombi yako yasipojibiwa usikate tamaa, Mungu alishakusikia na tayari alishaandaa malaika wa kukuletea jibu. Jibu wakati mwingine huchelewa kufika kwa sababu ya nguvu za giza. Usiwe na haraka, muda wako ukifika utajibiwa.”

“Meli ya kwanza kuondoka katika Bandari ya Salina Cruz kusini mwa Meksiko katika Bahari ya Pasifiki ni 'La Diosa de los Mares', 'Mungu wa Bahari', au 'Goddess of the Seas', Tani 6000, iliyoondoka saa tisa kamili usiku kuelekea Miami nchini Marekani; wakati ya mwisho kuondoka ilikuwa CSS ('Colonia Santita of the Seas', Tani 10000), na SPD ('El Silencio Depredador del Profundo', 'Mnyama Mtulivu wa Kina Kirefu', 'The Silent Predator of the Deep' – nyambizi ya Panthera Tigrisi), zilizoondoka saa kumi na moja alfajiri kuelekea Guatemala na Kolombia. Salina Cruz ni sehemu iliyopo kandokando mwa Bahari ya Pasifiki kusini kabisa mwa Meksiko na kaskazini-mashariki kwa Reparo Jicara katika jimbo la Oaxaca. Kambi ya Panthera Tigrisi ilijengwa ndani ya Msitu wa Benson Bennett – katika ufuko wa bahari kubwa kuliko zote ulimwenguni, iliyopuliza hewa na kuyumbisha miti anuai juu ya maabara kubwa kuliko zote katika Hemisifia ya Magharibi; ya kokeini, heroini, bangi, eksitasi na hielo ya China na Kolombia. Panthera Tigrisi alikamatwa katika Bahari ya Pasifiki. Kahima Kankiriho alikamatwa katika Msitu wa Bennett.”

“Kiswahili ni lugha rasmi ya nchi za Tanzania, Kenya na Uganda. Ni lugha isiyo rasmi ya nchi za Rwanda, Burundi, Msumbiji na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo. Lugha ya Kiswahili ni mali ya nchi za Afrika ya Mashariki, si mali ya nchi za Afrika Mashariki peke yake. Pia, Kiswahili ni lugha rasmi ya Umoja wa Afrika; pamoja na Kiarabu, Kiingereza, Kifaransa, Kireno na Kihispania. Kiswahili ni lugha inayozungumzwa zaidi nchini Tanzania kuliko nchi nyingine yoyote ile, duniani.”