Quotessence
Home / Authors / Enock Maregesi

Enock Maregesi Quotes

Author

Filter quotes by topic

Famous Enock Maregesi Quotes

“Kiswahili ni lugha ya Kibantu na lugha kuu ya kimataifa ya biashara ya Afrika ya Mashariki ambayo; maneno yake mengi yamepokewa kutoka katika lugha za Kiarabu, Kireno, Kiingereza, Kihindi, Kijerumani na Kifaransa, kutoka kwa wakoloni waliyoitawala pwani ya Afrika ya Mashariki katika kipindi cha karne tano zilizopita. Lugha ya Kiswahili ilitokana na lugha za Kisabaki za Afrika Mashariki; ambazo nazo zilitokana na Lugha za Kibantu za Pwani ya Kaskazini Mashariki za Tanzania na Kenya, zilizotokana na lugha zaidi ya 500 za Kibantu za Afrika ya Kusini na Kati. Lugha za Kibantu zilitokana na lugha za Kibantoidi, ambazo ni lugha zenye asili ya Kibantu za kusini mwa eneo la Wabantu, zilizotokana na jamii ya lugha za Kikongo na Kibenue – tawi kubwa kuliko yote ya familia ya lugha za Kikongo na Kinijeri katika bara la Afrika. Familia ya lugha za Kikongo na Kibenue ilitokana na jamii ya lugha za Kiatlantiki na Kikongo; zilizotokana na familia ya lugha za Kikongo na Kinijeri, ambayo ni familia kubwa ya lugha kuliko zote duniani kwa maana ya lugha za kikabila. Familia ya lugha ya Kiswahili imekuwepo kwa karne nyingi. Tujifunze kuzipenda na kuzitetea lugha zetu kwa faida ya vizazi vijavyo.”

“Ujanja wote ulimwisha Murphy. Ilimbidi kutoboa siri ili adui asizidi kumuumiza. Alilaumu mno kufa wakati alishakula ng’ombe mzima. Alifikiri Mogens na Yehuda walishauwawa kulingana na hasira nyingi za magaidi. Walihakikisha hawafanyi makosa hata kidogo. Alivyomaliza kumhoji, yule adui alizunguka nyuma katika mgongo wa Murphy na kwenda katika dirisha lililokuwa wazi – la mashariki – ambapo aliegemea na kuvuta sigara. Alichungulia kidogo nje kisha akageuka na kuendelea kupata upepo mdogo wa baridi.”

“Murphy hakupenda kupoteza muda. Alinyanyuka na kumimina risasi, Mungu akamsaidia akadondosha wawili huku wengine wakipotea kwa kuruka vibaya na kukwepa. Kwa kasi Murphy alikimbia huku ameinama mpaka katika milango mikubwa ya nje, ambayo sasa ilikuwa wazi. Hapo akasita. Chochote kingeweza kumpata kwa nje kama hangekuwa mwangalifu. Bunduki yake ilishakwisha risasi. Aliitupa na kuchungulia nje akaona adui mmoja akikatisha kwenda nyuma ambako ndiko mashambulizi yalikokuwa yakisikika sasa. Murphy hakumtaka huyo. Aligeukia ndani kuona kama kulikuwa na bunduki aichukue lakini hata kisu hakikuwepo. Akiwa bado anashangaa, ghafla alitokea adui – kwa ndani – na kurusha risasi, bahati nzuri akamkosa Murphy. Murphy, kama mbayuwayu, aliruka na kusafiri hewani hapohapo akadondoka nyuma ya tangi la gesi karibu na milango ya nje. Alipoona vile, adui alidhani Murphy alidondoka mbali. Alibung’aa asijue la kufanya. Wasiwasi ulipomzidi alishindwa kuvumilia. Alishika bunduki kwa nguvu na kupiga kelele, "Yuko hukuuu!" Halafu akajificha ili Murphy asimwone. Lakini Murphy alikuwa akimwona.”

“Shetani anatisha. Ana macho makubwa manane: macho ya serafi, macho ya mwanadamu, macho ya simba na macho ya tai, na ana mabawa makubwa sita yenye urefu wa futi sita mpaka nane kila moja. Ana rangi ya bluu, bluu iliyoiva, ambayo ni sehemu kubwa ya rangi ya kuzimu, na macho makubwa kama nguva wa Afrika. ‘Mtu’ wa namna hiyo akikwambia njoo nikupige kojoa kwanza ndiyo uende. Kukaa karibu na ‘mtu’ wa namna hiyo ni kujitafutia matatizo makubwa. Kuepukana naye, usiwe mkristo wa Shetani, usiwe mkristo wa kanisa, usiwe mkristo wa dini, kuwa Mkristo wa Yesu Kristo. Kwa maneno mengine, usiwe mkristo wa kufuata bendera, usiwe mkristo wa kinafiki – kuwa Mkristo wa kweli.”

“Watoto hupenda vitu vinavyong’aa ambavyo havijatulia na vilivyopangiliwa vizuri. Hivyo ndivyo macho ya binadamu yalivyo: yana unyevu na yanaakisi mwanga, hayajatulia, na yana rangi kadha wa kadha ikiwa ni pamoja na kope na vigubiko vya macho ambavyo pia hazijatulia. Mtoto mchanga hasa yule anayeona vizuri huangalia macho pale anapopata nafasi, kwa maana ya kuyashangaa. Vilevile, huangalia macho kwa maana ya kupokea molekuli ya maadili au homoni inayorahisisha maisha kutoka kwa mama yake iitwayo ‘oxytocin’. ‘Oxytocin’ husisimua ubongo wake na kuutayarisha kupokea neno lolote litakalosemwa na mama yake mzazi au mama yake mlezi.”

“WWPP ('WODEA Witness Protection Programme') ni Programu Maalumu ya Ushahidi ya Tume ya Dunia ya kuwakinga mashahidi wa kihalifu kwa kuwapa makazi mapya, majina mapya, kazi mpya, historia mpya ya maisha, na sura mpya, kuwakinga na Sheria ya Kitalifa ya Kolonia Santita. Ukivunja Sheria ya Kitalifa ya Kiapo cha Swastika cha Kolonia Santita utauwawa, tena utauwawa kinyama, wewe na familia yako.”

“Kila mtu kabla ya kuzaliwa alipewa na Mwenyezi Mungu unabii na nyota ya ufalme. Una bahari ya fursa ya kuwa kitu chochote unachotaka kuwa katika dunia hii. Kama unataka furaha, furaha iko ndani yako. Kama unataka utajiri, utajiri uko ndani yako. Kama unataka amani, amani iko ndani yako. Kama wewe ni tone na fursa ni bahari, wewe ni bahari ndani ya tone.”

“Kama George Bush angekuwa na amani ndani ya moyo wake na Saddam Hussein angekuwa na amani ndani ya moyo wake Vita ya Ghuba isingetokea. Vilevile, katika kitabu cha ‘Kolonia Santita’, kama Rais wa Tume ya Dunia angekuwa na amani ndani ya moyo wake na kiongozi wa Kolonia Santita angekuwa na amani ndani ya moyo wake Kolonia Santita isingepigana na Umoja wa Mataifa. Taifa lisingepigana na taifa, na mataifa yasingepigana na magaidi.”

“Lakini ukweli ni upi? Ukweli ni kwamba utajiri una changamoto nyingi kuupata na kuudumisha pia kuliko usomi na kwamba ukweli ni amani ya Mungu katika moyo wa mwanadamu. Heri msomi kuliko tajiri – Heri yule aliyesoma kuliko tajiri asiyesoma au yule aliyesoma kuliko vile alivyosoma tajiri au tajiri asiyesoma au aliyesoma lakini asiyekuwa na tamaa kabisa na dunia hii ambaye kukosa kwake tamaa na dunia hii kunamfanya msomi. Ndivyo Kristo anavyomaanisha. Si kwamba tajiri hawezi kuuona ufalme wa mbinguni. Ibrahimu, Isaka, Yakobo, Yusufu, Daudi, Sulemani, Yehoshafati, Hezekia, Zakayo, Yoana, Susana, na Lidia watauona ufalme wa mbinguni na walikuwa matajiri. Mali zao zilivyozidi hawakuangalia moyoni, hawakuwa na tamaa kabisa na dunia hii, bali walimtumaini Mungu kwa kila kitu walichokuwa nacho. Anaweza. Lakini asiipende dunia bali ayapende mambo ya ufalme wa Mungu kwa moyo wake wote.”