Quotessence
Home / Authors / Enock Maregesi

Enock Maregesi Quotes

Author

Filter quotes by topic

Famous Enock Maregesi Quotes

“Kama umeamua kuoa au kuolewa ukiwa na umri wa kati ya miaka 18 na 40, kulingana na kanuni ya kuachana na ukapera (‘optimal stopping’) umri wa kuwa na msimamo kuhusiana na mtu utakayeoa au kuolewa naye ni baada tu ya kufikisha umri wa miaka 26. Kabla ya hapo kuna uwezekano ukakosa wachumba bora, baada ya hapo wachumba bora wanaweza kuanza kupotea, hivyo kukupunguzia uwezekano wa kumpata mke au mume aliye mwema.”

“Hakuna mahali popote katika Agano Jipya ambapo sheria ya Sabato imekomeshwa (Kutoka 31:12-17), kwani Mungu alianzisha Sabato kwa ajili ya wanadamu wote (Marko 2:27). Kinyume cha hapo, Yesu aliitunza (Luka 4:16), Paulo aliitunza (Matendo 17:2) na Wamataifa waliitunza pia (Matendo 13:42-44; 16:13)! Mwandishi wa Waebrania anaandika bila kificho, “Basi, imesalia raha ya Sabato kwa watu wa Mungu” (Waebrania 4:9).”

“Soma sana. Andika sana. Ongea na watu kuhusu mambo ya muhimu unayoyafikiria. Tumia intaneti na maktaba kwa makini kwa ajili ya utafiti, kwa sababu habari nyingi za intaneti na maktaba haziaminiki. Kama una wazo kichwani mwako lizungumze kwa watu kama mazungumzo ya kawaida, ili upate maoni yao ya dhati, bila kusahau kuandika kwa siri wazo lolote jipya utakalolipata kutokana na mazungumzo hayo. Maana Mungu anaweza kuwasiliana na mtu mwingine yeyote yule akupe wazo, litakaloongeza maana zaidi katika mawazo ambayo tayari unayo.”

“Maana halisi ya ukarimu si kutoa vitu au mali nyingi kwa watu wanaohitaji msaada, bali ni kutoa vitu au mali hizo bila kinyongo au unafiki wowote. Ukarimu unapaswa kutolewa kwa watu sahihi, wakati sahihi, kiasi sahihi na kwa moyo mmoja bila kinyongo chochote. Ukitoa kwa lengo la kupata faida, huo ni ubinafsi na unafiki mkubwa.”

“Mwili wako una uwezo wa kujua kabla yako kitakachotokea baadaye. Kama una njaa kwa mfano, mwili wako utakwambia. Kama una kiu, mwili wako utakwambia. Kama unaumwa, mwili wako utakwambia. Kama kuna kitu kibaya kinatarajia kutokea katika maisha yako au katika maisha ya mtu mwingine, mwili wako utakwambia. Kuwa makini na alamu zinazotoka ndani ya mwili wako, kwani hizo ni ishara za Roho Mtakatifu kukuepusha na matatizo ya dunia hii.”